Mbowe: Haturudi nyuma

Mbowe: Haturudi nyuma

KAZI imeanza. Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya Serikali ya Rais John Magufuli jana kusababisha vurugu kubwa Kahama mkoani Shinyanga.

NI kwa mara ya kwanza ndani ya utawala wa Rais Magufuli, taifa linashuhudia vurugu za kisiasa zinazotokea kwa mgongo wa Jeshi la Polisi nchini.

Vurugu kubwa imetokea jana baina ya Jeshi la Polisi na wananchi kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusababisha sintofahamu.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA amesema kuwa, pamoja na vitisho vya demokarsia nchini, chama hicho hakitarudi nyuma kudai haki.

Mbowe amesema kuwa, wataendelea kudai haki ya demokrasia nchini ndani ya mahakamani, bungeni, ndani na nje ya nchi.

“Huu ni mwendelezo wa serikali na mabavu. Hawataki vyama vingine vya siasa kufanya mikutano,” amesema Mbowe na kuongeza kwamba, watakwenda mahakamani na kuongeza.

Taarifa kuhusu vurugu hizo zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi lilitumia maji ya kuwasha pamoja na mabomu ya machozi kutawanya watu waliokuwepo kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na CHADEMA mjini Kahama.

Mkutano huo ulikuwa ni uzinduzi wa ‘Dai Demokrasia’ ambapo Jeshi la Polisi liliingilia kati na kuuzuia ikiwa ni muda mchache baada ya Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa nchini.

“Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya habari limebaini kuwa, mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder),” ilieleza taarifa ya Nsato Mssanzya, Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Makao Makuu jijini Dar es Slaam jana

Vurugu hizo zilianza saa nane mchana baada ya polisi waliojiandaa kufika kwenye eneo la tukio na kisha kuuzuia kufanyika mkutano huo.

Hatua ya polisi kutoa maelezo ya kuzuia mkutano huo na kutaka watu watawanyike ilianza kuzua mzozo na hatimaye vurugu ambapo wananchi waliokuwa kwenye viwanja vya mkutano vya CDT walianza kupambana na polisi.

Hali hiyo iliwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha huku wananchi wakitumia mawe kukabiliana na mshindo wa polisi Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU).

Hayo yalifanyika ikiwa tayari Mbowe pamoja na viongozi wenzake wakiwa tayari wamewasili kwenye mkutano huo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, Mbowe, Dk. Vincent Mshinji, Katibu Mkuu wa CHADEMA pamoja na wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge walizingirwa na polisi huku wakimwagiwa maji ya kuwasha wakiwa kwenye magari yao.

Hali hiyo inaelezwa kuwazidisha hasira wananchia waliokuwa wamekwenda kuhudhuria ufunguzi huo na kusababisha kuwatupia mawe polisi.

Kabla ya tukio hili, yalianza majibizano kati ya polisi na viongozi wa CHADEMA kwa kutumia vipaza sauti.

Polisi walitumia kipaza sauti kilichokuwa kwenye gari lao kwa kusema “Tangazo, tunawataka wananchi mliopo kwenye uwanja huu muondoke kwa sababu mkutano huu si halali. Ondokeni eneo hili kwa ajili ya usalama wenu. Huu mkutano si halali.”

Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) alishika kipaza sauti na kupuuza tangazo la polisi.

“Hapa polisi CCM wasituvuruge. Jamaa wametupa wenyewe barua ya uturuhusu tufanye mkutano wetu, leo wanakuja na washawasha zao kuzuia, ebooh!” alisema Mwita.

Wakati akipuuza tangazo hilo wananchi waliokuwepo kwenye uwanja huo walikuwa wakimshangilia.
We are used to your journeys that always start but end nowhere. Go on because that is what you know; making a lot of noise but zero results.
 
NAUZA! WALE WAZEE WETU. SUMAYE NA LOWASSSA WALIKUWEPO KIPINDI MABOMU YANALINDIMA?
 
Huwa nawaza kila wanapotoka katika ukumbi wa bunge, kwa kawaida huwa wanaamka alfajiri wanajiandaa kwa kupiga suti matata, wanabeba mabegi ili kuwawakilisha waliowachagua lakini muda wa uwakilishi ukianza wanatoka nje. Hahaha sasa kuna maana gani ya kujisumbua kuamka na kuulamba na kuamka mapema hivyo.
Acha tuendelee kufanya utalii wa ndani
 
kuna suala posho ni haki yao usipoweka dole ysn fingerprint no allowance
 
halafu polisi mkituona tumeandamana na muheshimiwa wetu mbowe mtuchalaze bakora wote.yale ya kumchukua kikubwa na kumpeleka central baadaye mnamuacha ndo siwaelewagi.kama kichura na yeye aruke kama buti la mdomo tupigwe naye
 
Huwa nawaza kila wanapotoka katika ukumbi wa bunge, kwa kawaida huwa wanaamka alfajiri wanajiandaa kwa kupiga suti matata, wanabeba mabegi ili kuwawakilisha waliowachagua lakini muda wa uwakilishi ukianza wanatoka nje. Hahaha sasa kuna maana gani ya kujisumbua kuamka na kuulamba na kuamka mapema hivyo.
Acha tuendelee kufanya utalii wa ndani

Wanakuchekesha? Haya cheka mpaka unenepe, kwani mafisiemu mumebakishiwa akili za kuvukia bara bara na kukenua kenua meno tu
 
Afu kinachouma zaidi wanalamba na kodi zetu bure...Yaani ningewaona wa maana badala ya kuzichukua wao hizo posho wangezichukua na kukabidhi majimboni kwao kwa maana kiuhalisia hawastahili kuzichukua sababu hawatuwakilishi kama tulivyo watuma na kwasababu KATIBA yetu imeruhusu mwanya huu wa kujichukulia posho bure TUNGEWAONA WA MAANA wasaini na wazichukue posho hizo na kuzielekeza majimboni mwao na wao kubaki na a certain percentage na sikujinufaisha wao tu na kuwaumiza wananchi .....
 
Huwa nawaza kila wanapotoka katika ukumbi wa bunge, kwa kawaida huwa wanaamka alfajiri wanajiandaa kwa kupiga suti matata, wanabeba mabegi ili kuwawakilisha waliowachagua lakini muda wa uwakilishi ukianza wanatoka nje. Hahaha sasa kuna maana gani ya kujisumbua kuamka na kuulamba na kuamka mapema hivyo.
Acha tuendelee kufanya utalii wa ndani
DEMOCRASIA INABAKWA UNAKENUA MENO,.!STU....PD.
 
Chama cha vurugu na wasiotii mamlaka

Huwezi kuwa na vyama vya siasa visivyofanya mikutano ya hadhara ya kisiasa, maadamu ni vyama vya upinzani kwa vyovyote vile vitaponda utawala wa mtawala na kunadi utawala mbadala ili wakati ukifika wachaguliwe!!! Hii ndiyo utawala wa vyama vingi.
 
Kwanza ndo panakucha tunaanza kuona mengi.....
 
Ninazidi kushangaa mapambano yanayotokea sasa kati ya upinzani NA chama tawala kuna nini ni siasa tu au ni kushindwa kwa upinzani au chama tawala mapema
 
Huwezi kuwa na vyama vya siasa visivyofanya mikutano ya hadhara ya kisiasa, maadamu ni vyama vya upinzani kwa vyovyote vile vitaponda utawala wa mtawala na kunadi utawala mbadala ili wakati ukifika wachaguliwe!!! Hii ndiyo utawala wa vyama vingi.
Hoja nzuri,lakin wapinzani wa kwetu ni matapeli tu
 
Back
Top Bottom