Mbowe: Haturudi nyuma

Mbowe: Haturudi nyuma

KAZI imeanza. Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya Serikali ya Rais John Magufuli jana kusababisha vurugu kubwa Kahama mkoani Shinyanga.

NI kwa mara ya kwanza ndani ya utawala wa Rais Magufuli, taifa linashuhudia vurugu za kisiasa zinazotokea kwa mgongo wa Jeshi la Polisi nchini.

Vurugu kubwa imetokea jana baina ya Jeshi la Polisi na wananchi kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusababisha sintofahamu.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA amesema kuwa, pamoja na vitisho vya demokarsia nchini, chama hicho hakitarudi nyuma kudai haki.

Mbowe amesema kuwa, wataendelea kudai haki ya demokrasia nchini ndani ya mahakamani, bungeni, ndani na nje ya nchi.

“Huu ni mwendelezo wa serikali na mabavu. Hawataki vyama vingine vya siasa kufanya mikutano,” amesema Mbowe na kuongeza kwamba, watakwenda mahakamani na kuongeza.

Taarifa kuhusu vurugu hizo zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi lilitumia maji ya kuwasha pamoja na mabomu ya machozi kutawanya watu waliokuwepo kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na CHADEMA mjini Kahama.

Mkutano huo ulikuwa ni uzinduzi wa ‘Dai Demokrasia’ ambapo Jeshi la Polisi liliingilia kati na kuuzuia ikiwa ni muda mchache baada ya Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa nchini.

“Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya habari limebaini kuwa, mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder),” ilieleza taarifa ya Nsato Mssanzya, Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Makao Makuu jijini Dar es Slaam jana

Vurugu hizo zilianza saa nane mchana baada ya polisi waliojiandaa kufika kwenye eneo la tukio na kisha kuuzuia kufanyika mkutano huo.

Hatua ya polisi kutoa maelezo ya kuzuia mkutano huo na kutaka watu watawanyike ilianza kuzua mzozo na hatimaye vurugu ambapo wananchi waliokuwa kwenye viwanja vya mkutano vya CDT walianza kupambana na polisi.

Hali hiyo iliwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha huku wananchi wakitumia mawe kukabiliana na mshindo wa polisi Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU).

Hayo yalifanyika ikiwa tayari Mbowe pamoja na viongozi wenzake wakiwa tayari wamewasili kwenye mkutano huo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, Mbowe, Dk. Vincent Mshinji, Katibu Mkuu wa CHADEMA pamoja na wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge walizingirwa na polisi huku wakimwagiwa maji ya kuwasha wakiwa kwenye magari yao.

Hali hiyo inaelezwa kuwazidisha hasira wananchia waliokuwa wamekwenda kuhudhuria ufunguzi huo na kusababisha kuwatupia mawe polisi.

Kabla ya tukio hili, yalianza majibizano kati ya polisi na viongozi wa CHADEMA kwa kutumia vipaza sauti.

Polisi walitumia kipaza sauti kilichokuwa kwenye gari lao kwa kusema “Tangazo, tunawataka wananchi mliopo kwenye uwanja huu muondoke kwa sababu mkutano huu si halali. Ondokeni eneo hili kwa ajili ya usalama wenu. Huu mkutano si halali.”

Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) alishika kipaza sauti na kupuuza tangazo la polisi.

“Hapa polisi CCM wasituvuruge. Jamaa wametupa wenyewe barua ya uturuhusu tufanye mkutano wetu, leo wanakuja na washawasha zao kuzuia, ebooh!” alisema Mwita.

Wakati akipuuza tangazo hilo wananchi waliokuwepo kwenye uwanja huo walikuwa wakimshangilia.
Ohhh lala! Mzee wa kubadilishia GIA ANGANI bado yupo..... sasa hivi anakanyaga klach za BODA BODA
 
Mshaija toka bunge la bajeti lianze kuna habari ipi hujaisikia?
Wahaya mnadai nyie ni vichwa,yaani umeingia mkenge kuwaamini wasanii

Sijayasikia au kuona mengi sana kwa kuwa kuna tofauti kubwa kati ya live coverage na edited and recorded broadcasting.
Hapo ndiyo tafauti yako na Mshaija maana anajuwa tofauti.
 
Huyu mbowe anamaanisha nini hivi, mbona kila siku upinzani unarudi kaburini kwa kiasi?
 
"Hawa jamaa kumbe huwezi kuwahonga ili wabadilishe nyeusi kuwa nyeupe!"
Hayo ni maneno yaliyokuwa yanasemwa na abiria mmoja ndani ya departure Lodge ya uwanja wa ndege Mwanza wakati wa mjadala juu ya msimamo wa wabunge kugoma kuingia iwapo Tulia yupo mpaka suala lake litakapo shughulikiwa.
Wengi wamepongeza msimamo huo pamoja na kuambiwa watakatwa posho.
Hii imeonyesha wananchi kuwa hawakufuata posho na pia kukosekana kwao bungeni kumetoa picha halisi ni wabunge wa aina gani hao waliobaki kutokana na michango yao isiyo na faida kabisa.
Abiria mwingine alisema hata debate sessions za Shule za sekondari ni bora zaidi ya vikao vinavyo endelea baada ya kutoka Ukawa.
 
Duh! Mkuu, ina maana hiyo departure ya airport ya Mwanza imekuwa local zaidi kiasi ambacho mijadala kama hiyo hujadiliwa? Only in Tanzania. Sijapata kuona uwanja wowote wa kimataifa kunaibuka mijadala ya aina hiyo labda kwenye stand ya basi ama kituo cha daladala
 
Watu watatu au wanne mnaojuana hamuwezi kuwa na jambo mnaliongea? Au uhuru huo wananyimwa?
Chakaza ameidaka na kama ilivyo kawaida ya JF, kitu kizuri kula na wenzako
 
Kwanza siku zote haki haitolewi kama sadaka hupiganiwa kurudi nyuma ni mwiko makamanda
 
Hiki ni kipindi kigumu sana kwa viongozi wetu wa vyama vya upinzani hasa cdm na ukawa kwa ujumla kutokana na misuko suko wanayo ipata na kwa kufikishwa mahakamani na si ajabu kuna wengine wanaweza kufungwa,lkn hayo yasiwavunje moyo maana huo hasa ndio upinzani wa kweli kumbukeni kuwa hakuna mtawala aliye kabidhi madaraka kwa mpinzani wake kwa sherehe, jikumbushe yaliyo tokea kwa Nelson Mandela, nasi wananchi tupo bega kwa bega nanyi kwa maombi na sala......mungu awabariki sana.....
 
Ni kweli kupata haki ni ngumu lazima uwe na roho ngumu mapambano yaendelee
 
Hiki ni kipindi kigumu sana kwa viongozi wetu wa vyama vya upinzani hasa cdm na ukawa kwa ujumla kutokana na misuko suko wanayo ipata na kwa kufikishwa mahakamani na si ajabu kuna wengine wanaweza kufungwa,lkn hayo yasiwavunje moyo maana huo hasa ndio upinzani wa kweli kumbukeni kuwa hakuna mtawala aliye kabidhi madaraka kwa mpinzani wake kwa sherehe, jikumbushe yaliyo tokea kwa Nelson Mandela, nasi wananchi tupo bega kwa bega nanyi kwa maombi na sala......mungu awabariki sana.....

Watu mu wanafiki sana. Unayewapa pole hata jina tu hutaki kujitaja. Halafu unaongea nyuma ya keyboard. Kuwasaidia uwashauri wasivunje sheria.
 
Kabisa mkuu maana kipindi hiki ndio haswa upinzani unaonekana kuliko kipindi chote kwani kila siku utasikia mbunge fulani kafikishwa mahakamani

Washaurini waache ukorofi dhidi ya sheria
 
Watu mu wanafiki sana. Unayewapa pole hata jina tu hutaki kujitaja. Halafu unaongea nyuma ya keyboard. Kuwasaidia uwashauri wasivunje sheria.
Sikushangai kwa bandiko lako hili,unajua nini maana ya uwakilishi?au ulitaka wote twende bungeni?
 
Back
Top Bottom