Mbowe, Lissu nidhamu inaporejea wafundeni wafuasi heshima

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,860
35,868
Hongereni kwa kurejea kwa nidhamu chamani.

"Mbowe, Lissu chukueni hatua kurejesha nidhamu kwenye chama"

Kwamba hii ni kwa maelekezo yenu au ni kwa heshima au kuhofiwa kwa majina yenu? Hilo wala si la msingi tena:

"The end justifies the means."

Kuhusiana na "heshima," huu ni ushauri mwingine wa bure kwenu ukilenga kwenye kuwafunda wafuasi kuzingatia:

"Heshima ni kitu cha bure na kuwa hutokana na umri, hekima, mchango wa mtu katika jamii au kutokea katika mafanikio yake, yakiwamo u nguli."

Ni muhimu wafuasi wakaelekezwa na wakafahamu:

1. Tofauti zilizipo baina ya watu au baina ya viongozi na wanachama katika chama.

2. Mbowe au Lissu hawawezi kuwa sawa na mwanachama yeyote.

3. Kauli ya Mbowe au Lissu haiwezi kuwa sawa na kauli ya mwanachama au mfuasi yeyote (na eti kwa sababu tu ana mdomo).

4. Kauli ya Mbowe au Lissu ni kauli za chama, lakini si za kila mwanachama, mjumbe au mfuasi mwingine (na hasa inapokuwa bila ridhaa ya chama).

5. Kauli ya nguli mheshimika katika jamii haiwezi kubezwa kireja reja kwa niaba ya chama na hasa bila ridhaa ya chama.

6. Ni muhimu ikawa wazi kuwa wajumbe, wanachama au wafuasi wenye sharubu jamii ya kambale hawawezi kuvumiliwa.

Heshima ni nguzo kuu kuelekea kwenye nidhamu ya kudumu katika chama ambayo umuhimu wake hauwezi kupuuzwa.
 
Unafiki wako tu

Unafiki kwenye nini hapo? Kauli yako haiwezi kuwa kauli ya chama.

Shivji na mikataba hawezi kubezwa na wa aina ya wewe ndugu Mwaipopo kwa niaba ya chama bila ya ridhaa au CV yako kujulikana.

Na huo ndiyo ulio ukweli ndugu jamii ya kambale.
 
Watu wazima kama Lema, Mdude, Asenga na Mrema wanaweza kufundwa tena kweli?
 
Kama sijakuelewa kabisa

Ninafafanua kwa mifano:

1. Tofauti zilizipo baina watu au baina ya viongozi na wanachama katika chama. -

"Hadhi tofauti baina ya watu zizingatiwe. Obama, Mandela, Nyerere na wa namna hiyo si sawa na Deo Kisandu."

2. Mbowe au Lissu hawawezi kuwa sawa na mwanachama yeyote.

"Hadhi ya Mbowe, Lissu au viongozi katika chama si sawa sawa na wewe au mimi, katika chama."

3. Kauli ya Mbowe au Lissu haiwezi kuwa sawa na kauli ya mwanachama au mfuasi yeyote (na eti kwa sababu tu ana mdomo).

"Asemacho Mbowe au Lissu au viongozi wenye dhamana katika chama (kuhusu chama) ni kauli za chama.

Wasemayo wanachama au wafuasi (kuhusu chama) bila ridhaa ya chama, ni maoni binafsi."

4. Kauli ya Mbowe au Lissu ni kauli za chama, lakini si za kila mwanachama, mjumbe au mfuasi mwingine (na hasa inapokuwa bila ridhaa ya chama).

"Hii na #3 hapo juu ni baba mmoja mama mmoja."

5. Kauli ya nguli mheshimika katika jamii haiwezi kubezwa kireja reja kwa niaba ya chama na hasa bila ridhaa ya chama.

"Kauli ya Prof. Shivji kuhusu mikataba haiwezi kubezwa kireja reja na mfuasi yeyote kwa niaba ya chama bila ridhaa ya chama na hasa asiyekuwa na CV inayotambulika."

6. Ni muhimu ikawa wazi kuwa wajumbe, wanachama au wafuasi wenye sharubu jamii ya kambale hawawezi kuvumiliwa.

"Hapa ni kuwa wazi kiroho safi na anachoita beberu - rules of engagement. - watu wakachagua kusuka au kunyoa"

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Mara nyingi tuliwaonya sana kuhusu utovu wa nidhamu wa Mdude_Nyagali dhidi ya matusi na dharau kwa Rais Samia. Tuliwaambia viongozi wa CHADEMA wakapuuza na kuona kuwa Mdude ana haki ya kusema anayo yasema.

Sasa Mdude anawageukia nyinyi wenyewe CHADEMA na kuanza kuwatafuna
 
Ninafafanua kwa mifano:

1. Tofauti zilizipo baina watu au baina ya viongozi na wanachama katika chama. -

"Hadhi tofauti baina ya watu zizingatiwe. Obama, Mandela, Nyerere na wa namna hiyo si sawa na Deo Kisandu."

2. Mbowe au Lissu hawawezi kuwa sawa na mwanachama yeyote.

"Hadhi ya Mbowe, Lissu au viongozi katika chama si sawa sawa na wewe au mimi, katika chama."

3. Kauli ya Mbowe au Lissu haiwezi kuwa sawa na kauli ya mwanachama au mfuasi yeyote (na eti kwa sababu tu ana mdomo).

"Asemacho Mbowe au Lissu au viongozi wenye dhamana katika chama (kuhusu chama) ni kauli za chama.

Wasemayo wanachama au wafuasi (kuhusu chama) bila ridhaa ya chama, ni maoni binafsi."

4. Kauli ya Mbowe au Lissu ni kauli za chama, lakini si za kila mwanachama, mjumbe au mfuasi mwingine (na hasa inapokuwa bila ridhaa ya chama).

"Hii na #3 hapo juu ni baba mmoja mama mmoja."

5. Kauli ya nguli mheshimika katika jamii haiwezi kubezwa kireja reja kwa niaba ya chama na hasa bila ridhaa ya chama.

"Kauli ya Prof. Shivji kuhusu mikataba haiwezi kubezwa kireja reja na mfuasi yeyote kwa niaba ya chama bila ridhaa ya chama na hasa asiyekuwa na CV inayotambulika."

6. Ni muhimu ikawa wazi kuwa wajumbe, wanachama au wafuasi wenye sharubu jamii ya kambale hawawezi kuvumiliwa.

"Hapa ni kuwa wazi kiroho safi na anachoita beberu - rules of engagement. - watu wakachagua kusuka au kunyoa"

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
Basi sawa
 
Kweli mkuu

CHADEMA imara ni kwa maslahi ya wananchi:

F90vli0XkAAiik6.jpeg

Anasema uongo imhotep, Elli, Rabbon, Tindo, denoo JG, Accumen Mo, Zawadini, na wenye nchi wenzangu?
 
Back
Top Bottom