Mbowe, Slaa Watofautiana kuhusu Zitto...

Status
Not open for further replies.
Nchaby, pole sana kijana. Achana na porojo za wapuuzi, hakuna mjumbe hata mmoja ndani ya kamati aliye tayari kutetea usaliti au utovu wa nidhamu ndani ya chama bila kujali uzito wa mhusika. Tofauti ya Chadema na CCM ni kama ya mchana na usiku respectively, if you know what I mean...that's why people love Chadema!

Huyu atakua hajui au anaongea kufurahisha mabwana zake Lumumba Mag3 hajui tu watu wanavyoipigania Chadema kwa moyo kwa ajili ya maslahibya nchi akiwemo yeye mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
Mpaka sasa ZK amtakuwa au anatakiwa awe amejua kuwa 'team zitto' na spin projects zake hazitafanikiwa. Si rahisi kupambana na public opinion ambayo mara zote huwa sahihi. Mara hii ni public knowledge kwamba ZK ni msaliti mwenye ndoto kubwa kuliko upeo wake. Utetezi kuwa sijui alichukua kadi akiwa na miaka 16 eti wengine wakiwa CCM au kwamba ana jasho na damu CDM vinadhihirisha alivyo na fikra finyu. Je ZK anafikiri hivyo ni vigezo vinavyohalalisha usaliti?, anapodai kuwa CDM ni wahafidhina je anakijua chama chochote ambacho kingeweza kumruhusu na kumvumilia kwa alichokifanya? Mimi sio mwamanachama wa chama chochote cha siasa lakini ZK amenivunja moyo sana. Kwa nini anataka kuvutana na chama cha wahafidhina? Kwa nini asiachane nao? Hakumbuki Nyerere aliwaambia CCM kwamba chama hicho si mama yake? Hizi sarakasi zake zinalenga nini? Au ni kwa sababu 'mission is not complete' kwa mujibu wa mpango kazi na hivyo anataka ku-justify jambo fulani? Mpaka leo ZK bado hajatoa maelezo yoyote juu ya 'waraka wa siri' ila amekimbilia mahakamani kuzuia mjadala huo lakini kama ambavyo Chenge amehukumiwa na umma kuwa ni fisadi hata ZK umma sa haumuamini. Walikuwepo wengi wa aina yake na sasa wamebaki historia kujificha nyuma ya ukabila na ukigoma hakutamsaidia in the long run. Je amewahi kumuona jamaa yake Kabourou akifanya kazi za CCM taifa? ZK ni obsessed kuwa kwenye limelight lakini hajui njia sahihi namsikitikia kwa namna anavyohangaika kuiwekea shinikizo CDMkwa njia za kitoto kabisa. It is time he moves on, trying to pull CDM down with him is never going to happen,CCM with all its resources has failed and a traitor like ZK will not be able to do it even with the backing of his masters.
 
Huku katibu mkuu Dk Slaa akitaka zitto arudishiwe nafasi zake zote ndani ya Chama Mwenyekiti amepinga vikali kutorejeshwa katika nafasi zake, amesema kuna makosa yalitendeka katika kumvua nyadhifa hizo, kutoka na na msimamo huo imepelekea Hata kuachia nafasi ya katibu mkuu endapo Mwenyekiti Mbowe atashikilia msimamo wake huo. Habari zaidi soma JAMBO LEO.

Waandishi wengine bhana njaa tu
 
Waandike uongo kwa makusudi ili baadae wapoteze muda wa watu makini kukanusha. Ndiyo strategy mpya iliyoko mtamboni?

Chonganisha Mbowe na Slaa, tapeli wajumbe wa mikutano kwa kuwasainisha fomu 'feki' mkidanganya zimetoka Makao Makuu ya Chama, chonganisha wajumbe, chonganisha wanachama na chama chao, chonganisha, chonganisha, sema uongo, sambaza uongo...ndiyo strategy iliyoko mtamboni?

Ndani ya CHADEMA si suala la 'mtu kutaka' wala 'mtu kupinga vikali', ni misingi kutaka na kupinga vikali. Wanaotaka chama kisimame kwenye matakwa ya mtu ndiyo wanaoeneza uongo kama huu. Lengo nini? CHADEMA kuna mgogoro!

Hakuna mgogoro kuna kusimamia nidhamu na kujenga imani ya wananchi ambao wana matumaini makubwa na chama chao.

Hii ya kuwachonganisha Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake mbona haijaanza leo, bado mnahisi inaweza kufanikiwa na kuzaa matunda?

Ndani ya CHADEMA msingi wa masuala yote ni Katiba, Kanuni, taratibu, maadili na miongozo. Si mtu. Kama watu wanaamini hawajavunja misingi ya CHADEMA wasiwasi wote huu unatoka wapi hadi kuzusha maneno ya uongo mkavu kama huu.

Ndani ya CHADEMA, Katiba, kanuni, maadili, taratibu na miongozo ndiyo itampenda au kumchukia mtu yeyote. Si suala la mtu fulani kumpenda au kumchukia fulani.

Hakuna kitu kama hicho. Labda kama hata walioandika hawajui maana ya 'maamuzi ya kikao'...

Hivi kwanini suala la ubadhilifu ndani ya chama hamtaki kulizungumzia na suala la viongozi kukiuka maadili ya uongozi ? nadhani mngefanya hivyo mngemaliza mzizi wa fitina vinginevyo mnachofanya na funika kombe mwanaharamu apite.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom