Mbowe: Tupeni madaraka kwa masharti

You and I are the government
Untrue and 100% lie
A body of people that sets and administers public policy, and exercises executive, political, and sovereign power through customs, institutions, and laws within a state. In parliamentary systems, the government is composed of the prime minister and the cabinet. In other cases, "government" refers to executive, legislative, judicial, bureaucratic, and possibly also devolved powers.
Mimi na wewe akina kajambanani tuko wapi?


 
You can drive a donkey the liver but you cannot force it to drink water!
You are wasting your time; Zomba has no clue about the government and is not eager to learn.

what foolish english is this?do u know the meaning of the liver?kwanini usiandike kwa kiswahili kuficha aibu zako ndugu yangu,
 
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amewataka Watanzania kukiweka kando Chama cha Mapinduzi (CCM) na badala yake wakichague CHADEMA kwa masharti kwamba kikishindwa kusimamia masilahi yao nacho kiondolewe.
Alisema ni makosa makubwa kwa wananchi kufikiria kuwa CCM ndicho baba na mama yao, hivyo kuwataka wakinyime kura katika chaguzi mbalimbali kwa kuwa kimeshindwa kuwaondolea kero zao.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, alitoa kauli hiyo juzi jioni katika Kata ya Hembeti, jimboni Mvomero, mkoani Morogoro, alipozuiliwa kwa muda na wananchi wakitaka awahutubie.
Alisema kuwa kwa sasa wananchi wanapaswa kuachana na CCM badala yake wakichague CHADEMA lakini akaweka bayana kuwa endapo nacho kitashindwa kusimamia masilahi yao, kiwekwe pembeni.
“Mimi Mbowe leo nikiona CHADEMA haiendani na mahitaji ya wananchi na kushindwa kuongoza, sitakuwa na sababu ya kuendelea kuwa mwana-CHADEMA, sasa ninyi mnang’anga’nia CCM kwa nini?” alihoji huku akishangiliwa na wakazi hao.
Mbowe alipita eneo hilo akitokea mjini Dodoma alikokuwa akihudhuria vikao vya Bunge, akielekea Kata ya Mtibwa mkoani humo, kuungana na viongozi wenzake katika operesheni ya vuguvugu la mabadiliko ( M4C) ndipo akazuiliwa kwa muda katika Kata ya Hembeti ambako kulikuwa na mkutano wa chama hicho.
Mkutano huo ambao ulikuwa ukihutubiwa na Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Hamad Yusuph, ulisimama kwa muda huku wananchi wakizuia gari la Mbowe lisiendelee na safari wakitaka awahutubie.
Hali hiyo ilimlazimu kada wa chama hicho, Arcado Ntagazwa, aliyekuwa akihutubia kumpa kipaza sauti Mbowe kwa ajili ya kusalimia umati huo.
Akihutubia mkutano huo, Mbowe alisema kuwa dhamira ya CHADEMA kuwapo mkoani Morogoro ni kuwaondoa wananachi wa mkoa huo katika wimbi la usingizi wa kuishabikia serikali ya CCM aliyodai imeshindwa kutatua matatizo ya msingi ya nchi.
“Tunapita kila kata ya Mkoa wa Morogoro kujenga mtandao wa chama bila kujali dini, kabila wala rangi, ujumbe wangu kwa wana-Hembeti ni kujua wajibu wa chama cha siasa ni kupata viongozi na sera mbadala zitakazowezesha nchi kusonga mbele,” alisema Mbowe.
Mbowe aliongeza kuwa serikali ya CCM imeshindwa kuwatoa watu katika matatizo na kuwapeleka katika neema huku akiwataka wakazi hao kutafakari miaka 50 ya Uhuru imewafikisha wapi.
Alisema kuwa Mkoa wa Morogoro umefunga ndoa na CCM, hali inayowafanya wasiwe na sauti ya moja kwa moja hadi matatizo yao yaongelewe na wabunge wa vyama vya upinzani kutoka maeneo mengine.
“Tunawaunganisha wana CCM, CUF na vyama vingine na wengine katika kuikomboa Tanzania, tunawaomba msiwacheleweshe wakazi wa mikoa mingine katika kusonga mbele kwa kuwa ninyi mmefunga ndoa na Chama cha Mapinduzi,” aliongeza.
Naye Ntagazwa, akihutubia katika vijiji vya Kambala, Hembeti na Mkindo kunakokaliwa na jamii ya wafugaji na wakulima, alisema migogoro ya ardhi nchini inakuzwa kwa makusudi na watawala kwa vile wana masilahi nayo.
Alisema watendaji na watawala wa serikali ya CCM badala ya kuwakutanisha wakulima na wafugaji kwa ajili ya kuondoa tofauti zao wao hutumia fursa hiyo kuchukua fedha kwa mmoja wao na kisha kuacha uhasama miongoni mwa wafugaji na wakulima.
“Msidhani matatizo yenu yanashindwa kutatuliwa ila huo ni mradi wa watu kwa maana leo ng’ombe wa mfugaji akiingia katika shamba la mkulima na akapelekwa kwa mtendaji kwa ajili ya kulipwa fidia, mtendaji anachukua fedha kwa mfugaji na mkulima, hali inayomfanya mfugaji aendelee kuwa na kiburi cha fedha na mkulima awe na uchungu wa kuharibiwa mali yake,” alisema Ntagazwa.

katika mabaki yaliyooza kabisa na hayafai kusikika tena katika jamii ya watanzania ni pamoja na ntagazwa.
 
Nasoma mara mbili mbili hainiingii akilini,.we cant put life our into a test.hata siku moja., wachaga acheni kuwadanganya watanzania.
 
Tumewajaribu kwa kuwapa halmashauri kadhaa hapa nchini mmeshindwa vibaya matokeo yake ni migogoro ya mameya wenu kutuhumiwa kwa ufisadi.majaribio gani zaidi mwataka,mpaka mtunyonye na damu?
 
Manispaa ya moshi ambayo iko chini ya chadema imechoka kweli,mna mbunge tangu 95 ameishia kujenga uzio wa makaburi tu.acheni uongo wenu mbowe
 
Hivi huyu Mbowe ndio peupe namna hii? Dah!

Yeye mwenyewe ana madaraka makubwa sana kama kiongozi wa upinzani bungeni, ana mawaziri kivuli kibao, anashindwa kuwaingiza wawatumikie wananchi? anashindwa kuisimamia Serikali kwa wadhifa alionao? anataka madaraka yepi tena?

Ndugu yangu nasikitika kusema mawazo yako au yameganda au huna ufahamu wa nini maana ya serikali kivuli.
Serikali kivuli haikusanyi kodi,wala kujiamulia mambo,bali serikali iliyopo madarakani ndo inaruhusiwa kisheria kufanya hayo. nikuulize uliwahi kuona kivuli kinapigwa picha? japokuwa ukiwa mahali ukaona kivuli kinakupa wazo la kwamba kuna kitu fulani.
Tumeshuhudia mara nyingi wabunge wa upinzani wakitoa hoja nzito lakini serikali inazijibu kwa majibu rahisi na spika wa bunge anaridhia,sasa hapo Mbowe afanye nini,Nani aliwahi kuona bunge likiridhia bajeti kivuli mojawapo itumike kama bajeti rasmi ya wizara husika tukaona ikishindwa kutimiza matakwa ya watanzania? Badala yake tumeshuhudia wabunge wa NINYIM wakisema bajeti hizo hazitekelezeki.Na ninyi mmekariri mtu akionyesha kutoridhika mnapiga simu kwa spika kwamba bunge la sasa halina maadili.Huu ni wakati Wtz tubadilishe fikira zetu
Tusubiri tuihukumu CDM baada ya kuipa madaraka rasmi ikakusanya kodi alafu ikashindwa kuleta maendeleo kwa wananchi.Watanzania tukumbuke kwamba vyama vyote vya siasa vina haki ya kutuongoza watanzania na hakuna chama chenye hati miliki ya kuongoza watanzania wakati wote hata kwa kutuburuza kwa kutumia vyombo vya dola.Kamanda Mbowe yuko sahihi CDM ipewe madaraka ikishindwa kuendesha nchi kama ilivyo NINYIM,tuiwajibishe.hiyo ndio demokrasia.
 
what foolish english is this?do u know the meaning of the liver?kwanini usiandike kwa kiswahili kuficha aibu zako ndugu yangu,
Haya ni matokeo ya NINYIM kutudanganya kwamba kiswahili ni lugha ya taifa wakati watoto wenu mnawasomesha nje ya nchi ili mje mtutawale kwa mtindo wa ''Bandua baba,bandika mtoto" Tujue kiingereza vizuri tusijue,ukweli ni kwamba siku zenu zinahesabika.Angalieni mfano wa Gaddafi na Mubarak wa Misri walidhani wakiwakabidhi madaraka watoto wao watawalinda lakini nguvu ya umma imewapeleka mahali pabaya.
 
Dola mtu anapewa au unahangaika kuitafuta, huyu jamaa kweli punguani anawaomba dola watu wa kijijini huenda hata hiyo dola yenyewe kuiona hawajaiona.

hakyanani wewe ndo PUNGUANI, asipoitafuta dola kwa kuwaomba wananchi, unataka aitafute kwa kuingia msituni?? au wewe kwa upunguani wako, unadhani dola ni nini?? labda nikusaidie kidogo, dola hapa ni mamlaka ya nchi na sio aina ya fedha kama ile ya kimarekani. jitahidi upunguani ukupungue.
 
Nasoma mara mbili mbili hainiingii akilini,.we cant put life our into a test.hata siku moja., wachaga acheni kuwadanganya watanzania.

Read the above red, then refer to your own comment below!

what foolish english is this?do u know the meaning of the liver?kwanini usiandike kwa kiswahili kuficha aibu zako ndugu yangu,
 
Nasoma mara mbili mbili hainiingii akilini,.we cant put life our into a test.hata siku moja., wachaga acheni kuwadanganya watanzania.

Acha kudanganya watu wewe, mbona umeyaweka kwenye majaribio kwa muda wote wa miaka 50 tangu uhuru?? kama umeweza kwa miaka yote hiyo 50, unashindwa nini kubadili mwelekeo??? kama pamoja na kufikiri mara mbilimbili, bado umeona hili ndo la kuzungumza, nakuhurumia sana, si ajabu nyie ndo mnaopewa chumvi na t-shirt za njano halafu mnaishia kuwachagua mafisadi hawa kuchukua madaraka.
 
Acha kudanganya watu wewe, mbona umeyaweka kwenye majaribio kwa muda wote wa miaka 50 tangu uhuru?? kama umeweza kwa miaka yote hiyo 50, unashindwa nini kubadili mwelekeo??? kama pamoja na kufikiri mara mbilimbili, bado umeona hili ndo la kuzungumza, nakuhurumia sana, si ajabu nyie ndo mnaopewa chumvi na t-shirt za njano halafu mnaishia kuwachagua mafisadi hawa kuchukua madaraka.

Bado hajakomaa, amejiunga juzi tu hana hata wiki, and for sure, he/she is still very young in politics
 
Untrue and 100% lie
A body of people that sets and administers public policy, and exercises executive, political, and sovereign power through customs, institutions, and laws within a state. In parliamentary systems, the government is composed of the prime minister and the cabinet. In other cases, "government" refers to executive, legislative, judicial, bureaucratic, and possibly also devolved powers.
Mimi na wewe akina kajambanani tuko wapi?



Nakuona hata huelewi unachokisoma, wewe katika hayo makundi yote haupo? basi si binaadam wewe. Haupo kwenye insitutions wala laws? ikiwa haupo hata kwenye "devolved powers"? wala haupo kwenye kuwa governed? duh!

Ndio maana Tanzania haiendelei, kwani mtu kama wewe hau exist ingawa tuko pamoja kwenye nchi hii hii, Serikali hii hii, watu hawa hawa. Pole sana kwa kutokujijuwa wala kujitambuwa.
 
Back
Top Bottom