Washington: Freeman Mbowe kuzungumza na Watanzania Waishio Marekani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,600
217,999
Hii ndio Taarifa mpya iliyotufikia hivi Punde , Kwamba Mwamba wa siasa za Tanzania , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema atahutubia Watanzania wanaoishi nchini Marekani , maarufu kama Diaspora .

Mkutano huo unaotajwa kuvunja rekodi ya maombi ya wahudhuriaji , ukilinganisha na mikutano mingine kama hiyo iliyowahi kufanywa na viongozi wengine wa Tanzania , Utafanyika tarehe 10/12/2022 kwenye ukumbi wa BEST WESTERN HOTEL , Washngton DC .

Watanzania wote Mnakaribishwa , Kusikiliza Hotuba hiyo inayotarajiwa kutoa Dira ya Taifa la Tanzania , Umbali si hoja
 
Tupo vizuri ndani ya nchi na pia kimataifa, chama pekee cha kisiasa kilicho halisi kinachotumia ushawishi na hoja tofauti na vyama vingine ikiwemo CCM kinachoburuza nchi kwa kutumia dola, kukanyanga katiba iliyopo, kushindwa kusimamia huduma muhimu za raia kama maji, elimu, uhuru wa watu n.k
 
Hakika .
 
Waambie Lumumba gang wakakomboe ndege iliyozuiliwa ughaibuni, nchi Ina vilaza wenye uzuzu kuwa kuvunja mkataba kunakuja na gharama zake!
Hata Mbowe alivunja mkataba wa katiba na kujifanya mwe yekiti wa milele
 
Hii ndio Taarifa mpya iliyotufikia hivi Punde , Kwamba Mwamba wa siasa za Tanzania , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema atahutubia Watanzania wanaoishi nchini Marekani , maarufu kama Diaspora .

Mkutano huo unaotajwa kuvunja rekodi ya maombi ya wahudhuriaji , ukilinganisha na mikutano mingine kama hiyo iliyowahi kufanywa na viongozi wengine wa Tanzania , Utafanyika tarehe 10/12/2022 kwenye ukumbi wa BEST WESTERN HOTEL , Washngton DC .

Watanzania wote Mnakaribishwa , Kusikiliza Hotuba hiyo inayotarajiwa kutoa Dira ya Taifa la Tanzania , Umbali si hoja
Jambo pekee lililobaki kukamilisha heshima kwa huyu Kiongozi (Mbowe), wakati akielekea kumaliza uongozi wake ni hilo moja pekee, la upatikanaji wa Katiba Mpya Tanzania.

Akiikamilisha hii kazi vizuri, atakuwa amejijengea heshima kubwa sana.
 
Amen
 
Back
Top Bottom