Mbowe: Haturudi nyuma

Mbowe: Haturudi nyuma

KAZI imeanza. Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya Serikali ya Rais John Magufuli jana kusababisha vurugu kubwa Kahama mkoani Shinyanga.

NI kwa mara ya kwanza ndani ya utawala wa Rais Magufuli, taifa linashuhudia vurugu za kisiasa zinazotokea kwa mgongo wa Jeshi la Polisi nchini.

Vurugu kubwa imetokea jana baina ya Jeshi la Polisi na wananchi kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusababisha sintofahamu.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA amesema kuwa, pamoja na vitisho vya demokarsia nchini, chama hicho hakitarudi nyuma kudai haki.

Mbowe amesema kuwa, wataendelea kudai haki ya demokrasia nchini ndani ya mahakamani, bungeni, ndani na nje ya nchi.

“Huu ni mwendelezo wa serikali na mabavu. Hawataki vyama vingine vya siasa kufanya mikutano,” amesema Mbowe na kuongeza kwamba, watakwenda mahakamani na kuongeza.

Taarifa kuhusu vurugu hizo zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi lilitumia maji ya kuwasha pamoja na mabomu ya machozi kutawanya watu waliokuwepo kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na CHADEMA mjini Kahama.

Mkutano huo ulikuwa ni uzinduzi wa ‘Dai Demokrasia’ ambapo Jeshi la Polisi liliingilia kati na kuuzuia ikiwa ni muda mchache baada ya Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa nchini.

“Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya habari limebaini kuwa, mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder),” ilieleza taarifa ya Nsato Mssanzya, Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Makao Makuu jijini Dar es Slaam jana

Vurugu hizo zilianza saa nane mchana baada ya polisi waliojiandaa kufika kwenye eneo la tukio na kisha kuuzuia kufanyika mkutano huo.

Hatua ya polisi kutoa maelezo ya kuzuia mkutano huo na kutaka watu watawanyike ilianza kuzua mzozo na hatimaye vurugu ambapo wananchi waliokuwa kwenye viwanja vya mkutano vya CDT walianza kupambana na polisi.

Hali hiyo iliwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha huku wananchi wakitumia mawe kukabiliana na mshindo wa polisi Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU).

Hayo yalifanyika ikiwa tayari Mbowe pamoja na viongozi wenzake wakiwa tayari wamewasili kwenye mkutano huo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, Mbowe, Dk. Vincent Mshinji, Katibu Mkuu wa CHADEMA pamoja na wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge walizingirwa na polisi huku wakimwagiwa maji ya kuwasha wakiwa kwenye magari yao.

Hali hiyo inaelezwa kuwazidisha hasira wananchia waliokuwa wamekwenda kuhudhuria ufunguzi huo na kusababisha kuwatupia mawe polisi.

Kabla ya tukio hili, yalianza majibizano kati ya polisi na viongozi wa CHADEMA kwa kutumia vipaza sauti.

Polisi walitumia kipaza sauti kilichokuwa kwenye gari lao kwa kusema “Tangazo, tunawataka wananchi mliopo kwenye uwanja huu muondoke kwa sababu mkutano huu si halali. Ondokeni eneo hili kwa ajili ya usalama wenu. Huu mkutano si halali.”

Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) alishika kipaza sauti na kupuuza tangazo la polisi.

“Hapa polisi CCM wasituvuruge. Jamaa wametupa wenyewe barua ya uturuhusu tufanye mkutano wetu, leo wanakuja na washawasha zao kuzuia, ebooh!” alisema Mwita.

Wakati akipuuza tangazo hilo wananchi waliokuwepo kwenye uwanja huo walikuwa wakimshangilia.

Pole kijana wangu naona unautaka unaibu katibu mkuu bara kwa nguvu aaaah utaishia kuchoma mahindi
 
#HAPAHOFUTUU ndio falsafa yao. Hivi wanadhani washiriki wa mkutano 20,000 wakiamua kupambana na hao polisi 100 kutakuwa na usalama hapo?
Ni kweli watawaua kadhaa lakini hata baki polisi hata mmoja. Hilo hatutaki litokee katika nchi hii. Wasilazimishe
 
jisemee mwenyewe, hatujakupa kibali sisi kama wananchi kututolea tamko kwamba wote tunamkubali, acha ujesca ebooo!!!!
Polisi wa Kahama waliniudhi sana, walitakiwa kula kichapo hasa hadi wabadili gia angani. Wabunge wako kazini bungeni yy yeye anahamasisha vurugu, kama ana hamu ya kupiga kelele aende HAI kahama ina MBUNGE wake!
 
bila jeshi la polisi kufumuliwa na kuundwa upya nchi yetu ipo hatarini kupoteza umoja, amani na mshikamano wa taifa letu. jeshi hili linatumika kisiasa badala ya kulinda katiba...
 
Ukawa kumbukeni uhuru una mipaka yake,Demokrasia ipi tena inatakiwa?
UHURU hauna mipaka wewe, acha kukariri dhana ya kikoloni,.. uhuru ungekuwa na mipaka hata nchi za marekani na ulaya zingekomea huko huko kutubania pesa za maendeleo
 
Mkuu kwani Malisa nae kashikiliwa na hawa Polisi?
hapana,Facebook imempiga ban ya siku 7,eti kwa kuandika posts za uchochezi!google "Malisa Godlisten" halafu search akaunti yake ya Facebook!kuna watu wamemchongea!
 
hapana,Facebook imempiga ban ya siku 7,eti kwa kuandika posts za uchochezi!google "Malisa Godlisten" halafu search akaunti yake ya Facebook!kuna watu wamemchongea!
Kama wapo waliomchongea basi ni wapuuzi sana, uhuru wa kuongea hauna mipaka, afungue akaunti nyingine tutamfollow tu.
 
Safi sana............. Hii biashara ya serikali kutumia nguvu ya dola dhidi ya raia wanaoeleza kwa njia ya maandamano, mwisho wa siku inaweza kufanya raia watafute njia mbadala ku express their minds
 
Katika hili tuko pamoja sana Kamanda wa Anga MBOWE.

Demokrasia ina gharama yake; lets get united as we can all pay the price
 
Safari hii mtakoma maana zero ndiyo kashika akili zenu. Tena ningekuwepo mimi hapo kahama ningewachapa zaidi, mnatakiwa mukomeshwe kwa akili zenu za kizezeta! Sasa tunahitaji kufanya kazi na siyo maandamano au kueneza chuki. Yaani mpaka 2020 hamtakuwa na wafuasi maana sasa kila mwananchi anamkubali Dr Magufuli

Ndiyo nani huyo?
 
Back
Top Bottom