Mbowe ashangazwa na kauli ya Kardinali Pengo

Pengo umri umeenda baba maaskofu wengine wakifikia umri wako hua wanastaafu na kuwaachia wenye nguvu ya kufanya kazi.
 
Uwa nacheka sana Watanzania walivyokuwa wanafiki wakati wa JK povu lilikuwa limawatoka humu.
 
Kama ni uhuru wa maoni kwanini ukienda kinyume na magufuli unamiminiwa risas kama lissu au kuitwa mchochezi hamuoni huko ni kuingilia uhuru wa mtu binafsi wa kutoa maoni yake kwa mtazamo wake??
Mjifunze kuheshimu maoni na mitazamo ya watu wengine.
Kama una ushahidi wa ulichoandika peleka Central Police.
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kauli ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuhusu mchakato wa Katiba imewasikitisha.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema kiongozi huyo wa dini anapaswa kulinda heshima aliyonayo ndani na nje ya kanisa.

Akizungumza na Mwananchi, Mbowe amesema, “Askofu Pengo ni kiongozi wa kanisa, anaheshimika na wananchi ambao si wale anaowaongoza lakini kwa kauli yake kuhusu Katiba, imetushangaza na imenisikitisha.”

Mbowe amesema, “Suala la elimu, chakula na maisha yetu yanalindwa na Katiba, ndiyo msingi wa mifumo ya rasilimali za Taifa. Anaposema haoni umuhimu wa Katiba anatufikirisha, anataka kusema mchakato wa Katiba uliogharimu mabilioni ya fedha leo hauna maana?”

Amesema umefika wakati mchakato wa Katiba uliokwama ukaendelezwa na hasa kuanzia katika rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti, Jaji mstaafu Joseph Warioba.

“Katiba ni maridhiano, tunahitaji kupata maridhiano ya pande zote, nirudie tu kwamba alichokisema Askofu Pengo kinasikitisha,” amesema Mbowe.

Kardinali Pengo Jumamosi iliyopita alinukuliwa akisema kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi kuwa Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni yake binafsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Alisema hilo alipotoa ufafanuzi kuhusu sitofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo si msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu sisi tuna utaratibu wetu wa kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kipaumbele cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza yeye binafsi ni miongoni mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.

Chanzo: Mwananchi
Mbowee ni mpuuzi tu kama wapuuzi wengine..unahubiri democrasia huku ukiona watu wengine wanatoa maoni yao povu jingi ..that is stupidit...sisi tunataka kuona watu wakizungumza vile waonavyo then sisi tena tunazuia na kuwashambulia yeyote atakaeenda kinyume na mawazo ya huyu Dictecta wa chadema....Binafsi sijaona kosa alilonalo Askofu Pengo...ivi tujiulize hiyom katiba mimi au wewe itakusaidia nn wakati sina pesa ya kuendesha maisha yangu ya kila siku...badala ya kuwasaidia watu kupata kazi na kutengeneza mazingira ya watu kupata kazi unamuattack Pengo... Sasa naona amewaambukiza adi hao three IDIOT wako
Mwambieni Mbowe aache watu watoe maoni yao asijikute yeye pekee ndio mwenye sauti ya kuzungumza na kuwa yupo sahihi kwa kila jambo
 
embu toa vielelezo vinavyoonesha kuwa LISSU alimiminiwa Risasi kwa sababu ya kupayuka kwake..??tuache unafki tutaendelea sana kuliko kuja hapa jamii forum kucomment kisa unabando za chuo
 
Pengo anajichanganya mwenyewe ukichambua kauli zake. Anasema kwamba huo siyo msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa. Hii ni kauli ya kwanza na inaweza kuwa na ukweli. Lakini kauli ya pili anasema hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu wao wana utaratibu wa kuwasiliana na serikali.

Hapa ndipo alipokoroga. Hivi utaendaje kuwasiliana na serikali wakati huna msimamo unaokupeleka ikulu?! Hivyo, kama Niwe Mugizi angekweda Ikulu kimya kimya je Pengo angekubali msimamo ule kwa sababu kafuata njia anayoitaka Pengo?
wewe ndio unajichanganya pengo he speek what he think his right na hajakulazimisha wewe ufikili kama yeye
 
embu toa vielelezo vinavyoonesha kuwa LISSU alimiminiwa Risasi kwa sababu ya kupayuka kwake..??tuache unafki tutaendelea sana kuliko kuja hapa jamii forum kucomment kisa unabando za chuo
Una hakika umeninukuu mtu sahihi? Ni wapi nilipoandika Lisu alimininiwa risasi kwa sababu ya kupayuka?
Kuwa makini aisee!
Pathetic!
 
Kwa nini hampendi kuheshimu fikra na maoni ya wengine? Hayo ni maoni yake binafsi kama Raia wa Tanzania na ana uhuru na Haki kikatiba.
Shame!

Unapotoa maoni unatakiwa ujue impact ya maoni yako kwenye jamii kulingana na nafasi yako na influence yako kwenye jamii, hata kama maoni ni yake binafsi ila mchakato wa katiba ni muhimu kwa Taifa na kwa ulewa wa Pengo nahakika analijua hilo.....
Pengo katumia haki yake na nadhani anahaki pia ya kuonekana MJINGA pale inapobidi.........
 
Nyani Ngabu

Hawa jamaa wananishangaza sana!

Wao hawataki wengine watoe maoni yao ambayo yanakinzana na mitazamo yao.

Mbaya zaidi wanaanza kumshambulia mtoa maoni kwa kutumia matusi na dharau.

Suala la katiba lilishabuma na CCM wanafahamu lilileta mgawanyiko mkubwa na upotevu wa pesa. Hawawezi tena kuingia kwenye tatizo hilo kwa kipindi hiki.

Tatizo kuu ni idadi ya serikali.

Huyu ngosha Magu hawezi kuleta tena huo mchakato katika kipindi hiki cha utawala wake wa miaka 5 labda atafanya hivyo katika awamu ya pili ya utawala wake.
Nyani ngabu ndio nan? Mpk unamuita! Au anakupiga p.u.m.b.u?
 
Unapotoa maoni unatakiwa ujue impact ya maoni yako kwenye jamii kulingana na nafasi yako na influence yako kwenye jamii, hata kama maoni ni yake binafsi ila mchakato wa katiba ni muhimu kwa Taifa na kwa ulewa wa Pengo nahakika analijua hilo.....
Pengo katumia haki yake na nadhani anahaki pia ya kuonekana MJINGA pale inapobidi.........
Haya ni moja ya matatizo ya kuzaliwa nje ya ndoa. Unatumia mhemko na mtetemo kujadili mada badala ya kutumia hoja.
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kauli ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuhusu mchakato wa Katiba imewasikitisha.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema kiongozi huyo wa dini anapaswa kulinda heshima aliyonayo ndani na nje ya kanisa.

Akizungumza na Mwananchi, Mbowe amesema, “Askofu Pengo ni kiongozi wa kanisa, anaheshimika na wananchi ambao si wale anaowaongoza lakini kwa kauli yake kuhusu Katiba, imetushangaza na imenisikitisha.”

Mbowe amesema, “Suala la elimu, chakula na maisha yetu yanalindwa na Katiba, ndiyo msingi wa mifumo ya rasilimali za Taifa. Anaposema haoni umuhimu wa Katiba anatufikirisha, anataka kusema mchakato wa Katiba uliogharimu mabilioni ya fedha leo hauna maana?”

Amesema umefika wakati mchakato wa Katiba uliokwama ukaendelezwa na hasa kuanzia katika rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti, Jaji mstaafu Joseph Warioba.

“Katiba ni maridhiano, tunahitaji kupata maridhiano ya pande zote, nirudie tu kwamba alichokisema Askofu Pengo kinasikitisha,” amesema Mbowe.

Kardinali Pengo Jumamosi iliyopita alinukuliwa akisema kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi kuwa Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni yake binafsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Alisema hilo alipotoa ufafanuzi kuhusu sitofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo si msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu sisi tuna utaratibu wetu wa kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kipaumbele cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza yeye binafsi ni miongoni mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.

Chanzo: Mwananchi

HAJAKOSEA HATA KIDOGO. NI KWELI KWA SABABU WAUMINI WA KIKATOLIKI WANA MISIMAMO TOFAUTI, HUO HAUWEZI KUWA MSIMAMO WA KANISA LA KIKATOLIKI, HUMO KANISANI KUNA CCM, CHADEMA, ACT NA WENGINEO, MSIMAMO WA KANISA KWENYE MAMBO HAYO HAUWEZI KUWA HUO.
 
Ila kauli ya rowasa ya kufanya kampeni kanisani na kusema sasa ni zamu ya mrutheli ahikumshanga mbowe kwakuwa ilikuwa kauli ya sahihi?
 
PENGO INASADIFU JINA LAKE

TUNAMLISHA KWA SADAKA ZETU, ANAVAA BURE, ANASAFIRI BURE KILA K2 BURE, LAKINI BADO ANAKUWA 'PENGO'
 
Umri na maradhi pengine vinachangia.......Cardinal angesema yote lakini sio kusema haoni umuhimu Wa katiba, kwakweli ameshangaza.

Kuna sehemu yeyote aliyosema haoni umuhimu Wa katiba? So vyema kumshuhudia nduguyo uongo.
 
Mbowee ni mpuuzi tu kama wapuuzi wengine..unahubiri democrasia huku ukiona watu wengine wanatoa maoni yao povu jingi ..that is stupidit...sisi tunataka kuona watu wakizungumza vile waonavyo then sisi tena tunazuia na kuwashambulia yeyote atakaeenda kinyume na mawazo ya huyu Dictecta wa chadema....Binafsi sijaona kosa alilonalo Askofu Pengo...ivi tujiulize hiyom katiba mimi au wewe itakusaidia nn wakati sina pesa ya kuendesha maisha yangu ya kila siku...badala ya kuwasaidia watu kupata kazi na kutengeneza mazingira ya watu kupata kazi unamuattack Pengo... Sasa naona amewaambukiza adi hao three IDIOT wako
Mwambieni Mbowe aache watu watoe maoni yao asijikute yeye pekee ndio mwenye sauti ya kuzungumza na kuwa yupo sahihi kwa kila jambo
Mbowe yupo sahihi,Pengo anatoa matamko binafsi kuyafanya ya kanisa
 
Back
Top Bottom