Tatizo la Mbowe ni elimu ndogo. Eti Katiba ni maridhiano kati ya pande zote!! Yaani katiba ni maridhiano kati ya chama tawala cha wakati huu na vyama vya upinzani vya wakati huu. Kwa mantiki hiyo ndiyo maana mchakato wa kupata katiba mpya ulikwama baada ya kutumia zaidi trillion moja ya pesa (kuamzia maandalizi, tume za Waryoba hadi bunge la katiba). Ulikwama kwa sababu maridhiano kati ya CCM na vyama vya upinzani vilivyojibatiza jina la UKAWA na kuwabatiza CCM jina la INTARAHAMWE, hayakuweza kufikiwa.
Na kama mantiki ni hiyo, kamwe maridhiano hayo hayatawahi kutokea kati ya CCM na hivi vyama vya upinzani na hasa Chadema. Na hasa kwenye kipindi hiki cha awamu ya tano ambao tumeshuhudia mnyukano kati ya pande hizi kuwa mkali zaidi ukilinganisha na uliokuwepo wakati wa awamu ya nne. Sasa kama hayo maridhiano hayakuwezekana enzi hiyo ya juice ndiyo utegemee yatapatikana enzi hii ya Hapa Kazi Tu?
Katiba ya nchi si maridhiano baina ya vyama vya siasa vilivyopo. Katiba ya nchi ni mkataba kati ya wananchi wote kwa pamoja na watawala wa nchi waliopo na watakaokuwapo, wa namna nchi yao wanavyotaka iongozwe/ itawaliwe. Katiba si mkataba kati ya vyama vya siasa. Katiba si mali ya wanasiasa bali ni mali ya wananchi wote, wanachama na wasiokuwa wanachama wa vyama vya siasa, wa dini zote na wasio na dini, wa makabila yote na wasiokuwa na kabila, wa rangi zote na wasiokuwa na rangi.
My take: Si busara kabisa kwa sasa kutaka kutumia matrillion ya pesa kurudia mchakato huo wa katiba mpya ambao kwa asilimia 100% hautafanikiwa. Fedha hizo ni vyema zikaelekezwa kujenga miundombinu ya nchi hususani reli ya umeme, Stigler's gauge hydroelectric plant.
Katiba iliyopo inatosha. Kinachotakiwa sana sana ni kuifanyia marekebisho madogo hususani kuweka vipengele vinavyoruhusu wagombea binafsi kwenye nafasi za ubunge na urais, kupinga mahakamani matokeo ya kura za urais, kudhibiti harakati na maadili ya vyama vya siasa na kadhalika.