Mbowe: SMG bastola zilitumika Arusha

Mbowe: SMG bastola zilitumika Arusha

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
1,060
Reaction score
309
MWENYEKITI wa CHADEMA Freeman Mbowe, amevituhumu vyombo vya dola kuwa vinawafahamu watu walioshiriki kwenye mlipuko
wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa chama hicho. Mbowe, alisema tukio hilo ni la kupangwa na
wamegundua risasi za bunduki aina ya SMG na bastola zilitumika mara baada ya mlipuko huo jambo linalozusha hofu na kudidimiza demokrasia ya vyama vingi.

Wakati Mbowe akitoa tuhuma hizo kwa vyombo vya dola, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema ameunda timu itakayoongozwa na makamishna wawili (Paul Chagonja na Isaya Mungulu), kwenda mkoani Arusha kuongeza nguvu ya uchunguzi. Akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani hapa, Mbowe alisema uchunguzi wa awali walioufanya wamebaini tukio hilo ni la kisiasa na
lilipangwa. Alisema ni vema serikali ikatangaza kuachana na mfumo wa vyama vingi kuliko kuruhusu mauaji na vurugu katika mikutano ya vyama vya upinzani vinavyoonekana kutoa wakati mgumu kwa watawala.

Aliongeza kuwa uchunguzi wa awali katika eneo la tukio umebaini bomu lililolipuliwa ni la kiwandani na si la kutengenezwa. Alisema katika eneo la tukio maganda ya risasi kutoka katika bunduki ya SMG na bastola yalikutwa hali inayowafanya waamini kuna watu waliamua kufanya tukio hilo kwa kupanga.

Mbowe alisema risasi hizo pia ni miongoni mwa zilizopigwa kwenye tanki la mafuta la gari la matangazo la CHADEMA ambapo zililitoboa. Alibainisha kuwa inavyoonekana wahusika walitaka kuzalisha mlipuko mwingine mkubwa na kuleta maafa makubwa katika mkutano huo. "Haihitaji uchunguzi wa kwenda mwezini katika suala hili, ni wazi walipanga kutuua lakini wakaua watu wasiohusika. Waliouawa hawakuwa katika mpango wao na wamekuwa wahanga kwa niaba yetu.

"Hata kama utaamua kumuua Mbowe au (Godbless) Lema, huwezi kuiua CHADEMA kwani chama kitabaki, na wanachama wengine
wataendeleza harakati za chama kama kawaida," alisema. Wabunge kutohudhuria Bunge Mbowe alisema kutokana na tukio hilo ambalo limeua watu zaidi ya watatu, CHADEMA imeamua kulifanya ni la kitaifa na wabunge wake watashiriki kwenye maombolezo.

Alisema kuanzia leo wabunge wote wa CHADEMA hawatahudhuria vikao vya Bunge na watajumuika mkoani Arusha hadi misiba yote itakapomalizika. Alisema wanatarajia kufunga mahema katika eneo la tukio na marehemu wote wataagwa katika eneo hilo ambapo ibada zote za Kiislamu na Kikristu zitafanyikia hapo. IGP aunda timu Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwema ameunda timu ya kuongeza nguvu ya uchunguzi itakayoongozwa na makamishna wawili ambao ni Paul Chagonja kutoka idara ya operesheni na Isaya Mngulu kutoka ofisi ya upelelezi makao makuu.

IGP Mwema alisema baada ya tukio hilo, jeshi hilo lilituma makamishna wawili kutoka makao makuu kwa ajili ya kuongeza nguvu ya uchunguzi wa tukio hilo na kwamba wameshaanza kukusanya taarifa mbalimbali zitakazoweza kusaidia kuwabaini watu waliohusika. Alisema wameunganisha nguvu na vyombo vingine vya ulinzi na watawasaka wahalifu hao pamoja na walio nyuma yao kwa kile alichoeleza tukio hilo linaashiria kushamiri kwa matendo ya kigaidi nchini.

Akizungumzia tuhuma zinazotolewa na wananchi juu ya Jeshi la Polisi kuwajeruhi watu kwa risasi za moto, IGP Mwema alisema kila taarifa inafanyiwa kazi kwa umakini na kwamba baada ya uchunguzi watatoa taarifa kamili kwa umma juu ya kilichotokea jijini Arusha. Aliwaomba wananchi wenye taarifa za kuweza kumtambua aliyerusha bomu pamoja na watu walio nyuma yake wajitokeze au wamtumie ujumbe kupitia simu yake ya mkononi namba 0754 78 55 57 na kwamba uhusika wao utafanywa kuwa siri.

IGP Mwema pia alisema watachunguza kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bara, Mwigulu Nchemba liyowaambia wakazi wa Kimandolu kuwa wasipoichagua CCM katika uchaguzi wa madiwani wa Jiji la Arusha ulioahirishwa jana, watakufa. Mwema alisema watachunguza kauli hiyo baada ya kuulizwa swali la hatua zilichochukuliwa kabla na baada ya mlipuko huo dhidi ya kauli ya Nchemba.

Juzi katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani kwa CHADEMA uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, kitu kinachodhaniwa ni bomu kilipuka na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.
 
ujumbe kupitia simu yake ya mkononi namba 0754
78 55 57 na kwamba uhusika wao utafanywa kuwa
siri. IGP Mwema pia alisema watachunguza kauli ya
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
bara, Mwigulu Nchemba aliyowaambia wakazi wa
Kimandolu kuwa wasipoichagua CCM katika
uchaguzi wa madiwani wa Jiji la Arusha
ulioahirishwa jana, watakufa. Mwema alisema watachunguza kauli hiyo
baada ya
kuulizwa swali la hatua zilichochukuliwa kabla na
baada ya mlipuko huo dhidi ya kauli ya Nchemba. Juzi katika mkutano wa kufunga kampeni za
udiwani kwa CHADEMA uliofanyika kwenye viwanja
vya Soweto, kitu kinachodhaniwa ni bomu kilipuka
na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.[/QUOTE]

Kinacho nishangaza ni uchunguzi wa Kauli ya Mwigulu hapa kinachotakiwa kufanywa ni kumchukulia hatua muhusika wa kauli hiyo kwani kauli hiyo haiwezi kupindishwa kamwe na kwa mtazamo wangu Mwigulu anatakiwa awe mshitakiwa namba moja. wengine watafuata
 
tuko pamoja sana kamamda wetu katika wakati huu mgumu kamanda usichoke kuwatumikia wananchi wako tuko pamoja
 
Bwana Mbowe tafuteni wafadhili muirushe Ibada hii tuangalie nchi nzima kupitia Star TV au ITV huu ni msiba wa kitaifa maana serikali ya CCM wanataka kuiangamiza demokrasia.
 
Kinacho nishangaza ni uchunguzi wa Kauli ya Mwigulu hapa kinachotakiwa kufanywa ni kumchukulia hatua muhusika wa kauli hiyo kwani kauli hiyo haiwezi kupindishwa kamwe na kwa mtazamo wangu Mwigulu anatakiwa awe mshitakiwa namba moja. wengine watafuata

Embu fikiria kidogo tu, mfano kauli hii angeitoa Lema sijui angekuwa selo gani. Hapo ndipo tunapolichoka jeshi letu la polisi na tambo zake za polisi jamii.
 
wadau namba ya simu ya IGP SAID MWEMA naiweka vizuri muione ni hii: 0754 78 55 57
kwa wanaowajua wahusika wajaribu kumtumia IGP message, kisha tuone ujasiri wa polisi wa kuwashughulikia wahusika wa unyama huu.
 
Mwingulu chemba aliyeachiwa nchi na kuuvaa ugenerali ndiye haswa. Mweama huhitaji kupepesa macho. Somebody took your powers unceremoniously . Sijui kama inteligensia yenu inawapaga uwezo wa kuona mambo in the inteligent way. Ncehmba ni rebel. Take from me. Once CCM is out, the man will go into the forests.
 
Kinacho nishangaza ni uchunguzi wa Kauli ya Mwigulu hapa kinachotakiwa kufanywa ni kumchukulia hatua muhusika wa kauli hiyo kwani kauli hiyo haiwezi kupindishwa kamwe na kwa mtazamo wangu Mwigulu anatakiwa awe mshitakiwa namba moja. wengine watafuata

hata mimi nimeshindwa kuelewa kwamba kauli huwa inachunguzwa vipi....kauli ipo na ndivyo alivyosema mwigulu hakuna kuichunguza hapo ni kumkamata tu
 
another mwigulu thug shit, it was a tongue slip Mwema can not go after this government authorized untouchable gangstar.
 
Kila roho inayotoka Tanzania kuhusiana na siasa, Mwigulu yupo connected.
Na kama ye Mwigulu ndo anatoa order kwa Mwema inashangaza ni vipi Mwema aanzeje kuchunguza kauli from above.
Unless Mwigulu is nudged down from the peking order we'll continue to witness brutal killings and tortures of innocents
 
Last edited by a moderator:
msiba pole arusha,pole CHADEMA,pole tanzania
hii ni mkakati wa kuzima wadai mabadiliko lkn ninacho nisikitisha mm yakitokeaa zanzibar wengi humu huwa wrong side husimama kuupinga ukweli na wapingania mabadiliko wa zanzibar hufanywa magaidi wanaostahili kejeli na dharau na hujuma...wengi kwa kujua au kuto kujua husaidia ukandamizaji znz kwa maneno yao na kusahau kuwa ni mbinu za kuzima upizani mfano utasikia CUF,UAMSHO hao wanachoma makanisa,kuuwa padri wengi wetu huripuka tu na kushabikia bila kudadisi....kwa njia fulani tunasaidi ukandamizaji wa mawazo tafauti na ya watawala....leo tunaambiwa CDM ni chama cha kigaidi(viongozi wake wanashtakiwa kwa ugaidi).......RABDA NI ADHABU KWA KUWA NA SURA MBILI ....''USIPO MUUNGA MKONO MWEZIO AKIPIGANIA HAKI YAKE IKIFIKA ZAMU YAKO UTAKUWA PEKE YAKO''
MAY I BE WRONG BUT ALWAYS CLEAR
 
Emmanuel Nchimbi ni waziri wa mambo ya ndani na ni mjumbe wa kamati kuu CCM, Mwigulu Nchemba ni naibu katibu mkuu wa CCM, sijui IGP Mwema na timu yako mnatoa wapi ujasiri wa kumchunguza Mwigulu?
 
Mbona huku mtaani hata mkiwa wawili ukamwambia mwenzio NITAKUUA Polisi wakiripotiwa wanakukamata mara moja?vipi Mwigulu aliyesema hadharani wanasema watachunguza kauli yake? Au wanachunguza kauli hiyo ilitokea kwenye kiungo gani cha mwili?
 
Hakuna hatua ya maana itakayochukuliwa na polisi wala serikali zaidi ya siasa tu cha muhimu ni wananchi kuiadabisha ccm tu
 
Hizo SMG ndizo alifauta china ili magharibi wasiwe na serial number?Wachina watatuua sana ili magamba wahonge nchi ili wabaki madarakani.Na uatajiri uliopo unawaumiza sana roho CCM.
 
Mwingulu chemba aliyeachiwa nchi na kuuvaa ugenerali ndiye haswa. Mweama huhitaji kupepesa macho. Somebody took your powers unceremoniously . Sijui kama inteligensia yenu inawapaga uwezo wa kuona mambo in the inteligent way. Ncehmba ni rebel. Take from me. Once CCM is out, the man will go into the forests.

Pray for him to live another five years
 
Back
Top Bottom