Kwanza kabisa nakugongea thanks kwenye kitufe na kukupa kwa maandishi! Tukiwa na mijadala kama hii bila matusi tutafika mbali.
Nakubaliana na wewe kabisa kwamba wapinzani ni wachache na sheria haziwezi kupita bila CCM kukubaliana na muswada wowote kwa kuwa ni wengi. Umesema pia kwamba Dr. Slaaa alizomewa ni kweli lakini kama unafuatilia utaona kwamba Zitto hakuzomewa sijui kama Mbowe alizomewa. Ninachotaka kusema ni kwamba hii hoja imewaingia hata CCM wenyewe manake wanaona wasipoiangalia inaweza ikaawangusha sana 2015 kwa kuwa hii ni sumu kubwa sana kwa wapiga kura; waalimu, vijana, wakulima, nk. Hao wapiga kura wanaamini kuwa wananyonywa na CCM ndio kinara wa kuwanyonya kupitia kwenye miposho. Kwa hiyo siamini kama kuna Mbunge wa CCM ambaye atasimama na kusema posho ya kikao ni haki, sijamsikia zaidi zaidi walikuwa wakikwepa na kusema posho za Polisi sijui na wanajeshi wastaafu. Kwa hiyo basi serikali na CCM wameisha legea kinatotakiwa ni CHADEMA kwa umoja wao yaani wabunge wote wasimame waainishe posho haramu na wazikatae kama ni kufukuzwa Bungeni wote wafukuzwe. Hakika nakuambia hakuna wa kuwafukuza na utaratibu ama kanuni zitabadilishwa tena na hili bunge la kumi. Lakini kwa mtindo huu wa mmoja mmoja kukataa posho ambayo anaona ni kero kwake hatufiki kokote. Mbowe amekataa gari, posho zingine anachukua. Zitto anakataa posho za vikao ila zingine ambazo hazina mashiko anachukua. Mbowe ni KUB ana miposho mingine Lukuki, Zitto amekaa bungeni miaka mitano amezila posho za kutosha na ni mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za mashirika ya Umma huko pia kuna responsibility allowance. Je Mr. II, Joseph Selasini, Regia Mtema, nk amabo ni wapya na hawana uenyeviti watachagua kukataa posho gani? ndio maana nasema tusiishi kwa utashi tuweke kanuni ama taratibu kwenye maandishi.