Mbowe kunyang'anywa Bilicanas na NHC mwezi huu

Mbowe kunyang'anywa Bilicanas na NHC mwezi huu

Mkurugenzi wa NHC nEHEMIAH mCHECHU AMESEMA MMILIKI WA JENGO LA cLUB YA BILICANAS , freeman mbowe ni miongoni mwa wadaiwa sugu wa shirika hilo waliopewa notisi inayoisha mwezi huu
 
Mbinu hizi zilitumika mara nyingi na zimekua zikishindwa

Kwanza tujiulize kwanini Specifically atajwe Mbowe kama kuna taasisi nyingi?

Lengo ni kumtoa katika ajenda ya UKUTA

Wanatumia kila silaha na kila njia .Na hata kumalizana wao kwa wao ili kuhalalisha uharamia wao.Lakini kasi ya kuelekea Septemba 1 ndiyo imeshika Kasi
Vija wenzangu mtatumikaaaaaaaaaaaaaaaaa,then mtakuja kugundua mmepoteza sana muda.Tafuteni shughuli halali za kufanya au someniSkill yoyote itakayowasaidia kiuchumi.

Wakuu, inasemekana Zitto Kabwe ali-post facebook hii kitu halafu aka-edit later
.

Original post:
"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. NaaminiMkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini.

Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.

Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?

Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda. Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.

They must know I am not a push over. Chacha died, I won't. Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili."

Revised Post:
Wakili Tundu Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari moja mbili, freelnder ninayotumia Dar Es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni. Tuhuma hii haimo katika tuhuma nilizotuhumiwa nazo na kuandikiwa na chama ili kujibu.

Kama Tundu lissu anadhani tuhuma hii ana ushahidi nayo wa kutosha aiongeze kwenye tuhuma walizoniandikia ili niweze kujitetea kwenye vikao, vinginevyo ni mipasho tu. Nawapa changamoto Tundu lissu na wenzake kama wana tuhuma Mpya dhidi yangu waniandikie kwa mujibu wa taratibu. Tuhuma nilizo nazo hivi sasa na ambazo nimezikatia rufaa katika Baraza Kuu zinahusu mkakati wa kugombea uenyekiti Taifa na kutaka mahesabu ya chama yakaguliwe na CAG.
Kutoka Gazeti la Raia Tanzania
Zitto aanika siri nyeti za Mbowe

- Mbowe asema ni utoto tu

CHALILA KIBUDA NA MARY VICTOR

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ameshusha tuhuma nzito dhidi ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, zikimhusisha na ufisadi.

Hata hivyo, Mbowe naye amejibu tuhuma hizo akisema ni busara zaidi kwa mhusika kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake badala ya kuibua tuhuma nyingine.

Madai hayo ya Zitto kwa Mbowe ni kilele cha siasa za kuchafuana, kutukanana na kuvunjiana heshima kilichodumu kwa takribani miezi mitatu sasa kupitia vyombo tofauti vya habari.

Akiandika katika ukurasa wake binafsi wa facebook jana jioni, Zitto alisema Mbowe hawezi kumnyooshea yeye kidole kuhusu masuala ya maadili kwa vile yeye mwenyewe (Freeman) ndiye mvunja maadili namba moja ndani ya chama hicho.

Jana mchana, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba Zitto amepewa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono; ambaye ni mmoja wa watu waliotajwa na chama hicho kama mafisadi.

"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Mbowe Sh. milioni 40 ili Mbowe asifanye kampeni Jimbo la Musoma Vijijini.

“Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman Sh. milioni 20 za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa.

“Nadhani alimwambia pia kuwa mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe Sh. milioni 200 za Kampeni ya Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe Sh. milioni 100 za kampeni. Lissu anajua....?

“Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.

“Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu. Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.

“They must know I am not a push over (Ni lazima wafahamu kwamba mimi si mtu wanayeweza kumchezea wanavyotaka). Chacha (Wangwe) died, I won't (Chacha Wangwe alikufa, Mimi Hawaniwezi.”

“Mtu ambaye hawezi kuheshimu ...... hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili," aliandika Zitto katika ukurasa wake wa facebook baada ya Tundu kutoa tuhuma zake.

Lissu alikuwa akizungumza katika mkutano ambao Chadema ilitangaza kuwafuta uanachama wanachama wake wawili; Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.

Zaidi ya kuwafukuza akina Kitila, chama hicho jana kimewaagiza viongozi na wanachama wake kutoshirikiana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia chama hicho, Zitto Kabwe.

Zitto alifungua kesi wiki iliyopita akitaka kamati hiyo isijadili uanachama wake, lakini hatua hiyo ya kamati kuu kuwaagiza viongozi wake wasishirikiane na Kabwe kwenye masuala ya Chadema, imetafsiriwa kama kumfanya si mwanachama.

Mwanasheria wa Zitto, Albert Msando, ameliambia gazeti hili jana kwamba ilichofanya Kamati Kuu (CC) kwenye kikao hicho kuhusu Zitto ni “kuingilia uhuru wa mahakama” kwa vile tayari wameshampa adhabu wakati Mahakama inasikiliza shauri lake.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, alisema wamechukua hatua hiyo kwa sababu wamebaini Kitila na wenzake walikuwa na lengo la kubomoa Chadema.

“Viongozi hawa walikuwa wameandaa mkakati wa muda mrefu wa kukibomoa chama kwa kukichafua kwa wananchi na kuwachafua viongozi wa juu kwa kutumia tuhuma za uongo za ufisadi,” alisema Slaa.

Slaa alikuwa akizungumzia waraka wa siri ulioandaliwa na Kitila na Mwigamba uliotaka kufanyika kwa mabadiliko katika ngazi ya juu ya uongozi wa chama hicho.

Majibu ya Mbowe

Akizungumza na mwandishi wetu Mbowe alisema ni utoto kukwepa kujibu hoja kwa kuanzisha tuhuma dhidi ya mtu mwingine ambazo si za kweli.

“Mimi nimekuwa nikisimamia ukweli, mtu anapotuhumiwa ni lazima ajibu tuhuma hizo. Ni utoto kuacha kujibu tuhuma na kuzusha tuhuma nyingine. Anapaswa kufanya utetezi wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.

“Mimi ni mbunge, bungeni nimekuwa nikichangia watu mbalimbali mimi kama Freeman, si ajabu watu wengine kunichangia. Hapa jambo la msingi ni kwamba unapewa pesa kwa sababu gani, kwa nia ipi? Kupewa pesa na Kikwete au CCM si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi, kwa malengo gani?” alihoji Mbowe.

Mbowe alilaumu baadhi ya vyombo vya habari kushiriki kumchafua kwa taarifa za kutunga kutoka kwa watu anaodhani wamekuwa na uhusiano na Zitto.
===============================
==============================
Yangu macho.TANESCO msikate UMEME niko huku na CLINTON MBOWE Tunataka kufuatilia step by step namna UKUTA Inavyoenda saa 2 usiku ITV.
 
Magu alipata nyepesi kuwa jamaa anadaiwa na alihafikiana na NHC awe analipa kwa awamu na akawa anafanya hivyo ila Magu kaagiza apokonywe mara moja
 
Magu alipata nyepesi kuwa jamaa anadaiwa na alihafikiana na NHC awe analipa kwa awamu na akawa anafanya hivyo ila Magu kaagiza apokonywe mara moja
Utawala huu MBOWE Atapata tabu.Atabaki tu kuLA ruzuku NA KUPELEKA VIKAO VYA chadema kwenye vijiHOTELI Vyake.NSSF Inamsubiri pia.
 
Utawala huu MBOWE Atapata tabu.Atabaki tu kuLA ruzuku NA KUPELEKA VIKAO VYA chadema kwenye vijiHOTELI Vyake.NSSF Inamsubiri pia.
Inawezekana ukoo wako wote hata mgahawa hamjamiliki,zaidi kuuza maandazi getini,samahani barazani
 
Ndio kaona aseme leo haturud nyumaa #UKUTA
 
Inawezekana ukoo wako wote hata mgahawa hamjamiliki,zaidi kuuza maandazi getini,samahani barazani
Hunifahamu ndugu,ila namfahamu Mbowe.Namfahamu Mbowe ndio maana namzungumzia.Huwezi kunizungumzia mimi kwa kuwa hunifahamu.
 
Hunifahamu ndugu,ila namfahamu Mbowe.Namfahamu Mbowe ndio maana namzungumzia.Huwezi kunizungumzia mimi kwa kuwa hunifahamu.
Ukweli unauma siku zote,pole,unamfahamu Mh Mbowe kwani wewe nani kwake
 
**Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu amesema mmiliki wa jengo la Club ya Bilicanas, Freeman Mbowe ni miongoni mwa wadaiwa sugu wa shirika hilo waliopewa notisi inayoishia mwezi huu.

Chanzo mwananchi

Sisi kama wanachi wa kawaida tunafaidika na nini kwa NHC kutoa taarifa za madeni ya mtu mmoja kati ya wadaiwa wengi sugu wa shirika hilo ikiwemo serikali yenyewe????? Kwani Mkataba wao wa upangaji unasema Mbowe asipolipa kodi taarifa zake zitapelekwa kwenye vyombo vya habari??????
 
Baada ya Tangazo hili la NHC, litafuatia la TRA kudai kodi, Then NSSF kudai Michango ya Wafanyakazi, Then Osha, then Jiji kufuta kibali cha Night Club, then Msajili wa Magazeti kulifuta gazeti, then, then, then...mwisho wa siku mtasikia tangazo la kusitisha maandamano na mikutano nchi nzima! ,baada ya hakuna lolote atakalofanywa, life just as usual!.

Pasco
Uwekezaji wa mbowe hapa nchini ni 1/3 tu ya Uwekezaji wake duniani. Ile familia Ina pesa tena pesa kongwe.
 
duh kisa na mkasa ni swala la siasa za UKUTA
Acha ku think negative,kwa hyo akiwa ukawa na ukuta asilipe kodi?mbona watu mnapenda upinzani tu hata kwa maswala ya msingi?asidaiwe kisa ni mbowe?mpe kiwanja chako bure ajenge night club asidaiwe na mtu lakini bado atalipa kodi ya biashara tu!
 
Kumbe Mbowe mkwepa kodi,ndo maana wanamchukia Rais
 
Umenikumbusha ule msemo wa sungura
Czitaki mbichi hizi.jpeg
 
Kumbe ndo maana watu wanachukia sana Rais anaposema watu walipe kodi.

mbowe anajiaribia mwenyewe kwa kufanya biashara ambazo zinamahusiano ya moja kwa moja na chama chake mfano mzuri ni TANZANIA DAIM mauzo ya 2010..2013..2014.. huwezi kuyalinganisha na haya ya 2015..16 .. ukienda bilcana hivyo .. ule ushabiki umepungua sana baada ya watu kugundua wanatumiwa kama ngazi kufikia kwenye mafanikio yao , leo cdm ikifanya vibaya na biashara nazo zinafanya vibaya .. biashara inatakiwa iwe huru hata ikiwezekana kumkusoa mwenyekit pale inapo bidi ,
 
Hii Notisi haikutolewa siku zote mpaka walipoona UKUTA!

NHC kaeni chini na mteja wenu mmalizane huko huko, sisi hayatuhusu, kwani wakati mnakubaliana kumpangishia tulijulishwa?
Wangapi wanadaiwa miaka nenda rudi hamuandiki gazetini? Mchechu wewe ni msomi acha kujitoa ufahamu kwa ajili ya siasa chafu.
 
Back
Top Bottom