Mbowe: Hakuna Mwenye Ubavu wa Kuiyumbisha CHADEMA

Dk. Slaa: Tukish ika dola tutaruhusu utengenezaji pombe ya gongo


Saturday, 14 December 2013 · Posted in OMG, Siasa


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.


"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.


Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.


Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.


Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.


"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.
CHANZO: NIPASHE

Unashangaa nini? Kuna gongo huuzwa kila kona imekolezwa harufu ya tofauti na kubandikwa lebo fulani....inaitwa Konyagi. Mbona hiyo huishangai...
 
Mkuu Gamba Sugu, Ziara ya Lipumba Singida upo na hii ya Mbowe Mwanza pia ulikuwepo?

Mbona unajichanganya sanaaa

Singida-Mwanza ni masaa 4 kwa private Car!
Kwa ndege haizidi 45 minutes
Kwa Maji Marefu ni dk.10.
Tehe!
Kwa hiyo wakati unashangaa kafikaje, tafiti kwanza kujua the means of transport...
 
Wachagga munaichukia sana CCM lkn serikalini na kwenye mashirika ya Umma mumejaa nyinyi tu,na ndo mafisadi wenyewe.nasasa munataka Uraisi.
ulitaka upewe wewe kilaza,acha ubaguzi wachaga sio watanzania?????pumba..vu wa pwani wewe
 
Mi ndio MKUU WA KAYA mwenyewe ambaye mara zote huwa nakaa kimya kwa busara na ukiona nakamata mouse na kuanza kuisumbua keyboard basi ujue ninachotaka kuwaambieni ndicho chenyewe.

Mkuu wa kaya nakwabieni hivi CHADEMA haitakufa kwa utiriri kwa kashfa feki na propaganda za wachumia matumbo akina mwigulu na wenzake. CHADEMA ni sawa na jogoo. Mi ndio mzee wa kaya na mkuu wa hii kaya na mfugaji mzuri mwenye weledi. Toka nianze kufuga kuku MAJOGOO huwa hayafi kwa utiriri. Hivyo basi kesheni weeee kwenye twitter, fb, JF na uhuru, mzalendo,jamboleo,tazama tz na kwingine kote CHADEMA/JOGOO hatakufa kwa utitiri. Zaidi zaidi mnazidi kuipaisha. Kuna jogoo aliyewahi kufa kwa utitiri?
 
Pole sana Mkuu. Hata kama haitakufa, CHADEMA itaendelea kuwa SACCOS ya akina mbowe tu na si kutawala Tanzania
 
Kipindi hiki atakufa kwenda kutalii na pesa za umma ni propaganda acheni kuwatetea wezi
 
Aaaaagh jogoo hafi kwa utitili ila sijajua kati CDM na CCM yupi jogoo hapa bila shaka CDM basi kweli haitakufa.
 
Hata wakibaki na wabunge wawili mgao wao ruzuku uko tu. mishahara na posho uko palepale
 
Haita tetereka wala kufa, maana tumesha tolewa ufahamu wana cdm wooooote.
Kila asemacho sie "SAWA KAMANDA"
 
Back
Top Bottom