Mbowe kuunda baraza la Chadema pekee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe kuunda baraza la Chadema pekee

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mallaba, Feb 11, 2011.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  KIONGOZI wa upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema ataunda baraza za Mawaziri kivuli
  litakalojumuisha wabunge wa Chadema pekee.
  Akizungumza katika mahojiano maalum na Mwananchi ofisini kwake jana, Mbowe alisema atatangaza baraza hilo wiki ijayo huku akifafanua kuwa itakuwa unafiki kwake kuunda baraza kivuli la mseto katika kipindi ambapo kuna kejeli na matusi miongoni mwa vyama vya
  upinzani.

  "Majeraha yote haya ni mengi, yanahitaji muda kupona, katika hatua ya sasa nitaunda Baraza la Mawaziri Kivuli
  ambalo litakuwa la Chadema pekee," alisema Mbowe.

  Alifafanua kuwa muda huo aliosema ni wa kutibu majeraha, ni fursa ya kuona maendeleo ya vyama vingine tofauti na Chadema katika utendaji ili kutibu na kuondoa tofauti baina yao.

  Hata hivyo alisema kama ilivyo Bunge hudumu miaka mitano na Baraza la Mawaziri Kivuli pia hudumu miaka
  mitano hivyo linaweza kubadilika.

  "Ni matumaini yangu tutatibu majeraha yetu, kupata amani na kuwaingiza wenzetu katika Baraza la Mawaziri Kivuli.
  Tupende, tusipende tuna mawasiliano ya kibunge, pengine tutagundua tuna makosa au wenzetu watagundua wao
  walikosea, msimamo wetu ni ule ule kwa kanuni ile iliyobadilishwa, lakini sifungi uwezekano wa kuunda baraza
  la mawaziri shirikishi," alisema Mbowe.

  Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro alisema kuwa anaamini busara zitarejea kwa vyama vya
  upinzani na matendo yataashiria utulivu utakaowawezesha kurekebisha tofauti zao.

  Akizungumzia kuchelewa kuunda baraza hilo kivuli, Mbowe alisema ni kutokana na sintofahamu utaratibu utakaotumika
  kuunda baraza hilo, kutokuwepo kwa kamati za kibunge za kisekta na kwamba yupo katika hatua za mwisho kukamilisha hilo kabla ya kulitangaza wiki ijayo.

  Katika hatua nyingine Mbowe alisema Chadema inaheshimu na itawapa ushirikiano wabunge wa upinzani
  waliochaguliwa kuwa wenyeviti wa kamati za Bunge.

  "Kuna mambo matatu yaliyopo nataka niweke wazi, kanuni tayari, chaguzi za kamati tayari, binafsi naheshimu wabunge
  wenzangu, wote wana uwezo mzuri. Naheshimu waliochaguliwa uenyeviti wa kamati walio upande wa CCM
  hata upinzani, Chadema tutawapa ushirikiano kipekee walio
  nje ya CCM," alisema Mbowe na kuongeza:

  "Tutawasaidia kwa kila linalowezekana, pamoja na kuwa tulitofautiana na bado tunatofautiana kuhusu kanuni, wana
  jukumu kubwa kwa Watanzania, tutwasaidia, Cheyo, Mrema na Zitto waweze kufanya kazi kwa ufanisi."

  Alisema kimsingi Zitto, Cheyo na Mrema wanatakiwa kuwa polisi kwa CCM na serikali, lakini bahati mbaya wapinzani
  wamewapa CCM fursa ya kutekeleza mkakati wa kuwagawa na kuwatawala na wamefanikiwa azma hiyo.

  Awali Mbowe alieleza kuwa tangu kampeni hata baada ya uchaguzi kumekuwa na hali ya sitofahamu baina ya vyama vya upinzani hali iliyoutikisa upinzani.

  Alisema hali hiyo ya wapinzani kutetereka, imeipa CCM nguvu ya kuwa 'broker' (dalali) wa kuwachagulia namna ya kufanya mambo yao.

  "Katika mtiririko huo, tumeifanya CCM broker, broker anapokuwa adui yenu atawapa mkakati wa kuwekana sawa
  ili mumkosoe?," alihoji.
   
 2. d

  donald2011 New Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinacho nisikitisha mimi ni CCM kujiingiza kwenye matatizo ya upinzani. Chadema wasingeweza Kudeliver kama wangekuwa wao tu. Sasa CCM imewapa mpini wa kusema sisi tulikuwa tumebanwa na CCM,CUF,NCCR na TLP tulichaguliwa watu. Jamani hamuoni kwamba 2015 chama kitapoteza zaidi? Naogopa.
   
 3. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Halafu kila Waziri atakuwa na Wizara yake? na mshahara wao ni shilingi ngapi vile? jee, kila Waziri atakuwa na Waziri msaidizi? na makatibu wakuu atawataja sio?

  Upuuzi mtupu huu! sasa upinzani kuwa na mawaziri bungeni ndio kuna faida gani kwa mtanzania wa kawaida? jee, umaskini utapungua? elimu itaboreka? kazi zitaongezeka? afya yetu itaboreka?

  Tuache mchezo na maisha ya WaTZ!!!!!
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hata SiSi tumeunda, baraza pekeyetu kule visiwani, yaani CUF na SiSi, sasa tatizo liko wapi. Waacheni waunde halafu polepole sababu zitajitokeza kuwashirikisha CCM, CUF, NCCR, UDP NK
   
 5. BULLDOZZER

  BULLDOZZER Senior Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbowe yuko right kuunda baraza la mawaziri kivuli kutoka chadema kama kanuni inavyorushusu. lakini katika politics hostility hutumika zaidi. pia ni vizuri kuangalia implication ya watanzania katika haya yanayotokea. 2015 sio mbali sana na watanzania watawahukumu wanasiasa. tukumbuke madhara ya ile kauli ya JK kuwa hana shida na kura za wafanyakazi.
  Ni hayo hayo yanayoweza kutokea mbeleni kama hatukuyatibu tokea mwanzo.
  Nilifuatilia uchaguzi wa Uingereza mwaka jana na nikajifunza mengi sana. Nadhani tunahitaji kuonyesha ukomavu wetu katika siasa na kuachana na siasa za kitoto. Siasa za bi mkubwa na za bi mdogo.
   
Loading...