Mbowe: Haturudi nyuma

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
KAZI imeanza. Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya Serikali ya Rais John Magufuli jana kusababisha vurugu kubwa Kahama mkoani Shinyanga.

NI kwa mara ya kwanza ndani ya utawala wa Rais Magufuli, taifa linashuhudia vurugu za kisiasa zinazotokea kwa mgongo wa Jeshi la Polisi nchini.

Vurugu kubwa imetokea jana baina ya Jeshi la Polisi na wananchi kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusababisha sintofahamu.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA amesema kuwa, pamoja na vitisho vya demokarsia nchini, chama hicho hakitarudi nyuma kudai haki.

Mbowe amesema kuwa, wataendelea kudai haki ya demokrasia nchini ndani ya mahakamani, bungeni, ndani na nje ya nchi.

“Huu ni mwendelezo wa serikali na mabavu. Hawataki vyama vingine vya siasa kufanya mikutano,” amesema Mbowe na kuongeza kwamba, watakwenda mahakamani na kuongeza.

Taarifa kuhusu vurugu hizo zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi lilitumia maji ya kuwasha pamoja na mabomu ya machozi kutawanya watu waliokuwepo kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na CHADEMA mjini Kahama.

Mkutano huo ulikuwa ni uzinduzi wa ‘Dai Demokrasia’ ambapo Jeshi la Polisi liliingilia kati na kuuzuia ikiwa ni muda mchache baada ya Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa nchini.

“Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya habari limebaini kuwa, mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder),” ilieleza taarifa ya Nsato Mssanzya, Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Makao Makuu jijini Dar es Slaam jana

Vurugu hizo zilianza saa nane mchana baada ya polisi waliojiandaa kufika kwenye eneo la tukio na kisha kuuzuia kufanyika mkutano huo.

Hatua ya polisi kutoa maelezo ya kuzuia mkutano huo na kutaka watu watawanyike ilianza kuzua mzozo na hatimaye vurugu ambapo wananchi waliokuwa kwenye viwanja vya mkutano vya CDT walianza kupambana na polisi.

Hali hiyo iliwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha huku wananchi wakitumia mawe kukabiliana na mshindo wa polisi Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU).

Hayo yalifanyika ikiwa tayari Mbowe pamoja na viongozi wenzake wakiwa tayari wamewasili kwenye mkutano huo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, Mbowe, Dk. Vincent Mshinji, Katibu Mkuu wa CHADEMA pamoja na wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge walizingirwa na polisi huku wakimwagiwa maji ya kuwasha wakiwa kwenye magari yao.

Hali hiyo inaelezwa kuwazidisha hasira wananchia waliokuwa wamekwenda kuhudhuria ufunguzi huo na kusababisha kuwatupia mawe polisi.

Kabla ya tukio hili, yalianza majibizano kati ya polisi na viongozi wa CHADEMA kwa kutumia vipaza sauti.

Polisi walitumia kipaza sauti kilichokuwa kwenye gari lao kwa kusema “Tangazo, tunawataka wananchi mliopo kwenye uwanja huu muondoke kwa sababu mkutano huu si halali. Ondokeni eneo hili kwa ajili ya usalama wenu. Huu mkutano si halali.”

Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) alishika kipaza sauti na kupuuza tangazo la polisi.

“Hapa polisi CCM wasituvuruge. Jamaa wametupa wenyewe barua ya uturuhusu tufanye mkutano wetu, leo wanakuja na washawasha zao kuzuia, ebooh!” alisema Mwita.

Wakati akipuuza tangazo hilo wananchi waliokuwepo kwenye uwanja huo walikuwa wakimshangilia.
 
MAGUFULI KAMA ANGETAKA KUUA UPINZANI KAZI RAHISI TU,si anatuaminisha mtetezi wa wanyonge na anatumbua majipu ,mwisho wa siku wananchi tungekuja kuelewa TU kati ya CCM ya Magufuli na UPINZANI nani mtetezi wa kweli wa wananchi maskini
 
Miezi Sitta Tu Tayari Wanatembelea Magoti Ikifika Minne Si Watatembelea Ndimi!
Mbowe Tuko Nyuma Yako na Bega kwa Bega Kuleta Mabadiliko!
#FreeMalisaGodlisten!
Safari hii mtakoma maana zero ndiyo kashika akili zenu. Tena ningekuwepo mimi hapo kahama ningewachapa zaidi, mnatakiwa mukomeshwe kwa akili zenu za kizezeta! Sasa tunahitaji kufanya kazi na siyo maandamano au kueneza chuki. Yaani mpaka 2020 hamtakuwa na wafuasi maana sasa kila mwananchi anamkubali Dr Magufuli
 
jisemee mwenyewe, hatujakupa kibali sisi kama wananchi kututolea tamko kwamba wote tunamkubali, acha ujesca ebooo!!!!
 
Safari hii mtakoma maana zero ndiyo kashika akili zenu. Tena ningekuwepo mimi hapo kahama ningewachapa zaidi, mnatakiwa mukomeshwe kwa akili zenu za kizezeta! Sasa tunahitaji kufanya kazi na siyo maandamano au kueneza chuki. Yaani mpaka 2020 hamtakuwa na wafuasi maana sasa kila mwananchi anamkubali Dr Magufuli
sasa kama kila mwananchi anamkubali Makufuli si waachiwe tu,wautubie hewa, kweli kuwa mwana CCM lazima ujitoe Akili
 
Si mwanaukawa wala sikuunga mkono gia kubadilishwa angani-lakini kwa hili nwaunga mkono UPINZANI. Sasa Chama cha siasa kitakuwaje chama kama hakiruhusuwi kufanya mikutano, maandamano etc. Toka JPM ameingia ni wazi wapinzani wamebanwa au kwa jina lingine DEMOKRASIA jnavurugwa. Na si wapinzani tu hata sisi tusio kuwa na vyama ndio tunapotezewa kabisa. Kwa kifupi serikali hii inaleta giza totoro. "Taarifa tulidhopata dha ki-interrigisia dhina-onyesha kuna viashiria.........". Hawa ni wakupelekwa mahakamani wanavunja haki za binadamu mchana kweupe.
 
ahahaha,Malisa yuko Nyuma yako,ebu geuka umwone!kumbe mnamwogopa,enhe?
Ulivyo kiazi mbatata uogopwe umekuwa nani.... Magu kawapiga ban kila kona hata hapa jf mtapigwa ban tu we subiri sijui mtauzia wapi upuuzi wenu....
 
Safari hii mtakoma maana zero ndiyo kashika akili zenu. Tena ningekuwepo mimi hapo kahama ningewachapa zaidi, mnatakiwa mukomeshwe kwa akili zenu za kizezeta! Sasa tunahitaji kufanya kazi na siyo maandamano au kueneza chuki. Yaani mpaka 2020 hamtakuwa na wafuasi maana sasa kila mwananchi anamkubali Dr Magufuli

Inasikitisha!!!!
 
Back
Top Bottom