Mbowe: Tupeni madaraka kwa masharti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe: Tupeni madaraka kwa masharti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Aug 20, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amewataka Watanzania kukiweka kando Chama cha Mapinduzi (CCM) na badala yake wakichague CHADEMA kwa masharti kwamba kikishindwa kusimamia masilahi yao nacho kiondolewe.
  Alisema ni makosa makubwa kwa wananchi kufikiria kuwa CCM ndicho baba na mama yao, hivyo kuwataka wakinyime kura katika chaguzi mbalimbali kwa kuwa kimeshindwa kuwaondolea kero zao.
  Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, alitoa kauli hiyo juzi jioni katika Kata ya Hembeti, jimboni Mvomero, mkoani Morogoro, alipozuiliwa kwa muda na wananchi wakitaka awahutubie.
  Alisema kuwa kwa sasa wananchi wanapaswa kuachana na CCM badala yake wakichague CHADEMA lakini akaweka bayana kuwa endapo nacho kitashindwa kusimamia masilahi yao, kiwekwe pembeni.
  “Mimi Mbowe leo nikiona CHADEMA haiendani na mahitaji ya wananchi na kushindwa kuongoza, sitakuwa na sababu ya kuendelea kuwa mwana-CHADEMA, sasa ninyi mnang’anga’nia CCM kwa nini?” alihoji huku akishangiliwa na wakazi hao.
  Mbowe alipita eneo hilo akitokea mjini Dodoma alikokuwa akihudhuria vikao vya Bunge, akielekea Kata ya Mtibwa mkoani humo, kuungana na viongozi wenzake katika operesheni ya vuguvugu la mabadiliko ( M4C) ndipo akazuiliwa kwa muda katika Kata ya Hembeti ambako kulikuwa na mkutano wa chama hicho.
  Mkutano huo ambao ulikuwa ukihutubiwa na Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Hamad Yusuph, ulisimama kwa muda huku wananchi wakizuia gari la Mbowe lisiendelee na safari wakitaka awahutubie.
  Hali hiyo ilimlazimu kada wa chama hicho, Arcado Ntagazwa, aliyekuwa akihutubia kumpa kipaza sauti Mbowe kwa ajili ya kusalimia umati huo.
  Akihutubia mkutano huo, Mbowe alisema kuwa dhamira ya CHADEMA kuwapo mkoani Morogoro ni kuwaondoa wananachi wa mkoa huo katika wimbi la usingizi wa kuishabikia serikali ya CCM aliyodai imeshindwa kutatua matatizo ya msingi ya nchi.
  “Tunapita kila kata ya Mkoa wa Morogoro kujenga mtandao wa chama bila kujali dini, kabila wala rangi, ujumbe wangu kwa wana-Hembeti ni kujua wajibu wa chama cha siasa ni kupata viongozi na sera mbadala zitakazowezesha nchi kusonga mbele,” alisema Mbowe.
  Mbowe aliongeza kuwa serikali ya CCM imeshindwa kuwatoa watu katika matatizo na kuwapeleka katika neema huku akiwataka wakazi hao kutafakari miaka 50 ya Uhuru imewafikisha wapi.
  Alisema kuwa Mkoa wa Morogoro umefunga ndoa na CCM, hali inayowafanya wasiwe na sauti ya moja kwa moja hadi matatizo yao yaongelewe na wabunge wa vyama vya upinzani kutoka maeneo mengine.
  “Tunawaunganisha wana CCM, CUF na vyama vingine na wengine katika kuikomboa Tanzania, tunawaomba msiwacheleweshe wakazi wa mikoa mingine katika kusonga mbele kwa kuwa ninyi mmefunga ndoa na Chama cha Mapinduzi,” aliongeza.
  Naye Ntagazwa, akihutubia katika vijiji vya Kambala, Hembeti na Mkindo kunakokaliwa na jamii ya wafugaji na wakulima, alisema migogoro ya ardhi nchini inakuzwa kwa makusudi na watawala kwa vile wana masilahi nayo.
  Alisema watendaji na watawala wa serikali ya CCM badala ya kuwakutanisha wakulima na wafugaji kwa ajili ya kuondoa tofauti zao wao hutumia fursa hiyo kuchukua fedha kwa mmoja wao na kisha kuacha uhasama miongoni mwa wafugaji na wakulima.
  “Msidhani matatizo yenu yanashindwa kutatuliwa ila huo ni mradi wa watu kwa maana leo ng’ombe wa mfugaji akiingia katika shamba la mkulima na akapelekwa kwa mtendaji kwa ajili ya kulipwa fidia, mtendaji anachukua fedha kwa mfugaji na mkulima, hali inayomfanya mfugaji aendelee kuwa na kiburi cha fedha na mkulima awe na uchungu wa kuharibiwa mali yake,” alisema Ntagazwa.
   
 2. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Ntagazwaa!! hivi lazima na wewe uendelee kuwa mwanasiasa? siamini maneno na viongozi wa siasa, maneno yao yanapambwa katika kumtia ujinga mwananchi.Uwajibikaji si katika utawala wa nchi tu bali hata kwa ngazi ya ubunge,udiwani n.k labda swali kwa Mh Mbowe uliyoyaahidi katika jimbo lako la Hai utekelezaji wake uko vipi? Ulisema unarudisha gari la kiongozi wa upinzani bungeni na picha ukapiga ukifanya matembezi ya mshikamano leo unapiga nalo misele, tafadhalini ebu tafuteni cha kutuambia watanzania hatutaki kuwaita wababaishaji.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu Mbowe ndio peupe namna hii? Dah!

  Yeye mwenyewe ana madaraka makubwa sana kama kiongozi wa upinzani bungeni, ana mawaziri kivuli kibao, anashindwa kuwaingiza wawatumikie wananchi? anashindwa kuisimamia Serikali kwa wadhifa alionao? anataka madaraka yepi tena?
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  zomba, you do not understand the government position, and shadow ministries too!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Aliyoyasema mh Mbowe kwa wananchi Hembeti hayaendani na aina ya uongozi wake, ana kila dalili ya kuwa kiongozi wa kiimla endapo atakuwa kiongozi mwenye mamlaka ya dola.
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  You and I are the government, I may not know what is your knowledge about governing as you seem to be so shallow in your judgement on my understanding of the government(s). I simply know that I and any other citizen are the government, without you and me and the others how can you have "the" so called government? What would we govern? cats and dogs?

  I may also give you the lessons on shadows if you have the capacity, but based on your comments, I doubt.
   
 7. B

  Benaire JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,947
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mihimili mitatu ya taifa ni bunge,serikali na mahakama.......kwa maana hiyo mimi sio serikali coz anaeniwakilisha ni mbunge.....unapozungumzia serikali,moja kwa moja ni Central government....ila unapozungumzia utendaji kazi wa serikali,ndio tunasema unaanzia kwa mwananchi wa kawaida "local government".....Kamwe waziri kivuli sio kiongozi wa serikali that's why hata Rais akiwa anahutubia atasema serikali ya CCM...
  Cha msingi anachohubiri ni mabadiliko,yaani kuchange the whole system but under incumbent government...they find it difficult since they are few and democracy goes with the majority!
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Zomba bana, Malawi wewe.....

  [​IMG]
  [​IMG]

   
 9. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ngoja nitafute like mzee
   
 10. m

  makundi4619 JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 486
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mamlaka gani zaidi ya kuwa kiongozi wa upinzani? CDM haijashika dola. Usiwe na haraka ngoja CDM iwe na mamlaka kamili ya kuendesha dola ndipo utakapoelewa anachokizungumzia kwa sasa ni vigumu kwa wengi kuelewa. Wewe wape CDM kura yako 2015 uone kazi.
   
 11. m

  makundi4619 JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 486
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thank you for an elaborate answer.
   
 12. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Utawezaje kuleta maendeleo kama dola si yako!!!!! Mmhhhh, mtu mzima na ndevu mpaka miguuni lakini mawazo ni chekechea. Hasara gani hii, ptuuuuuuu!
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Anashika dola za kimerekani kila siku pale bilicanas. Kama mnategemea kushika dola, sijui ya wapi maana Tanzania msahau kabisa. Kura za Kaskazini tena za zamani, zinawatosha kupewa Tanzania? Maweee!
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nyie ndio wenye hasara mnaofikiri maendeleo yanaletwa na madaraka ya kuwa na dola. Ukiwaa fikra zenu ndio hizo? hata mshushiwe malaika hamtoendelea.
   
 15. MsemajiUkweli

  MsemajiUkweli JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 8,911
  Likes Received: 12,091
  Trophy Points: 280
  Ukweli husemwa:

  Kingcobra, Maendeleo hayaletwi na dola tu. Tatizo kuu hapa nchini ni wanasiasa kupotosha ukweli na watu wengi kuamini kile wakisemacho
  Mihimili mikuu mitatu ndiyo inayoleta maendeleo ya nchi nawe ukiwa ni chachu ya hayo maendeleo.(Bunge, serikali na mahakama)

  Huwezi kukaa tu chini ukitegemea hivi vyombo vitakuleletea maendeleo katika familia yako.
   
 16. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dola mtu anapewa au unahangaika kuitafuta, huyu jamaa kweli punguani anawaomba dola watu wa kijijini huenda hata hiyo dola yenyewe kuiona hawajaiona.
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hio ni kauli safi sana ,na hapo wananchi umewapa uhuru wa kuchagua ,hongera Mbowe kwa kauli hiyo.
   
 18. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Zomba, sidhani kama uko serious kwa hili! Naamini ni joke!
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Stick to the point zomba, I said you still not understand the responsibilities of the shadow ministries in the government, and ofcourse you do not understand the responsibilities of your government!

  The Shadow Cabinet is a senior group of opposition spokespeople in the system of government who together under the leadership of the Leader of the Opposition form an alternative cabinet to the government's, whose members shadow or mark each individual member of the government. Members of a shadow cabinet are often but not always appointed to a Cabinet post if and when their party gets into government. It is the Shadow Cabinet's responsibility to pass criticism on the current government (NOT TO MAKE DECISION) and its respective legislation, as well as offering alternative policies.

   
 20. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #20
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  He is not joking, based on his understanding capacity, the guy is real serious! shallow
   
Loading...