Mbowe ashangazwa na kauli ya Kardinali Pengo

Mbowe ashangazwa na kauli ya Kardinali Pengo

nadhani umemlisha maneno hakusema haoni umuhimu wa katiba bali amesema kanisa lina utaratibu wake wa kuishauri serikali na kuzungumzia masuala ya kijamii. lakini hata kama angekua amesema hayo bado askofu pengo ana uhuru wake wa kutoa maoni kulingana na mtazamo wake kama alivyofanya niwemugizi.
Lakini Niwemugizi hakusema Yale ni maoni ya Kabisa Mkuu...........hata hivyo labda kama nilisoma ile story kimwendo kasi, nakumbuka yeye kusema hivyo,tena akasisitiza umuhimu kwake ni afya bora,elimu nk......
 
Mie ni muumini wake lkn kwa kauli yake hii mimempa -(minus). Inatisha na kusikitisha manake bora asome na kujikita kusoma biblia na sio kuongelea mchakato wa KATIBA ambayo badala ya kuitetea hii dira , anatuletea ngonjera.
Inabidi tumjadili na kumsamehe tu, huu upepo Wa awamu hii unatisha mpaka viongozi wetu Wa Kiroho tunaotegemea kutusemea.
 
napata shida sana kuwaelewa chadema na viongozi wake.
Mh. Pengo alikuwa "akitoa ufafanuzi kutokana na hali ya sintofahamu iliyojitokeza miongoni mwa waumini wa dhehebu la katoliki, juu ya kauli ya askofu Niwemugizi"
Ninyi mmeambiwa kwamba kunahali ya sintofahamu ktk kanisa, waumini wanagawanyika kutokana na kauli ya askofu niwemugizi,
halafu anakuja pengo kutoa ufafanuzi kwamba hayo yalikuwa mawazo binafsi kama muumini/mtu mwingine yeyote,
then ninyi mnakuja kumpinga pengo kwa ufafanuzi huo!
maana yake ni kwamba, mnataka hali ya sintofahamu iendelee ktk kanisa na hatimaye ligawanyike kabisa labda kwa sababu ya nguvu kubwa iliyopo ktk kanisa hili, ambayo kwa namna moja ama nyingine mnahisi haipo upande wenu.
Mbowe muache pengo atetee kanisa kama kiongozi wa kanisa, na wewe tetea upinzani kama kiongozi wa upinzani.
 
Mkuu mawazo ya mtu yanaheshimiwa, lakini pia katika kuyaheshimu hatukatazwi kuyajadili........ndio maana naye amejadili mawazo ya mwenzake aliyesema Watanzania wanahitaji Katiba.
Alichofanya Askofu Pengo kama kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania ni kuyaweka mbali mawazo/kauli ya Niwemugizi mbali na Kanisa Katoliki. Kama kawaida ya Wanaharakati wamepindisha ukweli kwa kutumia propaganda za chuki na UHUNI kumshambulia Kiongozi wa Dini. Wewe binafsi huoni tatizo katika hilo boss!?
 
What do you mean?
Jana thread zote zilizomjadili Pengo ziliwekwa ndani ya uzi mmoja , tena uleule uliompa airtime Pengo , hata zile ambazo zilifika page kibao .

Sasa nashangaa huu umebaki vipi !
 
Wewe humfikii mange hata punje
...nafikiri ndio tatizo liko hapo... I smell envy!! Watu walishafikiri wamejijengea sifa fulani hivi huku pamoja na attention... sasa akatokea mwingine, tena 'ke' alafu kutoka kwenye lile zizi moja, smart and very knowlegeable, shrewd but quick witted...
 
Hawa jamaa wananishangaza sana!

Wao hawataki wengine watoe maoni yao ambayo yanakinzana na mitazamo yao.

Mbaya zaidi wanaanza kumshambulia mtoa maoni kwa kutumia matusi na dharau.

Suala la katiba lilishabuma na CCM wanafahamu lilileta mgawanyiko mkubwa na upotevu wa pesa. Hawawezi tena kuingia kwenye tatizo hilo kwa kipindi hiki.

Tatizo kuu ni idadi ya serikali.

Huyu ngosha Magu hawezi kuleta tena huo mchakato katika kipindi hiki cha utawala wake wa miaka 5 labda atafanya hivyo katika awamu ya pili ya utawala wake.

Kuna tofauti ya maoni kati ya:-
a) mtu binafsi,
b) nafasi au cheo
c) taasisi.

Kadinali Pengo amezungumza kwa cheo chake na kwa taasisi yake (b na c), na hiyo ina maana yule mwingine alizungumza kama (a). Huo ni uhuru na haki yake/yao kama Wakatoliki.

Lakini ukitazama upana na unyeti wa suala husika hapo lazima utaona tatizo. Kwa mfano je ni kweli Kadinali na Wakatoliki ndio wenye mustkabali wa nchi hii kuhusu Katiba mpya? Jibu ni hapana. Je Wakatoliki wote wanakubaliana na msimamo wa Kadinali wao? Jibu pia ni hapana. Hivyo yeye kama kiongozi anafanyaje katika muktadha huo?

Sasa suala la Katiba kama alivyosema Mh Mbowe ni maradhiano ya kila kada katika nchi husika; ina maana basi kada ya RC wataungana "automatically" na CCM (ambao msimamo wao umekuwa NO) kupinga uandikwaji wa Katiba mpya, na hilo ndilo la kusikitisha kwamba Kadinali haoni wala hajali maisha, usalama, haki na wajibu wa waumini wake kwa nchi yetu.

Suppose Mashehe au Maaskofu wa madhehebu mengine wakitoa msimamo kwa staili ya Mh Pengo tutakuwa tunaelekea wapi?
 
Umri na maradhi pengine vinachangia.......Cardinal angesema yote lakini sio kusema haoni umuhimu Wa katiba, kwakweli ameshangaza.

HAONI KWELI MKUU MAANA HAPO ALIPO ANAPUMULIA MASHINE SASA KATIBA MPYA YEYE ITAMSAIDIA NINI, CHA MSINGI NI KUWA AKAEPEMBENI VIJANA TUNAHITAJI KATIBA MPYA YEYE ASUBIRI MAZISHI TU
 
Nyani what is wrong with you now days? You no longer discuss issues!
Shida ni Mange mkuu, kaharibia watu kidunia chao walichokuwa wamejingea kichwani mwao... binadamu kiumbe wa ajabu kabisa...yani mtu anaona wivu kwa mambo ambayo amejiwekea tu kichwani kwake, smh!
 
Askofu Niwemugizi nadhani ni miongoni mwa wale maaskofu aliosema Dr Alaa kuwa walinunuliwa na Bwana yule mwenye kichwa cheupe, hivyo anamridhisha bwana yule aone kuwa anampinga mkuu wa kaya
 
Kwa kiongozi mkubwa wa kidini km Pengo kutoa kauli za kukinzana na moja ya viongozi wa dini aliye chini yake, unadhani kunawaweka kwenye wakati gani waumini wao?!, yan mfano ndani ya familia baba na mama kila mmoja awe na maamuzi tofauti kwa jambo ambalo linaigusa familia moja kwa moja unadhani humo ndani patakalika?!

Anasema kanisa lina namna ya kuishauri serikali na kuwa wao huwa wana vikao ambavyo hutoa maamuzi ya pamoja km kanisa sa km aliona mwenzie alikosea walishindwa vip kumuita wakazungumza naye ili waje na kauli ya pamoj km kanisa?! Leo kila mtu kaja na maoni yake km kiongozi wa dini aya sisi waumini ambao tunawaamini hao wapakwa mafuta wa bwana tushike lipi tuache lipi?!
Wewe hujamuelewa Mwadhama pengo, alichomaanisha ni kuwa Niwemugizi ana haki ya kutoa maoni kwa jambo lolote, ila maoni yake si maoni ya kanisa, ili yawe maoni ya kanisa lazima yapitie kwenye vikao, na mwenyekiti wa tec au makamu wake ndo atoe hiyo taarifa, ujue hakuna sintofahamu kati ya hao watu wawili, sasa amuite kwa lipi? Anaruhusa ya kutoa maoni lakini maoni yake si maoni ya kanisa, kama madhehebu yenu hayana taratibu mjifunze
 
Back
Top Bottom