BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Mbowe: Kikwete ameelemewa
na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema Rais Jakaya Kikwete anahitaji msaada wa haraka kiuongozi kwa sababu ameelemewa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho jana, Mbowe alisema kuwa mambo yanayotokea sasa hivi nchini ni dalili tosha kuwa uongozi wa Rais Kikwete umeelemewa na unahitaji kusaidiwa.
Alisema matukio yanayoiandama serikali ya Rais Kikwete kwa sasa ni ya kusikitisha kwa sababu yanaashiria kuwa nchi ipo hatarini kuelekea katika machafuko ya kijamii na kuanguka.
Alisema kwa kiasi kikubwa, hali hiyo inatokana na kile alichodai kuwa ni uongozi wa Rais Kikwete kushindwa kuongoza kwa matakwa ya wananchi na badala yake kutekwa na mafisadi.
Alisema taifa linahitaji mabadiliko ya haraka ya utawala, ili kudhibiti hali iliyoanza kujitokeza hivi sasa.
Akizungumza kwa sauti tulivu lakini yenye masikitiko na huruma, Mbowe alisema kupigwa mawe kwa msafara wa rais, kuzomewa kwa viongozi, migomo ya walimu, madaktari na kufungia ofisini kwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi na wastaafu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni ishara ya nchi kuelekea katika machafuko ambayo mwisho wake ni kuanguka kwa taifa la Tanzania.
Alisema matukio yote hayo ya kusikitisha yametokana na uongozi wa Rais Kikwete kutekwa na mafisadi na kusahau kuwahudumia wananchi ambao hivi sasa wana maisha magumu na wamekata tamaa kiasi cha kuwa tayari kufanya jambo lolote baya.
Uongozi wa Kikwete umeshindwa kuongoza, ndiyo maana wananchi wamekata tamaa na wanaanza kumrushia mawe na kuwazomea viongozi wake. Hali hii ni mbaya na kuna haja ya kufanya mabadiliko ya mfumo wa utawala, alisema Mbowe.
Aidha, Mbowe alionyesha masikitiko yake kwa msafara wa Rais Kikwete kupigwa mawe huko Mbeya na kusema jambo kama hilo halikupaswa kutokea, lakini wananchi wamelazimishwa kufikia hali hiyo.
Kuhusu kulegalega kwa ushirikiano wa CHADEMA na vyama vya upinzani vilivyokuwa katika ushirikiano vya TLP, NCCR-Mageuzi na CUF, alisema wameamua kurudi nyuma kujipanga lakini hawajavunja ushirikiano huo.
Kwamba wamegundua baadhi ya washirika wa umoja huo wamekuwa wakitumika kuibomoa CHADEMA, hivyo wanapaswa wajipange upya na ikiwezekana kuchagua vyama watavyoshirikiana navyo.
Kurudisha nyuma majeshi si kushindwa vita, bali ni kujipanga, hivyo na sisi tumefanya hivyo huku tukitafakari ushirikiano wetu ili uwe na tija, tumegundua kuwa washirika wetu wengine wanatumiwa na CCM kutubomoa, alisema Mbowe.
Akizungumzia uchaguzi mdogo wa Tarime uliofanyika wiki iliyopita, alisema walichokifanya Wanatarime ni mfano wa kuigwa na kinaonyesha ukomavu wa demokrasia, kwani hawakujali vitisho vya dola, fedha zilizokuwa zikitolewa na CCM na maneno ya uzandiki yaliyokuwa yakitolewa na watu.
Alisema pamoja na kupigwa risasi, mapanga, mabomu ya machozi na maji ya kuwasha, Wanatarime waliamua kumchagua Charles Mwera (CHADEMA) kuwa mbunge wao, hali inayodhihirisha kuwa wananchi wakiamua jambo, wanaweza.
Aliongeza kuwa kulikuwa na njama za kuiba kura pamoja na kubadilisha matokeo, lakini wakazi wa Tarime walikuwa macho kuhakikisha hakuna hila inayofanyika na kumpata kiongozi waliyekuwa wakimtaka badala ya aliyekuwa akitakiwa na CCM.
Naye Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema Watanzania wanapaswa kuamka, kwa vile maisha bora waliyoahidiwa na Rais Kikwete hayaonekani na kadiri siku zinavyokwenda ndivyo yanazidi kuwa magumu.
Alisema utawala uliopo hivi sasa haufuati sheria na kutoa mfano wa watuhumiwa wa ufisadi kupewa muda wa kurejesha kile walichokiiba na kuachiwa badala ya kufikishwa mahakamani kama wanavyofanywa wezi wa kuku au wengineo.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, alisema kama Watanzania wataliacha taifa mikononi mwa CCM, litaangamia na vizazi vijavyo vitakuja kulaumu kizazi kilichopo sasa kwa kutoungana na kufanya mapambano ya kudai uhuru kutoka kwa watawala wasiojali masilahi ya wananchi.
Na katika kile kinachoonyesha kuwa Kikwete amelemewa na majukumu, jana alilazimika kufuta baadhi ya shughuli zilizokuwa zimepangwa katika ziara yake mkoani Mbeya, kutokana na kubana kwa ratiba hiyo.
Ilidaiwa kuwa Kikwete alilazimika kuahirisha baadhi ya shughuli hizo kutokana na ratiba kubana, huku akisubiriwa Dar es Salaam kuongoza harambee iliyoandaliwa na Chama cha Maalbino nchini. Harambee hiyo ilipangwa kufanyika jana na kufuatiwa na maandamano leo.
Moja ya shughuli aliyoifuta ni mkutano wa hadhara wa majumuisho, uliokuwa umepangwa kufanyika katika Uwanja wa Sokoine, mjini Mbeya.
Ilitarajiwa kuwa katika uwanja huo, pamoja na kuelezea masuala mengine kadhaa, Rais Kikwete angepata fursa ya kujibu hoja za wafanyabiashara wa Soko la Mwanjelwa, ambao katika siku ya pili ya ziara yake, waliuzuia msafara wake kwa kulala barabarani.
Aliposimama, kundi kubwa la wafanyabiashara walianza kupiga makelele, na hivyo kusababisha kutoelewana baina yao na rais, jambo lililomfanya Rais Kikwete awatake waorodheshe matatizo yao na atayajibu kwenye mkutano wa hadhara wa jana, ambao ulifutwa dakika za mwisho.
Aidha, Rais Kikwete alishindwa kwenda kukabidhi hundi ya fedha za ujenzi wa soko hilo la Mwanjelwa, ambalo liliungua moto siku zilizopita, na badala yake shughuli hiyo aliifanya katika mkutano wa majumuisho wa ndani.
Akizungumza katika mkutano huo, Rais Kikwete aliwataka viongozi wa mkoa huo kufanya kazi kwa pamoja na kuacha kupigana vijembe na kuwekeana vikwazo.
Hizi inaelekea kuwa ni salamu nzito kwa viongozi wa mkoa huo, ambao wanasifika kwa uhasama miongoni mwao, kiasi cha kuhujumiana wao kwa wao.