Mbowe ashangazwa na kauli ya Kardinali Pengo

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
2,194
Reaction score
4,805
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kauli ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuhusu mchakato wa Katiba imewasikitisha.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema kiongozi huyo wa dini anapaswa kulinda heshima aliyonayo ndani na nje ya kanisa.

Akizungumza na Mwananchi, Mbowe amesema, “Askofu Pengo ni kiongozi wa kanisa, anaheshimika na wananchi ambao si wale anaowaongoza lakini kwa kauli yake kuhusu Katiba, imetushangaza na imenisikitisha.”

Mbowe amesema, “Suala la elimu, chakula na maisha yetu yanalindwa na Katiba, ndiyo msingi wa mifumo ya rasilimali za Taifa. Anaposema haoni umuhimu wa Katiba anatufikirisha, anataka kusema mchakato wa Katiba uliogharimu mabilioni ya fedha leo hauna maana?”

Amesema umefika wakati mchakato wa Katiba uliokwama ukaendelezwa na hasa kuanzia katika rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti, Jaji mstaafu Joseph Warioba.

“Katiba ni maridhiano, tunahitaji kupata maridhiano ya pande zote, nirudie tu kwamba alichokisema Askofu Pengo kinasikitisha,” amesema Mbowe.

Kardinali Pengo Jumamosi iliyopita alinukuliwa akisema kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi kuwa Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni yake binafsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Alisema hilo alipotoa ufafanuzi kuhusu sitofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo si msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu sisi tuna utaratibu wetu wa kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kipaumbele cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza yeye binafsi ni miongoni mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu Mbowe yeye mbona huwa anatoa kauli zinazoshangaza na kusikitisha mara nyingi tu!
Ana uhuru na haki kutoa maoni yake kikatiba bila ya kuvunja sheria za nchi.
Mnataka watu watoe maneno yanayowapendeza na kuwasifia ili iweje? Vumilieni fikra, maoni na mitazamo ya wengine kama wao wanavyowavumilia.
 
Nyani Ngabu

Hawa jamaa wananishangaza sana!

Wao hawataki wengine watoe maoni yao ambayo yanakinzana na mitazamo yao.

Mbaya zaidi wanaanza kumshambulia mtoa maoni kwa kutumia matusi na dharau.

Suala la katiba lilishabuma na CCM wanafahamu lilileta mgawanyiko mkubwa na upotevu wa pesa. Hawawezi tena kuingia kwenye tatizo hilo kwa kipindi hiki.

Tatizo kuu ni idadi ya serikali.

Huyu ngosha Magu hawezi kuleta tena huo mchakato katika kipindi hiki cha utawala wake wa miaka 5 labda atafanya hivyo katika awamu ya pili ya utawala wake.
 
Naona wameahirisha kumtumia yule kiongozi mkuu wa KKKT
Kama tulivyo penyezewa habari zao za ndani jana
Wameamua kupambana wenyewe
 
Pengo anajichanganya mwenyewe ukichambua kauli zake. Anasema kwamba huo siyo msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa. Hii ni kauli ya kwanza na inaweza kuwa na ukweli. Lakini kauli ya pili anasema hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu wao wana utaratibu wa kuwasiliana na serikali.

Hapa ndipo alipokoroga. Hivi utaendaje kuwasiliana na serikali wakati huna msimamo unaokupeleka ikulu?! Hivyo, kama Niwe Mugizi angekweda Ikulu kimya kimya je Pengo angekubali msimamo ule kwa sababu kafuata njia anayoitaka Pengo?
 
Mkuu,

Kuwasiliana na Ikulu sio
Lazima waende Ikulu

Hata kutoa tamko kwenye vyombo vya habari linalohusu serikali ni njia mojawapo ya kuwasiliana na serikali.

Tamko la kanisa katoliki hutolewa na Baraza la Maaskofu nchini.

Kumbuka pia kwa sasa Niwemugizi hana cheo chochote kwenye Baraza la Maaskofu.
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kauli ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuhusu mchakato wa Katiba imewasikitisha.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema kiongozi huyo wa dini anapaswa kulinda heshima aliyonayo ndani na nje ya kanisa.

Akizungumza na Mwananchi, Mbowe amesema, “Askofu Pengo ni kiongozi wa kanisa, anaheshimika na wananchi ambao si wale anaowaongoza lakini kwa kauli yake kuhusu Katiba, imetushangaza na imenisikitisha.”

Mbowe amesema, “Suala la elimu, chakula na maisha yetu yanalindwa na Katiba, ndiyo msingi wa mifumo ya rasilimali za Taifa. Anaposema haoni umuhimu wa Katiba anatufikirisha, anataka kusema mchakato wa Katiba uliogharimu mabilioni ya fedha leo hauna maana?”

Amesema umefika wakati mchakato wa Katiba uliokwama ukaendelezwa na hasa kuanzia katika rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti, Jaji mstaafu Joseph Warioba.

“Katiba ni maridhiano, tunahitaji kupata maridhiano ya pande zote, nirudie tu kwamba alichokisema Askofu Pengo kinasikitisha,” amesema Mbowe.

Kardinali Pengo Jumamosi iliyopita alinukuliwa akisema kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi kuwa Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni yake binafsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Alisema hilo alipotoa ufafanuzi kuhusu sitofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo si msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu sisi tuna utaratibu wetu wa kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kipaumbele cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza yeye binafsi ni miongoni mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.

Chanzo: Mwananchi
Huyo Pengo ni wa kutandika viboko amekengeuka
 
Pengo ni kipenzi wa pogba!! unakumbuka Gwajima alivyomrudi?
 
Mbowe atambue kuwa Pengo sio KKKT. kanisa lilelaukanda ule wanae shughuli zao kwa kuegemea. CDM. sana. Pengo ni mwanazuoni mzuri na. Ataheshimika. Hivyo
 
Hawa jamaa wananishangaza sana!

Wao hawataki wengine watoe maoni yao ambayo yanakinzana na mitazamo yao.

Mbaya zaidi wanaanza kumshambulia mtoa maoni kwa kutumia matusi na dharau.

Suala la katiba lilishabuma na CCM wanafahamu lilileta mgawanyiko mkubwa na upotevu wa pesa. Hawawezi tena kuingia kwenye tatizo hilo kwa kipindi hiki.

Tatizo kuu ni idadi ya serikali.

Huyu ngosha Magu hawezi kuleta tena huo mchakato katika kipindi hiki cha utawala wake wa miaka 5 labda atafanya hivyo katika awamu ya pili ya utawala wake.
Yani wanataka kila mtu aseme wanachotaka wao, hata hiyo katiba mpya ikipatikana kwa mwenendo wao hawawezi kuchukua nchi.
 
Back
Top Bottom