Mbowe: Wabunge wamejiongezea Mishahara Kutoka Tsh milioni 13 za awali na sasa wanalipwa Tsh milioni 18 kwa mwezi mbali na posho

Manake kwa siku moja mbunge analipwa laki sita. Hii ni kufuru..mei mosi ikifika wengine wanaambiwa uchumi haujakaa vizuri..bado tuna miradi mingi inayohitaji fedha..shabaaashhh..wacha nisijetamka laana.
 
Romani Catholic.
Mwashambwa wewe ni Roman Catholic!! Ngumu sana kuamini.

Kama ni Roman Catholic, unafuata mafundisho ya nani?

Mama Kanisa aliagiza kuwa kutokana dhuluma nyingi zinazofanywa maeneo mbalimbali Duniani, na zaidi dhuluma hizo zinafanywa zaidi na watawala, Kanisa la karne hii ni lazima lisimame na watu wanaoonewa na watawala. Wewe mbona siku zote upo kwaajili ya kuwatetea watawala, tena ambao, muda mwingine ni dhahiri kabisa, matendo yao yanadhulumu haki za watu wanyonge? Au umeamua kuasi mafundisho ya Kanisa?

Hii ni kwaresma, ni wakati wa tafakari. Kama Kristo, kutokana na upendo wake kwetu, alikubali kuutoa uhai wake kwaajili yetu, sisi tunajitoleaje kwaajili ya watu wengine, hasa wanaoonewa, wanaodhulumiwa, na waliopo katika dhiki, ili kuuishi upendo wa Kristo?

Kristo, ....
 
Swali la kijinga.

Hivi hata ukiwa ni wewe umeingia bungeni, ukakuta mshahara ni huo, utaacha kuupokea? Na ukiuacha itasaidia nini?

Lakini ukiingia huko, ukakuta mshahara ni huo, na ukaona kwa kuzingatia uhalisia wa nchi, siyo halali. Ukautangazia umma kwa uwazi, tayari umetimiza wajibu wako. Wanaotakiwa kuchukua hatua ni wenye pesa yao, ambao ni wananchi. Kama wao wanaona ni halali mbunge achukue 26m kwa mwezi na Rais 50m kwa mwezi, basi hakuna wakubadilisha.
Mwananchi gani anaweza kubadilisha mshahara wa mbunge?😆
 
Wanafanya wanavyotaka si wanawajua waTanzania ni watu wa kubweka bweka lakini hawachukui hatua........

Watawala ni kama wanasimamia mochwari.......
Ukitaka kujua wabunge hawatuwakilishi,wamepitisha sheria inayowapa mamlaka maafisa wa usalama wa taifa kutoa uhai watanzania bila kushtakiwa.

wamepitisha bajeti ya manunuzi ya ndege mpya ya rais.
 
Vyama vya wafanyakazi angalie nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma.
 
Mbowe kaongea kitu sahihi ila kinafiki sana kwasababu inamuuma kuwa nje ya bunge. Ninatumaini uchaguzi 2025 utakuwa huru na wa haki ili nao waingie bungeni kutafuna keki ya nchi. Wabunge huwa kitu kimoja bila kujali vyama linapokuja suala la maslahi yao.
Acha ujinga basi. Kwa hiyo wewe wabunge wanapojirundikia mishahara minene huku wananchi wakifa njaa kwa umasikini wewe unaaona sawa tu?
 
mwakani na mimi nagombea kama kurogana tutarogana tu natafuta uchawi wa kenya nigeria yemen urusi malawi zimbabwe togo madagaska msumbiji uganda kongo nachanganya wote kwa pamoja niwapige juju wajumbe kwenye jimbo langu nyau nyie
 
Kwani ukiwa chawa kuna ulazima wa kujipoteza akili? Taifa limeshidwa kuajiri wataalam wa sector mbalimbali ikiwemo walimu na madaktari ambao hawatoshelezi kwa ukosefu wa fedha, unashadadia wabunge kujilipa kiasi hicho cha fedha?
And that is my problem

Alipovuta yeye? Alikua chawa

Sasa huko nje? Wengine chawa

We don’t need wajilipe makubwa whether aseme mbowe au mzee wa mihogo
 
Vyama vya wafanyakazi angalie nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma.
Vyama vya wafanyakazi vip?😅😅Mei mosi mnapata t-shirt wale wa VIP wanapata T-shirt na mwamvuli wa ju.


Hao hawawezi kukutetea hata siku moja ,wanalipana mishahara mara mbili mbili ni utapeli ...Ukiwa na kesi yako kazini tafuta wakili ila hao hawasogei hata usipolipwa overtime ,utaambiwa serikali haina pesa.

Fuatilia nyuzi humu watu wamefukuzwa makazini bila ya utaratibu ila wanapambana wenyewe haki zao ,ila wanachangia kweny vyama vya wafanyakazi.
 
Hivi hata Uingereza nako watu kushabikia sana mpira kuna athari kwa nchi?
Nazani umeona wabunge wa uingereza walivyonamsimamo hata kama ni kama ni kiongozi wa Chama ukienda tofauti na malengo wanaacha kukuunga mkono sababu ya shinikizo kutoka kwa wananchi wao viongozi wanaamua kujiuzuru
 
Back
Top Bottom