Ohhh lala! Mzee wa kubadilishia GIA ANGANI bado yupo..... sasa hivi anakanyaga klach za BODA BODAKAZI imeanza. Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya Serikali ya Rais John Magufuli jana kusababisha vurugu kubwa Kahama mkoani Shinyanga.
NI kwa mara ya kwanza ndani ya utawala wa Rais Magufuli, taifa linashuhudia vurugu za kisiasa zinazotokea kwa mgongo wa Jeshi la Polisi nchini.
Vurugu kubwa imetokea jana baina ya Jeshi la Polisi na wananchi kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusababisha sintofahamu.
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA amesema kuwa, pamoja na vitisho vya demokarsia nchini, chama hicho hakitarudi nyuma kudai haki.
Mbowe amesema kuwa, wataendelea kudai haki ya demokrasia nchini ndani ya mahakamani, bungeni, ndani na nje ya nchi.
“Huu ni mwendelezo wa serikali na mabavu. Hawataki vyama vingine vya siasa kufanya mikutano,” amesema Mbowe na kuongeza kwamba, watakwenda mahakamani na kuongeza.
Taarifa kuhusu vurugu hizo zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi lilitumia maji ya kuwasha pamoja na mabomu ya machozi kutawanya watu waliokuwepo kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na CHADEMA mjini Kahama.
Mkutano huo ulikuwa ni uzinduzi wa ‘Dai Demokrasia’ ambapo Jeshi la Polisi liliingilia kati na kuuzuia ikiwa ni muda mchache baada ya Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa nchini.
“Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya habari limebaini kuwa, mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder),” ilieleza taarifa ya Nsato Mssanzya, Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Makao Makuu jijini Dar es Slaam jana
Vurugu hizo zilianza saa nane mchana baada ya polisi waliojiandaa kufika kwenye eneo la tukio na kisha kuuzuia kufanyika mkutano huo.
Hatua ya polisi kutoa maelezo ya kuzuia mkutano huo na kutaka watu watawanyike ilianza kuzua mzozo na hatimaye vurugu ambapo wananchi waliokuwa kwenye viwanja vya mkutano vya CDT walianza kupambana na polisi.
Hali hiyo iliwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha huku wananchi wakitumia mawe kukabiliana na mshindo wa polisi Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU).
Hayo yalifanyika ikiwa tayari Mbowe pamoja na viongozi wenzake wakiwa tayari wamewasili kwenye mkutano huo.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, Mbowe, Dk. Vincent Mshinji, Katibu Mkuu wa CHADEMA pamoja na wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge walizingirwa na polisi huku wakimwagiwa maji ya kuwasha wakiwa kwenye magari yao.
Hali hiyo inaelezwa kuwazidisha hasira wananchia waliokuwa wamekwenda kuhudhuria ufunguzi huo na kusababisha kuwatupia mawe polisi.
Kabla ya tukio hili, yalianza majibizano kati ya polisi na viongozi wa CHADEMA kwa kutumia vipaza sauti.
Polisi walitumia kipaza sauti kilichokuwa kwenye gari lao kwa kusema “Tangazo, tunawataka wananchi mliopo kwenye uwanja huu muondoke kwa sababu mkutano huu si halali. Ondokeni eneo hili kwa ajili ya usalama wenu. Huu mkutano si halali.”
Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) alishika kipaza sauti na kupuuza tangazo la polisi.
“Hapa polisi CCM wasituvuruge. Jamaa wametupa wenyewe barua ya uturuhusu tufanye mkutano wetu, leo wanakuja na washawasha zao kuzuia, ebooh!” alisema Mwita.
Wakati akipuuza tangazo hilo wananchi waliokuwepo kwenye uwanja huo walikuwa wakimshangilia.
KAZI imeanza. Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya Serikali ya Rais John Magufuli jana kusababisha vurugu kubwa Kahama mkoani Shinyanga.

Mshaija toka bunge la bajeti lianze kuna habari ipi hujaisikia?
Wahaya mnadai nyie ni vichwa,yaani umeingia mkenge kuwaamini wasanii
Watu watatu au wanne mnaojuana hamuwezi kuwa na jambo mnaliongea? Au uhuru huo wananyimwa?Duh! Mkuu, ina maana hiyo departure ya airport ya Mwanza imekuwa local zaidi kiasi ambacho mijadala kama hiyo hujadiliwa? Only in Tanzania. Sijapata kuona uwanja wowote wa kimataifa kunaibuka mijadala ya aina hiyo labda kwenye stand ya basi ama kituo cha daladala
Kabisa mkuu maana kipindi hiki ndio haswa upinzani unaonekana kuliko kipindi chote kwani kila siku utasikia mbunge fulani kafikishwa mahakamaniNi kweli kupata haki ni ngumu lazima uwe na roho ngumu mapambano yaendelee
Hiki ni kipindi kigumu sana kwa viongozi wetu wa vyama vya upinzani hasa cdm na ukawa kwa ujumla kutokana na misuko suko wanayo ipata na kwa kufikishwa mahakamani na si ajabu kuna wengine wanaweza kufungwa,lkn hayo yasiwavunje moyo maana huo hasa ndio upinzani wa kweli kumbukeni kuwa hakuna mtawala aliye kabidhi madaraka kwa mpinzani wake kwa sherehe, jikumbushe yaliyo tokea kwa Nelson Mandela, nasi wananchi tupo bega kwa bega nanyi kwa maombi na sala......mungu awabariki sana.....
Kabisa mkuu maana kipindi hiki ndio haswa upinzani unaonekana kuliko kipindi chote kwani kila siku utasikia mbunge fulani kafikishwa mahakamani
Sikushangai kwa bandiko lako hili,unajua nini maana ya uwakilishi?au ulitaka wote twende bungeni?Watu mu wanafiki sana. Unayewapa pole hata jina tu hutaki kujitaja. Halafu unaongea nyuma ya keyboard. Kuwasaidia uwashauri wasivunje sheria.
Tatizo sheria ya Tanzania iko kama panga sio msumeno inawahusu wapinzani tuWashaurini waache ukorofi dhidi ya sheria
Na wala yeye hana haja ya kusifiwa na wewe mtumwa wa lumumbaAliyetoa hiyo post nilikuwa namuona anaakili kumbe ameshikiwa na viroba vya Ufipani
Ukorofi upi huo dhidi ya sheria unao usema?Washaurini waache ukorofi dhidi ya sheria
Mkuu hata kule afrika ya kusini ilikuwa hivyo lkn mwisho wa siku walio ibuka washindi ni wananchi wanyongeTatizo sheria ya Tanzania iko kama panga sio msumeno inawahusu wapinzani tu