MPIGA ZEZE
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 2,539
- 2,297
Tupo pamoja nanyi Kamanda. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa zima kwa wote wanaopenda demokrasia. Kitendo kilichofanywa Arusha si UGAIDI dhidi ya CHADEMA bali ni UGAIDI dhidi ya DEMOKRASIA. Ninaamini Watanzania walio wengi - wawe ni wafuasi wa CCM, CDM, CUF, TLP, na wasiojinasibisha na vyama - wangependa kuona DEMOKRASIA inakua. kama hivyo ndivyo, basi huu ni msiba wetu wote. Tuoneshe mshikamano kama taifa kwa kulaani vikali vitendo kama hivi vinavyokusudia ku-terrorize wananchi wasiwe huru kujumuika katika mijumuiko ya kisiasa kuunga mkono itikadi yo yote wanayochagua au kidini kushiriki katika imani walizochagua. Nasema tena huu ni UGAIDI DHIDI YA DEMOKRASIA na ulaaniwe na kila mpenda demokrasia. Waliotangulia RIP na waliojeruhiwa tunawaombea Muumba awarejeshee afya zenu mapema.