Mbowe asita kususia posho

Tuna tatizo pia la kuchanganua mambo, kuna watu wanasubiri mpaka wapewe kauli na CCM ndio waseme!! Hoja ya msingi inaeleweka, kupunguzama gharama, na yeye amependekeza mojawapo ni hiyo, badala ya kuukubali ukweli huo na kuujadili kwa maslahi ya Taifa watu wanaanza kuzungumzia mil.2 za kuendesha ofisi, what a shame!!
 
ukishikiwa akili hutashughulisha ubongo kunawachangiaji humu kama akili zao ziko likizo kabisa. uelewa ni jambo la muhimu sana hasa unapoongelea jambo nyeti la taifa hela zinazoongelewa ni posho kupunguzwa wala si kufuta posho zote. naomba tuwe na ufahamu kwa kiasi na tuangalie kwa mapana si kila kitu tushabikiee tu au tubishane
 
Ofisi lazima iendeshwe vinginevyo hakuna maana ya kuwa na ofisi. Tatizo hapa labda tumeongopewa kwamba anachukua Tshs. 2,000,000.00 kwa ajili ya posho ya viburudisho. Je hiyo pesa ianakuwa accounted for au? Tatizo lingine ambalo bado halijafafanuliwa ni kwamba je pesa hizi analipwa Mbowe in person kama KUB au inalipwa Ofisi ya KUB?

hii ni underw**r ya nipe
 
Kwanini watu mnakosa msimamo kiasi hiki?
Ishu ni Mbowe au kuipunguzia serikali mzigo wa gharama?
Hamuoni kuwa mbowe ni mzalendo wa juu sana kwa kitendo alichofanya?...tungekuwa msitari mmoja katika uelewa hii thread isingwekuwa subject-matter!

Angekuwa mzalendo angeacha kufuja fedha zetu kwenye vitafunwa na viburudisho. Alipokuwa akiwasilisha hotuba yake alionesha kuchukizwa na jinsi serikali inavyotumia vibaya fedha kununua vitumbua, maandazi, mayai, chapati etc. Shs 2,000,000 kwa mwezi anazotumia yeye kwa viburudisho si pesa sawa na pesa inayotumiwa na serikali?

Na issue ya nyumba mbili alizopewa na govt, moja Dom, nyingine Dar, ... Kwa nini asionyeshe mfano kwa kuzikataa pia?

Huu ni unafiki na usanii wa kisiasa... Chadema's cheap politics!
 
'WaChagga kwa pesa' ina maana kabila nyingine wote hawatafuti pesa? Wabunge waliotetea kuendelea kulipwa posho na wengine kudai iongezwe wote ni waChagga?! I bet you look exactly like your avatar...because that face really suits you!
Mkuu usipoteze muda wako kubishana na mtu kama huyu!yeye yupo kazini!!
 
Amejaribu kwa kweli , ila hili la viburudisho mil. 2 !!??? Hapana , wamueleweje waalimu , wafanyakazi wa kima cha chini wapatao 120,000 kwa mwezi , askari wa site wanaovuna 65,000 kwa mwezi ??? Hii ni kufuru ya matumizi
 
..mbona Mwalimu Nyerere alihama Ikulu kwenda kuishi kwenye nyumba yake msasani?

..mbona Salim Salim alipoteuliwa Waziri Mkuu hakuhamia kwenye nyumba ya serikali bali aliendelea kuishi nyumbani kwake masaki?

..kama Mbowe ameamua hataki kutumia gari la serikali sidhani kama ni kitu kibaya. watendaji wa bunge wanakosea wanapomlazimisha aachie na mafao mengine kama ofisi, na posho.

jamani nja ndio inasumbua kwenye siasa popote duniani.............na bila kushiba siasa haiwezi kufanyiwa kazi..ndio maana wanatakiwa mara nyingi viongozi ambao tayari wameshiba kufanya mambo ya siasa......sio unafanya kazi za siasa kwa kutaka kupata maendeleo.........Chadema walivyosemaga hawamtambui rais na Serikali na kutoka Bunguni wote ,asubuhi yake walikuwa wamepanga foleni kwenda kuchukua posho zinazotolewa na serikali..........na usiku unaofuata walikuwa wana gongesha Glass za beer kwenye Coctail ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya wabunge na Raisi .............CHADEMA WAWE NA MISIMAMO YA KWELI
 
Kweli Kabisa Wadau, kama kweli Chadema na Mbowe wanauchungu wa kweli na Pesa za Umma, inabidi waende mbele kukataa Posho za namna hii!.
Ni dhulma kubwa kwa Wavuja jasho wa Nchi hii.

Hata hivyo ninawapongeza Chadema kwa moyo wa kijasiri walioonyesha, wa kukataa sitting allowances na Shangingi, hata hivyo hiyo ni symbolic zaidi kwani tunahitaji juhudi kama hizo zihamie katika posho nyingine zilizobaki kama vile "posho za Viburudisho" n.k. Taifa changa kama letu linahitaji kubana matumizi sana, na ni bora watunga sheria wetu wakawa msitari wa mbele katika hilo!.
 
Mbowe kweli ni mnafiki na muongo sana, kama kweli anayo dhamira ya kweli mbona anachagua posho kama umeamua kususia posho usichukue posho yoyote Wachagga kwa pesa!! Endelea kuwadanganya Pro-Chadema-JF, ndio wengi wana upofu wa fikra
you are just like your avatar... confused and depressed

take time to know why
 
Acha unafiki wewe! Leo ndio umeona kuponda kabila ndio norrow thinking? au kwa sababu wewe ni Mchagga ndio imekuuma? Hiyo tabia ya kuponda makabila imeletwa humu JF, na Pro-CDM-JF, mara kibao wanapondwa Wakweree, Wapemba, watu wa pwani. Waarabu, mbona uwa sikuoni kupinga ilo acha unafiki
na wewe una mawazo FINYU sana. Wanaoleta hizo hoja ni wana cdm, halafu eti wachaga. Na ww akili yako inakutuma hivyo? Kwa mantiki hiyo ukaingia mkumboni? Akili huna!
 
Wadanganyika bana, mnaparuana makucha tu hapa wakti wenzenu wanakula nchi kwa gharama zetu. Ukweli ni kwamba kila mwanasiasa Tz is part and parcel of the downfall of this country kwa sababu his/her conformation of the current administration setup. Kama mnabisha waambie waondoe masurufu kwene kila nafasi ya siasa uone kama kutabakia 'mwanasiasa'. Kila mmoja ataingia mitini.
 
Kweli Kabisa Wadau, kama kweli Chadema na Mbowe wanauchungu wa kweli na Pesa za Umma, inabidi waende mbele kukataa Posho za namna hii!.Ni dhulma kubwa kwa Wavuja jasho wa Nchi hii.Hata hivyo ninawapongeza Chadema kwa moyo wa kijasiri walioonyesha, wa kukataa sitting allowances na Shangingi, hata hivyo hiyo ni symbolic zaidi kwani tunahitaji juhudi kama hizo zihamie katika posho nyingine zilizobaki kama vile "posho za Viburudisho" n.k. Taifa changa kama letu linahitaji kubana matumizi sana, na ni bora watunga sheria wetu wakawa msitari wa mbele katika hilo!.
Mnataka "juhudi kama hizo zihamie ktk posho nyingine zilizobaki.....!! Chadema wamekataa posho ya vikao ccm wanailamba, Chadema wamerudisha shangingi la Mbowe mawaziri wa ccm hawarudishi, wananchi bila aibu 'tunaidai' Chadema mengine zaidi wakati haya tu tumeshindwa kuisaidia!! Hivi hiyo 'posho ya viburudisho' inaenda ofisi ngapi hapa Tz na jumla ni sh. ngapi?! Chadema wametuonyesha kuna matumizi mabaya serikalini sisi wananchi tumechukua hatua gani??? Ni matumizi mangapi ya serikali hii ni mabaya lakini yamefichwa?! Vyama vya wafanyakazi viko wapi? Nilitegemea kuona juhudi kubwa toka kwao kudai matumizi yote ya viongozi na ofisi za serikali yawekwe wazi ili kila mTanganyika aone uozo uliopo... Badala yake wote wamebaki kukodoa macho kwa Chadema inafanya nini na kuimba upupu wa ccm eti 'kama Chadema ina uchungu' ifanye hiki na kile... Tumezoea misaada kiasi cha kuwa mazezeta! Nchi ni yetu, tunaonyeshwa hapa pana tatizo....jibu letu; Chadema ifanye hivi Chadema ifanye vile !! Hivi hata huko jeshini hakuna watu wenye akili wayalipue haya majizi ya ccm watu washike adabu tuanze moja??? Agggrrrrrrr! Na weekend yangu imeharibika, pambaf
 
Wakuu nchi yoyote duniani inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni. Haya masuala ya Waziri Mkuu kakataa VX V8, Mbowe kakataa shangingi la KUB, Zitto kakataa posho ni usaniii mtupu. Hivi kama PM na KUB wamekataa magari bila kubadilisha utaratibu kuna tija kweli hapo, je akija PM na KUB mwingine na akaamua kuvikubali is itakuwa ni sawa tu? Huu ni usanii wa kisiasa tu.

Hivi kwa mujibu wa kanuni za stahili za mawaziri wa Tanzania, Waziri inatakiwa atumie gari aina gani au ni kila mtu anaamua kununua gari anayoipenda? Kama ni kila mtu kuamua kununua gari anayoipenda basi kuna tatizo kubwa. Na kama kuna gari ambalo limeamuliwa kuwa ni la waziri, PM ama KUB na kuna sehemu limeandikwa inabidi tuyaangalie hayo maandiko badala ya utashi wa mtu; nchi haiwezi kuendeshwa kwa utashi.

Stahili za viongozi wetu ziwekwe hadharani tuzijadili na kuziweka barabara na si kutegemea tu utashi wa watu. Tuwe na makubaliano kimaandishi.

Hizi za kwamba KUB kakataa basi na waziri mwingine akatae si hoja kwa kuwa huo ni utashi. Zitto kakataa posho basi na ole sendeka azikatae; huo ni utashi na mtu anaweza kuutumia kujitafutia umaarufu ambao si wa kudumu. CHADEMA wameonyesha kwa mmoja mmoja kuwa hawataki posho na gari, huo ni mwanzo mzuri inabidi kuwe na shinikizo kubwa ili taratibu zibadilishwe.
 
Muzee hat-off. Hoja zako madhubuti.

Hizi za 'kukataa' ni sarakasi za kisiasa za ku-fool the gullible, kama ukiniuliza.

Mkakati wa kubana matumizi ni mzuri lakini lazima uwekewe taratibu, otherwise mambo ya utashi, kama ulivosema it won't help that much.

Kama kweli wapo serious na kubana matumizi kwanza wafute hilo bunge lenyewe, the biggest white elephant ambalo ni mzigo mkubwa sana kwa mlipa kodi, kama ukiniuliza.
 
Wakuu nchi yoyote duniani inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni. Haya masuala ya Waziri Mkuu kakataa VX V8, Mbowe kakataa shangingi la KUB, Zitto kakataa posho ni usaniii mtupu. Hivi kama PM na KUB wamekataa magari bila kubadilisha utaratibu kuna tija kweli hapo, je akija PM na KUB mwingine na akaamua kuvikubali is itakuwa ni sawa tu? Huu ni usanii wa kisiasa tu.Hivi kwa mujibu wa kanuni za stahili za mawaziri wa Tanzania, Waziri inatakiwa atumie gari aina gani au ni kila mtu anaamua kununua gari anayoipenda? Kama ni kila mtu kuamua kununua gari anayoipenda basi kuna tatizo kubwa. Na kama kuna gari ambalo limeamuliwa kuwa ni la waziri, PM ama KUB na kuna sehemu limeandikwa inabidi tuyaangalie hayo maandiko badala ya utashi wa mtu; nchi haiwezi kuendeshwa kwa utashi. Stahili za viongozi wetu ziwekwe hadharani tuzijadili na kuziweka barabara na si kutegemea tu utashi wa watu. Tuwe na makubaliano kimaandishi.Hizi za kwamba KUB kakataa basi na waziri mwingine akatae si hoja kwa kuwa huo ni utashi. Zitto kakataa posho basi na ole sendeka azikatae; huo ni utashi na mtu anaweza kuutumia kujitafutia umaarufu ambao si wa kudumu. CHADEMA wameonyesha kwa mmoja mmoja kuwa hawataki posho na gari, huo ni mwanzo mzuri inabidi kuwe na shinikizo kubwa ili taratibu zibadilishwe.
Mkuu, hicho ndicho ninachokiamini. Sasa naomba unisaidie, hilo shinikizo litawekwa na Chadema pekee??? Ndo maana mi nauliza wananchi na hasa wafanyakazi wa Taifa hili wanafanya nini kuhusu hili. Mi nadhani Chadema kukataa wako sahihi na wala si usanii, wewe mwenyewe umesema nchi inaongozwa kwa sheria zilizopo, wapinzani ni wachache bungeni, bila ccm kukubali hakuna sheria itabadilishwa. Kwanza ccm walianza kupinga na kukebehi hoja hii hata kabla ya kikao cha bunge hili kuanza, bunge lililopita waliwahi kumzomea Dr. Slaa alipoongelea mapato yao. Kama Pinda anawakejeli kuwa wanazimezea mate angesema nini kama wangezipinga huku wakizichukua?! Tatizo liko kwa ccm, na kwa wananchi.
 
Kwanza kabisa nakugongea thanks kwenye kitufe na kukupa kwa maandishi! Tukiwa na mijadala kama hii bila matusi tutafika mbali.

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba wapinzani ni wachache na sheria haziwezi kupita bila CCM kukubaliana na muswada wowote kwa kuwa ni wengi. Umesema pia kwamba Dr. Slaaa alizomewa ni kweli lakini kama unafuatilia utaona kwamba Zitto hakuzomewa sijui kama Mbowe alizomewa. Ninachotaka kusema ni kwamba hii hoja imewaingia hata CCM wenyewe manake wanaona wasipoiangalia inaweza ikaawangusha sana 2015 kwa kuwa hii ni sumu kubwa sana kwa wapiga kura; waalimu, vijana, wakulima, nk. Hao wapiga kura wanaamini kuwa wananyonywa na CCM ndio kinara wa kuwanyonya kupitia kwenye miposho. Kwa hiyo siamini kama kuna Mbunge wa CCM ambaye atasimama na kusema posho ya kikao ni haki, sijamsikia zaidi zaidi walikuwa wakikwepa na kusema posho za Polisi sijui na wanajeshi wastaafu. Kwa hiyo basi serikali na CCM wameisha legea kinatotakiwa ni CHADEMA kwa umoja wao yaani wabunge wote wasimame waainishe posho haramu na wazikatae kama ni kufukuzwa Bungeni wote wafukuzwe. Hakika nakuambia hakuna wa kuwafukuza na utaratibu ama kanuni zitabadilishwa tena na hili bunge la kumi. Lakini kwa mtindo huu wa mmoja mmoja kukataa posho ambayo anaona ni kero kwake hatufiki kokote. Mbowe amekataa gari, posho zingine anachukua. Zitto anakataa posho za vikao ila zingine ambazo hazina mashiko anachukua. Mbowe ni KUB ana miposho mingine Lukuki, Zitto amekaa bungeni miaka mitano amezila posho za kutosha na ni mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za mashirika ya Umma huko pia kuna responsibility allowance. Je Mr. II, Joseph Selasini, Regia Mtema, nk amabo ni wapya na hawana uenyeviti watachagua kukataa posho gani? ndio maana nasema tusiishi kwa utashi tuweke kanuni ama taratibu kwenye maandishi.
 
Kwanza kabisa nakugongea thanks kwenye kitufe na kukupa kwa maandishi! Tukiwa na mijadala kama hii bila matusi tutafika mbali. Nakubaliana na wewe kabisa kwamba wapinzani ni wachache na sheria haziwezi kupita bila CCM kukubaliana na muswada wowote kwa kuwa ni wengi. Umesema pia kwamba Dr. Slaaa alizomewa ni kweli lakini kama unafuatilia utaona kwamba Zitto hakuzomewa sijui kama Mbowe alizomewa. Ninachotaka kusema ni kwamba hii hoja imewaingia hata CCM wenyewe manake wanaona wasipoiangalia inaweza ikaawangusha sana 2015 kwa kuwa hii ni sumu kubwa sana kwa wapiga kura; waalimu, vijana, wakulima, nk. Hao wapiga kura wanaamini kuwa wananyonywa na CCM ndio kinara wa kuwanyonya kupitia kwenye miposho. Kwa hiyo siamini kama kuna Mbunge wa CCM ambaye atasimama na kusema posho ya kikao ni haki, sijamsikia zaidi zaidi walikuwa wakikwepa na kusema posho za Polisi sijui na wanajeshi wastaafu. Kwa hiyo basi serikali na CCM wameisha legea kinatotakiwa ni CHADEMA kwa umoja wao yaani wabunge wote wasimame waainishe posho haramu na wazikatae kama ni kufukuzwa Bungeni wote wafukuzwe. Hakika nakuambia hakuna wa kuwafukuza na utaratibu ama kanuni zitabadilishwa tena na hili bunge la kumi. Lakini kwa mtindo huu wa mmoja mmoja kukataa posho ambayo anaona ni kero kwake hatufiki kokote. Mbowe amekataa gari, posho zingine anachukua. Zitto anakataa posho za vikao ila zingine ambazo hazina mashiko anachukua. Mbowe ni KUB ana miposho mingine Lukuki, Zitto amekaa bungeni miaka mitano amezila posho za kutosha na ni mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za mashirika ya Umma huko pia kuna responsibility allowance. Je Mr. II, Joseph Selasini, Regia Mtema, nk amabo ni wapya na hawana uenyeviti watachagua kukataa posho gani? ndio maana nasema tusiishi kwa utashi tuweke kanuni ama taratibu kwenye maandishi.
Kweli kabisa mkuu, namekupata vizuri kabisa. Imefika wakati viongozi wawe serious kwenye mambo muhimu kwa taifa letu na watu wake.
 
Kwanza kabisa nakugongea thanks kwenye kitufe na kukupa kwa maandishi! Tukiwa na mijadala kama hii bila matusi tutafika mbali.

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba wapinzani ni wachache na sheria haziwezi kupita bila CCM kukubaliana na muswada wowote kwa kuwa ni wengi. Umesema pia kwamba Dr. Slaaa alizomewa ni kweli lakini kama unafuatilia utaona kwamba Zitto hakuzomewa sijui kama Mbowe alizomewa. Ninachotaka kusema ni kwamba hii hoja imewaingia hata CCM wenyewe manake wanaona wasipoiangalia inaweza ikaawangusha sana 2015 kwa kuwa hii ni sumu kubwa sana kwa wapiga kura; waalimu, vijana, wakulima, nk. Hao wapiga kura wanaamini kuwa wananyonywa na CCM ndio kinara wa kuwanyonya kupitia kwenye miposho. Kwa hiyo siamini kama kuna Mbunge wa CCM ambaye atasimama na kusema posho ya kikao ni haki, sijamsikia zaidi zaidi walikuwa wakikwepa na kusema posho za Polisi sijui na wanajeshi wastaafu. Kwa hiyo basi serikali na CCM wameisha legea kinatotakiwa ni CHADEMA kwa umoja wao yaani wabunge wote wasimame waainishe posho haramu na wazikatae kama ni kufukuzwa Bungeni wote wafukuzwe. Hakika nakuambia hakuna wa kuwafukuza na utaratibu ama kanuni zitabadilishwa tena na hili bunge la kumi. Lakini kwa mtindo huu wa mmoja mmoja kukataa posho ambayo anaona ni kero kwake hatufiki kokote. Mbowe amekataa gari, posho zingine anachukua. Zitto anakataa posho za vikao ila zingine ambazo hazina mashiko anachukua. Mbowe ni KUB ana miposho mingine Lukuki, Zitto amekaa bungeni miaka mitano amezila posho za kutosha na ni mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za mashirika ya Umma huko pia kuna responsibility allowance. Je Mr. II, Joseph Selasini, Regia Mtema, nk amabo ni wapya na hawana uenyeviti watachagua kukataa posho gani? ndio maana nasema tusiishi kwa utashi tuweke kanuni ama taratibu kwenye maandishi.

Mkuu upo sawa, seriousness ni muhimu sana. kwanza ukumbuke walilamba ile hela ya mkopo wa magari karibu milion 90 kila mmoja na wote walikuwa kimya, na kama ulivyosema hao akina Zitto na Mbowe wana maposho kibao kutokana na nyadhifa zao na pia kuwepo bungeni kwa muda mrefu ndiyo maana hatuwasikii wengine wakisema chochote (akina Lema Mr II nk). labda tutajua huko mbeleni - time will tell.
lakini suala la posho ni aibu kwa nchi yetu masikini, watu wachache wananufaika kupitia migongo ya wengine. hii imeota mizizi hata kwenye idara za mawizara na mashirika ya umma kuna watu wachache ndiyo wanatafuna hizo posho
 
Back
Top Bottom