Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kitazindua kanda ya kichama ya Pwani inayojumuisha mikoa ya Pwani,Kinondoni,Ilala na Temeke.Uzinduzi huo utafanyika siku ya Jumapili tarehe 14/04/2013
Viongozi wakuu wa chama hicho wakiongozwa na Mkiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa ndiyo watakaoongoza uzinduzi huo.
Uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vya maili moja Kibaha na utatanguliwa na maandamano makubwa ya wanachama na wananchi kwa ujumla.
Kibaha imeteuliwa kuwa makao makuu ya Kanda hii ambapo wananchi wengi wa Kibaha wameeleza kufurahishwa na uamuzi huo kwani wamesema ni kuleta madaraka kwa wananchi wenyewe.Kibaha ni ngome kuu ya Chadema kwa ukanda huu wa Pwani.
Source:Tanzania Daima.