Mbowe, Kunahitajika mkakati wa haraka Bungeni

Mbowe, Kunahitajika mkakati wa haraka Bungeni

Km C UPUUZI NA KUTOKUJITAMBUA AU KWANINI KIONGOZ MKUBWA WA NCH UTUKANWE LIVE HLF UVUNGE KIAINA? ANAJUA MADHAMBI YAKE NA ANAELEWA KW MATUSI YANAYOMSUBIR NI MENGI INAMBIDI AWE MPOLE MANA HANA LA KUFANYA
 
nilimuona anaanza kuchangia nikaondoka kwenye luninga kwa sababu ni matapishi
 
Hahaha...mhariri wa ITV nimempenda sana!!CDM wanafanya upupu ili kujitafutia umaarufu kupitia vyombo vya habari!!
 
mama Chiku Abwao ameongelea mambo mengi sana, la kwanza maandamano amesisitiza kuwa maandamano ya CDM yanaungwa mkono na watu wa rika lote kwa kuwa yanawaamusha na kuwasemea wanyonge. akaonya kuhusu kejeli ya magamba kuhusu maandamano na kusema mbona na nyie mmeunga tela kwa kuandamana Mbeya na sisi CDM hatujawakejeli?ameonya serikali kuwa iliridhia mfumo wa vyama vingi ila inaongoza nchi kwa watisha wananchi hasa wa upinzani na akasema ndo sbb leo wabunge wa upinzani walokuwepo bungeni mwaka 1995 pamoja naye hawapo,wamekata tamaa na kurudi ccm na wachache walobaki ni mawakala wa ccm kama Mzee mrema(akaonywa na m/kiti asitaje majina) ila ujumbe ulikuwa umeshafika. akairudia rudia hotuba ya Mh Lema(soma thread ya hotuba ya lema) na kuitia nguvu zaidi. Akawaonya magamba kuwa nchi haitatawalika kama CDM wakikosa uvumilivu na akawaonya tena viongozi kuwa kama wataendelea hivi wananchi watawazomea popote wapitapo na maandamano yatazidi zaidi na wananchi wameamka ndo maana wanawaunga mkono. kuhusu wabunge wa ccm kusimama na kusema wananchi watawahukumu 2015, akasisitiza hakika watawahukumu ktk haki ya kuwatetea wanyonge na katu hawataogopa wala kukata tamaa kama hao walorudi ccm. kuhusu mauaji ya polisi akasema hawalaumu polisi kwa kuwa wanatii amri haramu ya viongozi wa ccm na akasema yeye na wenzake hawatacha kuwasemea wanyonge kama polisi imeua ndivyo watakavyosema bila kumung'unya maneno. kuhusu amani akasema hakuna amani palipo na udhalimu na umasikini na akampinga waziri nahodha aliyesema kuwa maandamano yanaleta umaskini, akampasha kuwa mbona maandamano yameanza juzi tu na miaka 49 mbona hamkuwapa maendeleo????ki ukweli ameongea with authority ya hali ya juu sana mpaka mawaziri walionyeshwa wanavyosisimkwa na kupigwa ganzi kwa kila sentensi aloongea.
CDM ina hazina kubwa sana...sikuwahi kumjua huyu mama kuwa ni strong that much.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Mkuu wewe hutaki kuangalia TV ya Taifa unaangalia TV Station za watu binafsi. TBC1 wame cover vizuri sana hiyo habari kwenye taarifa yao ya saa mbili usiku.
 
Walikuwa wanatania tuu mkuu, au umesahau Tanzania ni nchi ya mzaha, kuanzia viongozi, vyombo vya habari etc
 
Hivi ni kweli simbachawene kasomea sheria?? Mbona mweupe sana.! Amejishusha mno.!
 
Huyo kalewa nyazifa za magamba alizopewa eti watu wadanganywa kufanya mandamano soma alama ya nyakati mh simbachewema tz hii ipo gizani unadhani wanainchi watashindwa kuandamana ushauri mdogo kwako tatueni matatizo ya wanainchi sio kupigana vijembe na ubabe.
 
Aliongeza na hili katika mchango wake ".........hawa wanataka wachukue nchi/serikali kirahisi......." kauli hii imedhihirisha jinsi "jamaa" walivyokwisha kata tamaa kwa hiyo wananchi tuwe makini na nyendo zao wakati wa harakati zetu za kutaka "kujikwamua".
 
du! Kwa hili ITV wamechemsha wakuu. Hii inatokana na ukosefu wa uhuru wa vyombo vya habari. MENGI anachunga ugali wake.
 
WaTanganyika wote tumemsikia na kuona akichangia Hoja ya kutaka wabunge wapimwe akili. Angekuwa ni Mbunge wa CDM meomba Muongozo huo leo wote wangetolewa nje na kuzomewa. oh katutukana oh wana maneno ya kitoto lakini kwa vile wa CCM mwenyekiti kamchekelea na kumtuliza! Kusema ile haki hawa wapinzani wa CDM nawakubali sana na hata jana nilikuwa najaribu kupima wanakosea wapi kumbe nikaona Udhaifu wa yule Mwenyekiti UCHWARA. eti anatishia kabisa kumuitia Mbunge Sagenti wa Hamu aje amkamate Mbunge kwa kutaka tu kutoa hoja yenye manufaa kwa watanzania. oh bunge huahirishwa vita ikizuka tu. na kama huyo mbunge alikuwa anataka kuleta taarifa hizo angejuaje ikiwa hakutaka kumsikiliza? nashauri huyu Mwenyekiti wa Jana apimwe wa kwanza na hata mkojo wake waone kama anavuta Bangi au Unga.
 
Hali inayoendelea bunge ni mtaji mzuri wa kisiasa kwa CDM. Msubiri muone
 
Hata polisi watashindwa kuwalinda sasa. Chuki! chuki! yani Ndugai hovyoo sijui alisoma shule gani yule. Yaani ***** kabisa!
 
ninaimani watarudi nyumbani 2015, msafi na mnafiki awadumu
 
Nilidhani nlipitiwa na mbonji (usingizi) ndo sikuiona, kumbe dah.! Watutake radhi aisee
 
Back
Top Bottom