Mbowe ashikiliwa Central Police

Mahakama iko kwa ajiri ya nani?Wapinzani na walalahoi?Mifisadi iliojaa CCM pamoja na JK mwenyewe imefuja na inaendelea kufuja rasilimali zetu inaendelea kudunda na kutanua na hata huku ndani ya chama inafahamiana badala ya kuchuliwa hatua za kisheria inaendelea kutuimbia nyimbo za kujivua magamba huu ni wakati muafaka kwa nguvu ya umma kuchukua mkondo wake.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 

Ndio sheria za nchi inayotawaliwa na mafisadi, sheria zinaruhusu mtu akamatwe Jumamosi lakini sheria hiyo hiyo hairuhusu mtu huyo kuwekewa dhamana mpaka baada mwisho wa wiki kwisha.
 
Pipozzzzzzzzzzz pawaaaaaaaar
Tunasubiri tamko la CDM tu,ttulio tayari kwa ukombozi tuzame street kwa ukombozi.kwani
"ni bora ufe ukipigania ukombozi,kwani hata usipojitokeza utakufa kinyonge kwa malaria,kipindupindu au ajali za barabarani"
kukubali kuishi chini ya magamba ni sawa kabisa na ku opt kifo,kwani watanzania wengi wameshakufa wakiwa hai kutokana na ufisadi na udhalimu wa magamba na taasisi zake kandamizi.
 
naona viashilia vya ccm kuondoka madarakani kwa nguvu yetu/nguvu ya umma,mh.mbowe kasema yuko tiyari kufa amesimama kuliko kuishi amepiga magoti,mimi pia nipo tiyari kufanae tukiwa tumesimama!!! Imetosha!! Sasa basi wajinga wakubwa hawa watawala,wanafiki majizi.mashetani!!! Hivi Mwalimu nyerere aliyajua haya shetani?
 


Chombeza hiyo!!! Funga safari ukashiriki.
 

Huoni kama hii ni kununua umaarufu kwa Mbowe? Mbona wenziwe walienda baada ya kutishiwa kukamatwa? Ukweli wenyewe ni kuwa huko aliko sio keko lakini asingefanya mchezo huo. Mimi naona ni kutumia vitendo nyie wenye nguvu ya wananchi badala ya kuendeleza malumbano>
 
Kwa nini wasimkamate Ijumaa siku ya kazi? wamesubiri hadi Jumamosi wakijua fika kwamba kupata dhamana itakuwa nguvu- huu ndio ubabe= state intimidation!


Na kwanini hasa ashindane na mahakama kwani anaogopa nini wakati anajuwa hana makosa? Huku kuidharau mahakama hakuna maana na badala yake unajikuta kwenye matatizo bure. CHADEMA ina mahelkopta kwanini asiende alikoitwa kwa kutumia helkopta?
 
Ndio sheria za nchi inayotawaliwa na mafisadi, sheria zinaruhusu mtu akamatwe Jumamosi lakini sheria hiyo hiyo hairuhusu mtu huyo kuwekewa dhamana mpaka baada mwisho wa wiki kwisha.

Mimi najiuliza, Dhamana hiyo apewe na nani iwapo dhamana inatolewa mahakamani au polisi. Polisi wameshaamriwa wamkamate kwa kukiuka dhamana na mahakama haifanyi kazi siku hiyo, sijui lawama zinakujaje? Hapa kuna mambo mawili, moja ni sheria zetu tulizoziweka na la pili ni uamuzi wake mwenyewe Mbowe kuidharau mahakama kwa sababu anazozijuwa mwenyewe. Nafikiri ingekuwa busara tukangojea utetezi wake mahakamani kwani ni yeye anaeelewa kwanini alifanya alivyofanya.
 
mwandishi mwangulumbi alisha andika kuwa hawa jamaa ni mbwa wa watawala wanabweka pasipo na haja,wanabweka au kung'ata wakiambiwa kufanya hivo na wanaowafuga mbwa hao GP AND MK.sasa wamezunguka wanabweka,wanambwekea mh.mbowe,mapinduzi ya uhuru wa kweli yataanza naMBWA hao,then kwa wafuga mbwa! Kibaya zaid mengine majibwa koko!!
 
 
Nimekatishwa tamaa na uamuzi wa Mbowe kujipeleka polisi mwenyewe. Najiuliza ni kwa nini amekiuka matamshi ya mdomo wake na maandiko ya chama chake yaliyotolewa na Lisu?
Hivi jamani naomba mnijuze ukweli kama alijipeleka mwenyewe au vipi..... kama ndivyo basi ana matatizo ya kutujengea imani upya juu yake. Ikiwa polisi walimkamata kwa nguvu basi anapaswa kusaidiwa na nguvu ya Umma ili kuionesha serikali kuwa mafisadi hawapaswi kuwa huru barabarani wakati mbowe akiwa Rumande.
 

Wamepigia hesabu sawasawa kwani masaa 48 atakuwa mahakamani kuomba radhi ili aachiwe. Kama kweli hawa BAVICHWA hawajuwi hili danganya toto ya Mbowe wangetowa masaa7 tu atolewe na kama sivyo .......
 

Mbona amri ya kukamatwa imetolewa na Mahakama baada ya Mbowe kuamuwa kuvunja sheria!! Polisi na CCM wanahusikaje? Wahusika ni Mbowe mwenyewe na Mahakama wanaoonyeshana ubabe!
 
Heche usilete balaa nyingine hapa... Tatizo si la Mbowe na polisi. Polisi hawajamkamata ili wamuhoji au kuna tatizo na mbowe ila anakamatwa kama kutimiza matakwa ya Mahakama. Heche usisahau kuwa kuna nguzo tatu - Mahakama, Bunge na Dola. Mahakama imeamuru dola kutekeleza wajibu fulani na dola inatekeleza ila kama kuna udhuru dola inautoa kama ilivyotokea kwa mgombea binafsi. Serikali ilikata rufaa. Dola haijaona kosa kumkamata mbowe hivyo wametekeleza wajibu wao. Anne Makinda pia anao wajibu wa kumtetea Mbowe lakini labda ameshatoa kibari cha polisi kumsomba .....who knows?

Tusubiri uamuzi wa Mahakama bila kuweka mashinikizo. Hakimu atamwacha huru tu kwani hiko wazi kuwa waliomba ruksa na mdhamini wake alikuwa mgonjwa hakuja so no problem to Mbowe.........
 
Mbona amri ya kukamatwa imetolewa na Mahakama baada ya Mbowe kuamuwa kuvunja sheria!! Polisi na CCM wanahusikaje? Wahusika ni Mbowe mwenyewe na Mahakama wanaoonyeshana ubabe!

Kwa nini wamkamate weekend???inahusuika vipi hii taratibu??kwa nini wasingesubiria mpaka siku za kazi???fikiria kwanza......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…