pantheraleo
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 691
- 878
JK ni International figure, ana heshimika kimataifa, tumwache aendelee na majukumu yake ya kimataifa yanagharamiwa na wahusika wanaomwalika.
Nimefuatilia mitandao ya kijamii kuna baadhi ya watu wanajaribu kupotosha kuhusu safari za Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Nawakumbusha kuwa nchi yetu ina historia ya kuheshimika kimataifa tangu awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere. Alipostaafu alikuwa na majukumu ya kimataifa. Kutokana na heshima aliyojijengea kimataifa na mchango wa Tanzania kimataifa.
Mwalimu aliweka msingi ambao bado unaheshimika. Mtakumbuka Hayati Rais Ben Mkapa baada ya kustaafu naye pia alipewa majukumu kadhaa ya kimataifa na hivyo alikuwa akihudhuria vikao vingi nje ya nchi.
Ndugu zangu watanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete naye pia amebeba vema bendera ya Tanzania kimataifa kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake. Tusimbagaze kwa maslahi binafsi. Anawakilisha nchi kutokana na historia na heshima ya nchi yetu kimataifa iliyojengwa na mwasisi wa taifa letu.
Lakini pia tusisahau mchango wake binafsi alipokuwa kiongozi wa taifa letu umemjengea heshima kubwa kimataifa. Tukubali tu anao uwezo na ndio maana anapewa majukumu ya kimataifa na taasisi za kimataifa.
UKWELI KUHUSU SAFARI ZAKE ZA HIVI KARIBUNI NJE YA NCHI NI;
Mbowe,Kigogo na Maria just got it wrong.
Safari ya JK Addis Ababa ya trh 17 mpaka 22 February, 2024 ilikuwa kwa ajili ya kushiriki mikutano miwili;
1) High Level Panel on Water Investment in Africa na Green Climate Fund. Mh. Jakaya Kikwete ni Alternate Co-Chair wa hiyo High Level Panel. Co chairs wenyewe wa hiyo panel ni Macky Sall, Rais wa Senegal, the late Hage Geingob Rais wa Namibia aliyezikwa Feb25 mwaka huu na Mark Rutte, Waziri kutoka Uholanzi.
Mkutano mwingine ni ule wa Heads of State Domestic Financing for Education in Africa,ulioandaliwa na Rais wa Ghana Mheshimiwa Nana Akufo Ado na GPE in Africa. Mh. Kikwete ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya GPE na Rais wa Ghana ndiye Champion wa kuhamasisha nchi kuongeza bajeti za elimu.
Walipomaliza shughuli ya mkutano wao wa masuala ya elimu Mh. JK na Rais wa Ghana walikwenda kujumuika na wakuu wa nchi kwenye uzinduzi wa sanamu ya Julius Nyerere.
Mikutano yote miwili ilikuwa inahusisha Marais waliokuwa wanahudhuria mkutano wa AU pale Adis Ababa.
Kusema kila safari za Rais J.K yupo ni uongo wa kitoto. J.K alikuwa na majukumu yake ya kimataifa yaliyomfanya naye kushiriki katika majukumu ya Marais. Sio kitu rahisi kumuondolea heshima aliyojijengea kimataifa kwa kumsingizia uongo. Ikumbukwe safari za kimataifa zinazohusu shughuli za kimataifa anazoshiriki huwa zinagharamiwa na wahusika sio fedha za serikali.
Ataendelea kushiriki shughuli zake za GPE,Global Water Partnership(GWP),High Level Panel on Water Investment in Africa, SADC Panel of Elders,Africa Food Prize Committee bila kukosa. Kwanza tumshukuru kwa kupaisha brand ya taifa letu.
Mnawajua ambao wanaambatana na mama kila safari hata kama sio waajiriwa wa Serikali.
Sio sawa kumbagaza Rais Mstaafu. Mwacheni atekeleze majukumu yake ya kimataifa kwani ni heshima kwa taifa letu.
Kama hamjui habari ndio hiyo.
Mimi nilikuwepo huko Adis na nimeona nieleze huu kweli ili kuwaelimisha watanzania kuhusu uongo wanaoaminishwa kwa sababu za kibinafsi za kutaka kumchafua huyu mzee anayeheshimika duniani.