Waandike uongo kwa makusudi ili baadae wapoteze muda wa watu makini kukanusha. Ndiyo strategy mpya iliyoko mtamboni?
Chonganisha Mbowe na Slaa, tapeli wajumbe wa mikutano kwa kuwasainisha fomu 'feki' mkidanganya zimetoka Makao Makuu ya Chama, chonganisha wajumbe, chonganisha wanachama na chama chao, chonganisha, chonganisha, sema uongo, sambaza uongo...ndiyo strategy iliyoko mtamboni?
Ndani ya CHADEMA si suala la 'mtu kutaka' wala 'mtu kupinga vikali', ni misingi kutaka na kupinga vikali. Wanaotaka chama kisimame kwenye matakwa ya mtu ndiyo wanaoeneza uongo kama huu. Lengo nini? CHADEMA kuna mgogoro!
Hakuna mgogoro kuna kusimamia nidhamu na kujenga imani ya wananchi ambao wana matumaini makubwa na chama chao.
Hii ya kuwachonganisha Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake mbona haijaanza leo, bado mnahisi inaweza kufanikiwa na kuzaa matunda?
Ndani ya CHADEMA msingi wa masuala yote ni Katiba, Kanuni, taratibu, maadili na miongozo. Si mtu. Kama watu wanaamini hawajavunja misingi ya CHADEMA wasiwasi wote huu unatoka wapi hadi kuzusha maneno ya uongo mkavu kama huu.
Ndani ya CHADEMA, Katiba, kanuni, maadili, taratibu na miongozo ndiyo itampenda au kumchukia mtu yeyote. Si suala la mtu fulani kumpenda au kumchukia fulani.
Hakuna kitu kama hicho. Labda kama hata walioandika hawajui maana ya 'maamuzi ya kikao'...