Mbowe ashangazwa na kauli ya Kardinali Pengo

Tatizo la Mbowe ni elimu ndogo. Eti Katiba ni maridhiano kati ya pande zote!! Yaani katiba ni maridhiano kati ya chama tawala cha wakati huu na vyama vya upinzani vya wakati huu. Kwa mantiki hiyo ndiyo maana mchakato wa kupata katiba mpya ulikwama baada ya kutumia zaidi trillion moja ya pesa (kuamzia maandalizi, tume za Waryoba hadi bunge la katiba). Ulikwama kwa sababu maridhiano kati ya CCM na vyama vya upinzani vilivyojibatiza jina la UKAWA na kuwabatiza CCM jina la INTARAHAMWE, hayakuweza kufikiwa.

Na kama mantiki ni hiyo, kamwe maridhiano hayo hayatawahi kutokea kati ya CCM na hivi vyama vya upinzani na hasa Chadema. Na hasa kwenye kipindi hiki cha awamu ya tano ambao tumeshuhudia mnyukano kati ya pande hizi kuwa mkali zaidi ukilinganisha na uliokuwepo wakati wa awamu ya nne. Sasa kama hayo maridhiano hayakuwezekana enzi hiyo ya juice ndiyo utegemee yatapatikana enzi hii ya Hapa Kazi Tu?

Katiba ya nchi si maridhiano baina ya vyama vya siasa vilivyopo. Katiba ya nchi ni mkataba kati ya wananchi wote kwa pamoja na watawala wa nchi waliopo na watakaokuwapo, wa namna nchi yao wanavyotaka iongozwe/ itawaliwe. Katiba si mkataba kati ya vyama vya siasa. Katiba si mali ya wanasiasa bali ni mali ya wananchi wote, wanachama na wasiokuwa wanachama wa vyama vya siasa, wa dini zote na wasio na dini, wa makabila yote na wasiokuwa na kabila, wa rangi zote na wasiokuwa na rangi.

My take: Si busara kabisa kwa sasa kutaka kutumia matrillion ya pesa kurudia mchakato huo wa katiba mpya ambao kwa asilimia 100% hautafanikiwa. Fedha hizo ni vyema zikaelekezwa kujenga miundombinu ya nchi hususani reli ya umeme, Stigler's gauge hydroelectric plant.

Katiba iliyopo inatosha. Kinachotakiwa sana sana ni kuifanyia marekebisho madogo hususani kuweka vipengele vinavyoruhusu wagombea binafsi kwenye nafasi za ubunge na urais, kupinga mahakamani matokeo ya kura za urais, kudhibiti harakati na maadili ya vyama vya siasa na kadhalika.
 
7
Umri na maradhi pengine vinachangia.......Cardinal angesema yote lakini sio kusema haoni umuhimu Wa katiba, kwakweli ameshangaza.
Kwani pengo ni nani hadi awe anaona umuhimu wa kila hitaji la kila mtanzania. Kama haoni umuhimu wa katiba mpya ni sawa na ambavyo mie pia sioni umuhimu wa kuwa na bunge linalopatikana kwa njia ya kupigiwa kura na kila mtu. Kutoona umuhimu wa chochote ni haki kama hayo mapenzi hayavunji sheria.
 
Tatizo la Mbowe ni elimu ndogo. Eti Katiba ni maridhiano kati ya pande zote!! Yaani katiba ni maridhiano kati ya chama tawala cha wakati huu na vyama vya upinzani vya wakati huu. Kwa mantiki hiyo ndiyo maana mchakato wa kupata katiba mpya ulikwama baada ya kutumia zaidi trillion moja ya pesa (kuamzia maandalizi, tume za Waryoba hadi bunge la katiba). Ulikwama kwa sababu maridhiano kati ya CCM na vyama vya upinzani vilivyojibatiza jina la UKAWA na kuwabatiza CCM jina la INTARAHAMWE, hayakuweza kufikiwa.

Na kama mantiki ni hiyo, kamwe maridhiano hayo hayatawahi kutokea kati ya CCM na hivi vyama vya upinzani na hasa Chadema. Na hasa kwenye kipindi hiki cha awamu ya tano ambao tumeshuhudia mnyukano kati ya pande hizi kuwa mkali zaidi ukilinganisha na uliokuwepo wakati wa awamu ya nne. Sasa kama hayo maridhiano hayakuwezekana enzi hiyo ya juice ndiyo utegemee yatapatikana enzi hii ya Hapa Kazi Tu?

Katiba ya nchi si maridhiano baina ya vyama vya siasa vilivyopo. Katiba ya nchi ni mkataba kati ya wananchi wote kwa pamoja na watawala wa nchi waliopo na watakaokuwapo, wa namna nchi yao wanavyotaka iongozwe/ itawaliwe. Katiba si mkataba kati ya vyama vya siasa. Katiba si mali ya wanasiasa bali ni mali ya wananchi wote, wanachama na wasiokuwa wanachama wa vyama vya siasa, wa dini zote na wasio na dini, wa makabila yote na wasiokuwa na kabila, wa rangi zote na wasiokuwa na rangi.

My take: Si busara kabisa kwa sasa kutaka kutumia matrillion ya pesa kurudia mchakato huo wa katiba mpya ambao kwa asilimia 100% hautafanikiwa. Fedha hizo ni vyema zikaelekezwa kujenga miundombinu ya nchi hususani reli ya umeme, Stigler's gauge hydroelectric plant.

Katiba iliyopo inatosha. Kinachotakiwa sana sana ni kuifanyia marekebisho madogo hususani kuweka vipengele vinavyoruhusu wagombea binafsi kwenye nafasi za ubunge na urais, kupinga mahakamani matokeo ya kura za urais, kudhibiti harakati na maadili ya vyama vya siasa na kadhalika.
Another stooge
 
Katiba sio ya vyama, Upinzani au chama tawala...
Katiba ni ya wananchi wote, wenye vyama na wasio na vyama
 
Kama alivyosema, hata umuhimu wa BIBLIA hawauonagi, kwao cha muhimu ni MISALE YA WAUMINU.
 
Huyu Mbowe yeye mbona huwa anatoa kauli zinazoshangaza na kusikitisha mara nyingi tu!
Ana uhuru na haki kutoa maoni yake kikatiba bila ya kuvunja sheria za nchi.
Mnataka watu watoe maneno yanayowapendeza na kuwasifia ili iweje? Vumilieni fikra, maoni na mitazamo ya wengine kama wao wanavyowavumilia.
Mbowe naye katoa maoni yake, ambayo ndiyo hayo. sasa shida iko wapi kwani?
 
Nyani Ngabu

Hawa jamaa wananishangaza sana!

Wao hawataki wengine watoe maoni yao ambayo yanakinzana na mitazamo yao.

Mbaya zaidi wanaanza kumshambulia mtoa maoni kwa kutumia matusi na dharau.

Suala la katiba lilishabuma na CCM wanafahamu lilileta mgawanyiko mkubwa na upotevu wa pesa. Hawawezi tena kuingia kwenye tatizo hilo kwa kipindi hiki.

Tatizo kuu ni idadi ya serikali.

Huyu ngosha Magu hawezi kuleta tena huo mchakato katika kipindi hiki cha utawala wake wa miaka 5 labda atafanya hivyo katika awamu ya pili ya utawala wake.
hayo ni maoni ya Mbowe, naye katoa maoni yake binafsi. shida iko wapi?
 
Kardinali Pengo Jumamosi iliyopita alinukuliwa akisema kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi kuwa Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni yake binafsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Kwa maana kwamba Kanisa inaamini Mchakato uliofanywa kabla yalikuwa maigizo siyo?.
Naona Kiranja wa Kulinda Kondoo wa Bwana via RC umri na ugonjwa kunamtia hofu.
 
Tatizo ni kwamba, Kanisa Katoliki, na hasa Mwadhama Kardinali Pengo, amekuwa mkali sana kwa serikali ya Mwinyi na Serikali ya Kikwete. alikuwa mkimya kabisa serikali ya Mkapa na sasa katika serikali ya Magufuli. tofauti na wakati wa Mkapa, sasa hivi anaonesha mapenzi makubwa kwa CCM na serikali yake. na yuko mkali sana pale vyombo vya kanisa vinapotofautiana na serikali hii. mfano kuna waraka uliwahi kutolewa kipindi kile cha uchaguzi, Pengo aliushambulia, japo ulitolewa na kitengo cha Baraza la Maaskofu. lakini kule nyuma enzi ya Jakaya Kikwete, Kanisa lilitoa waraka mzito sana kipindi cha uchaguzi mwaka 2010, na hatukumuona Baba Kardinali kuingilia kati. waraka huo ulitamba sana na kuitikisa nchi. ilikuwa ni kipindi Dr. Wilbrod Slaa aligombea urais wa nchi.

Ni kweli ana haki ya kutoa maoni yake binafsi, lakini anayatoa kwa namna ya kufunika wengine, maana ilitakiwa pia aseme kwamba haya ni maoni yake na siyo msimamo wa kanisa katoliki. Lakini pia anapiga propaganda kwa serikali iliyoko madarakani. ili iweje?
 
KATIBA SI KIPAUMBELE CHA MAGUFULI wakati anajinadi wala hakuwahi kuzungumzia achilia mbali kugusia. Mimi naona wote wanapoteza muda. Hii kitu wangoje raisi mwingine labda atalianzisha
 
Tatizo ni kwamba, Kanisa Katoliki, na hasa Mwadhama Kardinali Pengo, amekuwa mkali sana kwa serikali ya Mwinyi na Serikali ya Kikwete. alikuwa mkimya kabisa serikali ya Mkapa na sasa katika serikali ya Magufuli. tofauti na wakati wa Mkapa, sasa hivi anaonesha mapenzi makubwa kwa CCM na serikali yake. na yuko mkali sana pale vyombo vya kanisa vinapotofautiana na serikali hii. mfano kuna waraka uliwahi kutolewa kipindi kile cha uchaguzi, Pengo aliushambulia, japo ulitolewa na kitengo cha Baraza la Maaskofu. lakini kule nyuma enzi ya Jakaya Kikwete, Kanisa lilitoa waraka mzito sana kipindi cha uchaguzi mwaka 2010, na hatukumuona Baba Kardinali kuingilia kati. waraka huo ulitamba sana na kuitikisa nchi. ilikuwa ni kipindi Dr. Wilbrod Slaa aligombea urais wa nchi.

Ni kweli ana haki ya kutoa maoni yake binafsi, lakini anayatoa kwa namna ya kufunika wengine, maana ilitakiwa pia aseme kwamba haya ni maoni yake na siyo msimamo wa kanisa katoliki. Lakini pia anapiga propaganda kwa serikali iliyoko madarakani. ili iweje?
Labda kama unatatizo naye binafsi kama Polycap ila amesema kwa mtazamo wake yeye,wala hajalisemea kanisa..hivyo naona ni haki yake tu,kama na yule mwenzake alivyosema kwa maoni yake mwenyewe.Kusikitishwa au kufurahishwa ni juu ya msikilizaji mwenyewe pia,hatuna msaada.

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
Kwa nini hampendi kuheshimu fikra na maoni ya wengine? Hayo ni maoni yake binafsi kama Raia wa Tanzania na ana uhuru na Haki kikatiba.
Shame!
Hata hayo anayoongea muheshimiwa pia ni maoni yake kama raia wa tanzania kwa hiyo kama hajkubaliana nae akae kimya tuu, mbona hampendi kupingwa nyie kila kitu mnata tuwakubalie tuu
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kauli ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuhusu mchakato wa Katiba imewasikitisha.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema kiongozi huyo wa dini anapaswa kulinda heshima aliyonayo ndani na nje ya kanisa.

Akizungumza na Mwananchi, Mbowe amesema, “Askofu Pengo ni kiongozi wa kanisa, anaheshimika na wananchi ambao si wale anaowaongoza lakini kwa kauli yake kuhusu Katiba, imetushangaza na imenisikitisha.”

Mbowe amesema, “Suala la elimu, chakula na maisha yetu yanalindwa na Katiba, ndiyo msingi wa mifumo ya rasilimali za Taifa. Anaposema haoni umuhimu wa Katiba anatufikirisha, anataka kusema mchakato wa Katiba uliogharimu mabilioni ya fedha leo hauna maana?”

Amesema umefika wakati mchakato wa Katiba uliokwama ukaendelezwa na hasa kuanzia katika rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti, Jaji mstaafu Joseph Warioba.

“Katiba ni maridhiano, tunahitaji kupata maridhiano ya pande zote, nirudie tu kwamba alichokisema Askofu Pengo kinasikitisha,” amesema Mbowe.

Kardinali Pengo Jumamosi iliyopita alinukuliwa akisema kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi kuwa Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni yake binafsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Alisema hilo alipotoa ufafanuzi kuhusu sitofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo si msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu sisi tuna utaratibu wetu wa kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kipaumbele cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza yeye binafsi ni miongoni mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.

Chanzo: Mwananchi
HII NI NCHI YA DEMOKRASIA KILA MTU ANA HURU WA KUTOA MAONI, MAWAZO YAKE,

Mbona MBOWE alichengi GIA ANGANI, ALIMKARIBISHA LOWASSA CHADEMA ETC.....tujifunze kukubari maoni na mawazo ya watu wengine.
 
Katiba sio ya vyama, Upinzani au chama tawala...
Katiba ni ya wananchi wote, wenye vyama na wasio na vyama
Hicho ndicho nilichosema. Hakuna cha maridhiano na pande ye yote. Na asilimia 75% ya wananchi wako vijijini. Mamlaka ya nchi iko kwa wananchi wenyewe ambao 80% si wanachama wa chama cho chote cha siasa. Hivyo wanasiasa wasitulishe maneno kwamba tunataka katiba mpya. Wananchi wanataka amani na utulivu, wanataka elimu bora ya bure, wanataka matibabu bora ya bure, wW anataka maji safi na salama ya bure, wanataka umeme wa bei nafuu kila sehemu, wanataka usafiri bora wa bei nafuu, wanataka vifaa bora vya ujenzi wa nyumba zao kwa bei nafuu, wanataka nguo nzuri za bei nafuu. Hayo mambo ya serikali tatu, tano au 10 are very irrelevant to the wananchi. Kwanza wao wanajua serikali ni moja tu.
 
Mbowe atambue kuwa Pengo sio KKKT. kanisa lilelaukanda ule wanae shughuli zao kwa kuegemea. CDM. sana. Pengo ni mwanazuoni mzuri na. Ataheshimika. Hivyo
Pengo simheshimu tena sijui ameshiba maharage ya wapi
 
Back
Top Bottom