Tuache kukurupukia mada jamani!
kardinali amesema kauli aliyoitoa Bishop Niwemugizi sio msimamo wa kanisa katoliki.
Hii inamaanisha kwamba haijawahi kutokea viongozi wote na waumini wa kanisa katoliki wakakaa pamoja na kusema kwamba KIPAUMBELE CHA KANISA KATOLIKI NAMBA MOJA NI KATIBA MPYA
Kwa muktadha huo, alichokisema Niwemugizi ni maoni yake binafsi ila kanisa katoliki halijamtuma kulisemea kwa niaba
unapoanza kutoa kashfa na lugha za kejeli kwa kardinali ni makosa, hebu jaribu kufikiria kiundani kwamba kardinali alivyosema alikuwa anamaana gani? sio kusoma juu juu tu na kuanza kufanya analysis zisizokuwa na tija na za kupotosha ukweli.
Narudia tena, kauli ya Pengo inamaanisha kwamba, Kanisa Katoliki halijamuagiza Niwemugizi kulisemea kwa niaba, ila Niwemugizi alikuwa anatoa maoni yake binafsi kwani ni haki yake kikatiba kama mwanachi halali ww Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
PENGO YUKO SAHIHI NA HAKUNA ALICHOKOSEA!