Kizitto Noya, DodomaKIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema licha ya kurejesha kwa hiari gari alilopewa na serikali ataendelea kuchukua posho za ubunge nyinginezo anazopewa kutokana na nafasi hiyo ya uongozi.Mbowe alisema hayo jana wakati alipotakiwa kujibu hoja zilizotolewa kwa nyakati tofauti na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ofisi ya Bunge zikimtaka aeleze kama ameamua kurejesha gari, basi aache pia kuchukua posho mbalimbali anazozipata kama mbunge na nafasi yake ya uongozi wa kambi ya upinzani.Katika mahojiano na gazeti hili, Mbowe alingaka na kusema kuwa hayuko tayari kuacha posho anazopewa kwa vile zipo kisheria na ni muhimu katika kufanikisha majukumu yake."Naweza kusema kuwa huu ni upuuzi! Alingaka Mbowe alipoulizwa kama yuko tayari kufuata ushauri wa CCM na ofisi ya bunge.Lakini, akaongeza: Kuna mambo mengi ya msingi tunaendeleaa kuyafanya. Unaposema niache na huduma zingine, ofisi ile inaendeshwaje? "Mambo hayo (kuacha gari) tunayafanya kwa sababu tunaangalia pia ni kwa namna gani hayaathiri shughuli za kiofisi. Ukisema nisichukue Sh2 milioni kwa mfano, unataka ofisi hii iendeshweje?" Alieleza kuwa ataendelea kupata huduma hizo kwa kuwa ni haki yake, hivyo kuzikubali au kuzikataa ni uamuzi wake na hashurutishwi na mtu.[/QUOTES] Wewe ni MWONGO. Tena MWONGO MKUBWA Habari iliyoandikwa ktk gazeti la Mwananchi haiko ki-ivyo. Ni Mwongo umetia maneno yako mengi na sehemu nyingine umebadilisha sentensi ikiwa ni zaidi ya kuziondoa sentensi nyingine.Habari iliiyopo ktk gazeti la Mwananchi, toleo na 04014 la 23 Juni 2011 uk 4, iliyoandikwa na Kizitto Noya, Dodoma na Raymond Kaminyoge,Dar yenye kichwa " SHANGINGI LA MBOWE LATIKISA CCM, BUNGE haijawa kama hii unayoileta. Umechakachua sana