Mbowe asita kususia posho

'WaChagga kwa pesa' ina maana kabila nyingine wote hawatafuti pesa? Wabunge waliotetea kuendelea kulipwa posho na wengine kudai iongezwe wote ni waChagga?! I bet you look exactly like your avatar...because that face really suits you!

Thanks Riwa! kweli kabisa huwezi kusema kabila fulani linapenda pesa as if makabila mengine ukiwapa pesa wanakataa this is bullshit!!!kwanini basi makabila yote yanafanya kazi basi wangewaacha wachaga wafanye kazi wao walale home wafe na njaa! Alichokifanya mbowe haina relationship na ukabila, at least yeye amerudisha hilo shangingi, mind you CCM hawawezi kukubali kuwa defeated kirahisi so lzm watafute sehemu ya kumcorner ili waonyeshe umma mbowe ni muongo!! huyo jamaa anayekimbilia kuponda mambo ya ukabila ana narrow thinking
 
Tatizo ccm wanaamin kuwa watz tu bado wajinga,..wamechelewa sana..posho ile ni kwa ajil ya wagen na sio yake.. Ni ya ofis ya upinzan.. hawez kuikataa wagen wakija watahudumiwaje?chadema hawakusema wafute gharama za uendeshaji bal wafute matumiz yasiyo ya lazima ndo kama hvo mashanging,sitting allowance n.k..TUTAFIKA TU
 
Gazeti la Mwananchi la jana ambalo halijachakachuliwa majibu ya Mbowe yalikuwa,fedha za viburudisho zinatolewa kwa vipindi na sio kila mwezi kama mwanzisha mada anavyosema,Bravo Mbowe kwa kurudisha gari wamechanganyikiwa CCM wasipoyarudisha ile nyongeza ya bajeti inayotakiwa ijazwe na wafahili hawataipata ,moja tu litakuwa vipi nyie mbona upinzani wamerudisha Shangingi nyie munayatumia wakati hata nchi zetu viongozi wetu hawatumii magari ya aina hiyo,lazima wachanganyikiwe hawaelewi watatokaje
 
hapo ndipo wanasiasa wa dunia hii wanaponiacha na alama za mshangao
 
Hiii ndo bongo politician movies,dah yangoswe muachie ngoswe bt its good, alwayz masive&true revolution sparked by full pain so,ipo day wote hatuwezi kuwa wajinga kiasi hicho kila Mtz elimu ya uraia itamfikia na hapo ndo mwanzo wa ukomozi.ipo na inakuja ata Misri imeanzia ivi ivi kwa Gadaf nako, inayo fuatia ndo hapa
 
Soda na chai kwa wageni wa KUB ni Tshs. 2,000,000.00 kwa mwezi na kwa mwaka Tshs. 24,000,000.00!! Wakati kima cha chini ni Tshs. 120,000.00 kwa mwezi na mwaka ni Tshs. 1,440,000.00 kwa Mtanzania wa kawaida! Jamani jamani kama kweli Mbowe ana huruma kwa Watanzania akatae hii pesa ya viburudisho ofisini kwake. Hii ni kufuru kabisa tena dhihaka kwa watanzania wanaopata kima cha chini! Yaani Kiongozi wetu anatumia mara mbili ya pesa unayopata kwa mwaka kwa ajili ya kuwanunulia wageni wake soda kwa mwezi mmoja tu!!
Mkuu, kuna gari lingine pia kapewa na serikali afanyie kazi zake sijui kama mnajua nyie Pro-Chadema-JF, mnaofata mkumbo ilo bado analo tofauti na ilo shangingi, mwambieni nalo aliache sio kuleta usanii
 
mkubwa kashikwa pabaya...... ngoja tuone utetezi!alianza vizuri nami nilimsapoti, ila hili "VIBURUDISHO" hapana
serikali ya ccm ipo kuwanyonya watanzania iweje baba wa taifa alikataa kujengewa nyumba ya kifahari ila cha kushangaza wakamlazimisha so ata kwa Mbowe sinto shangaa badala wamshukuru kwa kugunguza matumizi ya serikali wanamdhihaki na kumkejeli.
 
itakuwa ajabu sna kumshangaa kumshangaa Mbowe kusita kuchukua posho naamini anasimamia imani yake c km wakina Zitto wanasema hawataki ili hali roho zinawauma.
 
Thanks Riwa! kweli kabisa huwezi kusema kabila fulani linapenda pesa as if makabila mengine ukiwapa pesa wanakataa this is bullshit!!!kwanini basi makabila yote yanafanya kazi basi wangewaacha wachaga wafanye kazi wao walale home wafe na njaa! Alichokifanya mbowe haina relationship na ukabila, at least yeye amerudisha hilo shangingi, mind you CCM hawawezi kukubali kuwa defeated kirahisi so lzm watafute sehemu ya kumcorner ili waonyeshe umma mbowe ni muongo!! huyo jamaa anayekimbilia kuponda mambo ya ukabila ana narrow thinking
Acha unafiki wewe! Leo ndio umeona kuponda kabila ndio norrow thinking? au kwa sababu wewe ni Mchagga ndio imekuuma? Hiyo tabia ya kuponda makabila imeletwa humu JF, na Pro-CDM-JF, mara kibao wanapondwa Wakweree, Wapemba, watu wa pwani. Waarabu, mbona uwa sikuoni kupinga ilo acha unafiki
 
I said it before, kwamba subirini majibu ya CCM na ndiyo mtajua they are working against us. Hivi pinda livyokataa hiyo sijui VX aliitwa mnafiki na muongo mkubwa? Aliambiwa aachie na nyumba pamoja na expenses ya ofisi yake???

Yaani kweli nchi yetu ni mafala, watu wanaong'ang'ania hizo posho na migari wasiyostahili wanaonekana eti ndiyo heroes na the only one aliyerudisha hilo shangingi eti ndiyo wa kuwa attacked. "ONLY IN TANZANIA"
 
NINANUKUU...... "Soda na chai kwa wageni wa KUB ni Tshs. 2,000,000.00 kwa mwezi na kwa mwaka Tshs. 24,000,000.00!! Wakati kima cha chini ni Tshs. 120,000.00 kwa mwezi na mwaka ni Tshs. 1,440,000" MWISHO WA KUNUKUU
Hebu ulizia Soda na Chai kwenye Ofisi ya Spika
 
I said it before, kwamba subirini majibu ya CCM na ndiyo mtajua they are working against us. Hivi pinda livyokataa hiyo sijui VX aliitwa mnafiki na muongo mkubwa? Aliambiwa aachie na nyumba pamoja na expenses ya ofisi yake???
Yaani kweli nchi yetu ni mafala, watu wanaong'ang'ania hizo posho na migari wasiyostahili wanaonekana eti ndiyo heroes na the only one aliyerudisha hilo shangingi eti ndiyo wa kuwa attacked. "ONLY IN TANZANIA"
Wanafki tu hao? Ungesikia walivyokua wanamsifia Pinda kwa kurudisha VX, leo wanamuona Mbowe mnafski!!
Kusema kweli hakuna kitu kinachonikasirisha nikisia hawa magamba wanaongea. Point ya mbowe ni kupunguza gharama za uedeshaji leo mtu anakuja anasema akatae posho zote. hivi kweli hawa jamaaa wanatumia migongo nini katika kufikiria?
 
Wabongo na akili za kushikiwa! Hivi mwandishi aliyeenda kumhoji Mbowe anashindwa nini kuwahoji vingozi wengine tujue wanapata kiasi gani kama fungu la viburudisho?! Jamani kwa waandishi wote mlioko humu wekeni hadharani bajeti za 'viburudisho' za ofisi kubwa zote za uma.
 
Hivi kama Mbowe kaanza kwa kurudisha gari, kwa nini wengine wasifuate kwa walau kusema Posho fulani zipunguzwe?

Hivi Lowassa, Chenge, Rostam, Membe nk hawawezi kutumia magari yao ili kuokoa hela za walalahoi?

Hivi Chai za Ikulu, Bunge, Wizara ...... kwa mwezi ni shilingi ngapi?

Kwa nini watu wanakomalia kambuzi wakati nina imani kuna watu wana nyati na wamekaa kimya?

Kama Zitto alianza, Mbowe kafuata, kwa nini sioni Gamba moja la CCM likija na njia nyingine ya kubana matumizi?

Eti Mbowe mnafiki, ebo......... Kwani mnafikiri hatuna macho na masikio? Ngoja Slaa aje hapa na Chai za Serikali ya CCM/CCM yenyewe.
 
Aje nazo tuziangalie tuzikemee si zinatokana na kodi zetu? Posho ni hatari
 
muwe na akili, milioni mbili kwa mwezi ni hela ya kurun ofisi ya bunge kambi ya upinzani..... labda siku mmgetafuta usafiri na kuja kuangalia how the place is busy kabla ya kusema...vitu vingine ni sawa na kusema binadamu asivae nguo ...hilo haliwezekani, lakini asivae nguo ya gharama kubwa hiklop linawezekana...

vitu ni hatua, na there is logic in every thing...kitu ambacho nadhani ni more appropriate ni kwamba Mbowe anapaswa kuomba ABADILISHIWE USAFIRI na apewe wa gharama nafuu......KWA SABABU USAFIRI NI STAHILI YAKE

hapa atakuwa amewakata kilimi vizabizabina wote.....

watz sio wajinga hivyo jamani..wanamagamba!
 
Siku moja nilikuwa na profesa wa kiholanzi na tukatembelea ukumbi wa bunge!! Kimsingi alishtushwa na ule umati wa LUXURIOUS 4wd pale uwanjani....NJIA NZIMA MPAKA NAMPELEKA AIRPORT ALIKUWA ANAWEWESEKA
 
Cdm lengo lao ni kupunguza matumizi, na siyo kufuta matumizi. wabunge wa Ccm nao warudishe magari ya Tzs 90m/= kisha wapate posho. huwezi kukwepa matumizi bali unaweza kuyapunguza yale ambayo hayana tija. Ofisi ya mkuu wa kambi lazima iendeshwe na ndicho anachofanya m/kiti wa cdm.
 
Ofisi lazima iendeshwe vinginevyo hakuna maana ya kuwa na ofisi. Tatizo hapa labda tumeongopewa kwamba anachukua Tshs. 2,000,000.00 kwa ajili ya posho ya viburudisho. Je hiyo pesa ianakuwa accounted for au? Tatizo lingine ambalo bado halijafafanuliwa ni kwamba je pesa hizi analipwa Mbowe in person kama KUB au inalipwa Ofisi ya KUB?
 
Soda na chai kwa wageni wa KUB ni Tshs. 2,000,000.00 kwa mwezi na kwa mwaka Tshs. 24,000,000.00!! Wakati kima cha chini ni Tshs. 120,000.00 kwa mwezi na mwaka ni Tshs. 1,440,000.00 kwa Mtanzania wa kawaida! Jamani jamani kama kweli Mbowe ana huruma kwa Watanzania akatae hii pesa ya viburudisho ofisini kwake. Hii ni kufuru kabisa tena dhihaka kwa watanzania wanaopata kima cha chini! Yaani Kiongozi wetu anatumia mara mbili ya pesa unayopata kwa mwaka kwa ajili ya kuwanunulia wageni wake soda kwa mwezi mmoja tu!!

Hebu twende taratibu,hivi hizo hela aliziweka nani,na ni serikali ya chama gani inalipa hizo posho.
 
Back
Top Bottom