Mbowe na Matiko kuzungumza na Watanzania kupitia Wanahabari Golden Tulip Hotel 15 march 2019

Kwani hata wasingeenda hapo GT hiyo hela ingesaidia kuleta mboga nyumbani kwako!??
Ruzuku ambayo inatokana na kodi yangu inaniuma inatumika ovyo.hiyo ni kodi yangu ambayo Chadema wanapewa ruzuku ndio maana inaniuma
 
Ruzuku ambayo inatokana na kodi yangu inaniuma inatumika ovyo.hiyo ni kodi yangu ambayo Chadema wanapewa ruzuku ndio maana inaniuma
wewe ni shetani kwani zile KOROSHO zilizopora na lile chz zilikuuma vile? yale maduka ya dolla yaloporwa mchana kweupeee na utawala huu wa kiimla ulishaamika kama kweli unapenda haki
 
Swali lingine kabla hajaleta taarifa mpya ya kuchangia Lisu aje na taarifa ya mapato na matumizi iliyokaguliwa na CAG ya matibabu ya Lisu ya michango waliyochanga watu kabla ya kuitisha mipya.Alete hata ya kuishia pale Kenya tu alipokuwa kalazwa Lisu.Watu hawajaletewa audited report waletewe kwanza asianze kusema changia!!! Lete Ripoti kwanza Mangi.

Muulize Magu hela ya zile plastiki card kapata Shilingi ngapi mpaka sasa?
 
wazungumze juu ya umuhimu wa viongozi wa siasa kuwa mfano bora kwa wananchi, na sio kuandamana kila siku bila mipango ya kujenga uchumi
 
Loosers!
Wanakwenda kuzungumzia walioyaona gerezani
Serikali ndio inataka watu wasikie habari mbaya za jela,ili waogope kutenda jinai
Ukiona kiongozi mkubwa wa chama,anaita waandishi kuzungumzia vyoo vya mahabusu,basi tambua ya kwamba hicho chama kipo kwenye majaribu makubwa sana
 
ukiambiwa mmiliki ndiye Erythrocyte wa jf na ameamua kuitoa bure kwa ajiri ya makamanda wenzake utakuwa tayari kujiuwa ?

Hili mimi naweza kuamini.

Lakini naomba CHADEMA muache masihala. Hizi sio enzi za lelemama.

Mwambieni Mwenyekiti wenu hizi "Press" zinazofanyika na kuwa kama mazoea hazisaidii kitu.

Anatakiwa achukue mda; afanye 'retreat' na "core cadre" ya chama na watoke na tamko lenye kueleza hali ya chama kilvyo sasa hivi. Mmekuwa na mamluki wengi mno ndani ya chama. Hawa watu wanakipaka kinyesi chama chenu.

Ni lazima mtafute wakati mwafaka mueleze mipango yenu ya kukisafisha chama.

Ndani ya CHADEMA wamo watu wenye 'commitment' na chama. Hawa mamluki wanawakatisha tamaa hata hao walio na msimamo wa dhati wa kuleta mabadiliko Tanzania.

Ni wakati mwafaka, Mbowe, na timu ya watu wachache waliojitoa mhanga kabisa kuona mabadiliko; wakae chini na warekebishe udhaifu huu mkubwa unaoonekana ndani ya chama.

WaTanzania hawawezi kuwaamini mkiwa na watu wa aina hizi za akina Nassari na wengineo. Nidhamu ndani ya chama ni kila kitu wakati huu. Mamluki yeyote hawezi kujiunga na chama makini.

"Press" za ulalamishi na kulialia kuonewa wakati wake ulishapita zamani. WaTanzania hawawezi kuwaonea huruma kwa kulialia. Wekeni mipango madhubuti jinsi mtakavyopambana na CCM waione. Wakiipenda mipango hiyo, watawaunga mkono.
 
Back
Top Bottom