Waandike uongo kwa makusudi ili baadae wapoteze muda wa watu makini kukanusha. Ndiyo strategy mpya iliyoko mtamboni?
Chonganisha Mbowe na Slaa, tapeli wajumbe wa mikutano kwa kuwasainisha fomu 'feki' mkidanganya zimetoka Makao Makuu ya Chama, chonganisha wajumbe, chonganisha wanachama na chama chao, chonganisha, chonganisha, sema uongo, sambaza uongo...ndiyo strategy iliyoko mtamboni?
Hii ya kuwachonganisha Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake mbona haijaanza leo, bado mnahisi inaweza kufanikiwa na kuzaa matunda?
Ndani ya CHADEMA msingi wa masuala yote ni Katiba, Kanuni, taratibu, maadili na miongozo. Si mtu. Kama watu wanaamini hawajavunja misingi ya CHADEMA wasiwasi wote huu unatoka wapi hadi kuzusha maneno ya uongo mkavu kama huu.
Hakuna kitu kama hicho. Labda kama hata walioandika hawajui maana ya 'maamuzi ya kikao'...