Jamani viongozi na wanachama wa chadema naona sasa mmeanza kulewa madaraka na sifa. Kumbukeni kuwa wananchi wengi wanamatumaini na chama hichi kama ndio mkombozi wao wa kweli. Lakini hebu ona kila siku vurugu na shutuma wenyewe kwa wenyewe. Tafadhali sana hebu fikirieni ilipo NCCR na CUF ambapo wakati fulani vilikuwa ni vyama vyenye nguvu kubwa, lakini leo vipo wapi? Hiyo dhamana ndogo tu mliyopewa na wananchi mnakuwa hivyo, je mkipewa dola itakuwaje. Kumbukeni kwa nguvu mliyonayo kwa sasa mmekuwa kimbilio la watu wengi ambao wengine ni kwa ajili ya tamaa ya uongozi au nimapandikizi ili kuwavuruga kabla ya uchaguzi wa 2015. Mfano mzuri ni watu wa kalba kama kina Shibuda. Nanyie viongozi wa juu punguzeni ufisadi, chama kisiwe kama mali ya ukoo au kabila fulani, wapeni nafasi na wengine. CUF kiliporomoka kwa kashfa moja tu ya udini. Kubalini kukosolewa kwani ndio uongozi, siyo anayejaribu kuwakosoa anaonekana msaliti na kuishia kufukuzwa kama mbwa. Msipojirekebisha nachelea kusema kuwa ikulu tutaisikia tu. Ni mimi mwananchama mwaminifu kutoka mkoani TABORA.