Uchaguzi 2020 Mbowe: CHADEMA inafanya kampeni kimkakati, kesho tutakuwa Arusha na keshokutwa Mwanza

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,962
141,961
Mwenyekiti wa CHADEMA mh Freeman Mbowe amesema chama chao kinafanya kampeni za kimkakati na kitovu cha kampeni zao ni jiji la DSM.

Mbowe amesema mgombea urais wa CHADEMA kesho atakuwa jijini Arusha na keshokutwa atakuwa jijini Mwanza kwa shughuli za kampeni.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Chadema wanaonekana kukomaa na majiji na manispaa tu, wakumbuke na maeneo ya pembezoni mwa miji nayo yana umuhimu wake.

Japo naona wanawekeza zaidi kule wanapoona wanakubalika zaidi, sio vibaya kufanya hivyo.
 
Nachokiona mbowe kataarifiwa na benchi la ufundi aende kwanza sehemu ambayo atapata nyomi la wallpaper itakayotumika kutengenezea mabango ya kampeni maana hii ya sasa watu wanasema ni ya lowasa 2015
 
Kweli mkakati kwa sababu kutegemea fedha za michango ya raia kwa kampeni hii hufiki popote . Chadema wapo hoi fedha hazitoki ndio maana kampeni kubwa watafanyia Dar pekee gharama ni ndogo. Poleni makamanda
Inakuhusu? Basi faidika nayo
 
Chadema wanaonekana kukomaa na majiji na manispaa tu, wakumbuke na maeneo ya pembezoni mwa miji nayo yana umuhimu wake.

Japo naona wanawekeza zaidi kule wanapoona wanakubalika zaidi, sio vibaya kufanya hivyo.
Hizo sehemu zina watu wengi hivyo kwa siku jizo watakuwa wamefikia watu mil 19 ya watu
 
Kweli mkakati kwa sababu kutegemea fedha za michango ya raia kwa kampeni hii hufiki popote . Chadema wapo hoi fedha hazitoki ndio maana kampeni kubwa watafanyia Dar pekee gharama ni ndogo. Poleni makamanda
Na unajua vyema nani aliyetufikisha ila tutashinda tu, tuna watu na sio vitu
 
Kweli mkakati kwa sababu kutegemea fedha za michango ya raia kwa kampeni hii hufiki popote . Chadema wapo hoi fedha hazitoki ndio maana kampeni kubwa watafanyia Dar pekee gharama ni ndogo. Poleni makamanda
wabunge mlishawanunua ruzuku hakuna tena tunachanga sisi ww inakuuma nini
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe amesema chama chao kinafanya kampeni za kimkakati na kitovu cha kampeni zao ni jiji la Dsm.

Mbowe amesema mgombea urais wa Chadema kesho atakuwa jijini Arusha na keshokutwa atakuwa jijini Mwanza kwa shughuli za kampeni.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

ITV imejivua uITVCCM ? Imeanza kutumia weledi wa taaluma yao ya habari?!
 
Hy awamu ya kwanza ni majiji na kanda zote.Kisha wanaanza kutembea kwa barabara na herikopta kuingia kijijin. Watarudi tena kwenye majiji yote kwa mara nyingine
 
Back
Top Bottom