Mbowe ashangazwa na kauli ya Kardinali Pengo

Mbowe ashangazwa na kauli ya Kardinali Pengo

Haitatokea CHADEMA na Waluteli kupewa nchi ni watu wa ajabu kabisa, yaani mnataka kutuaminisha kinachosemwa na Mbowe na Lowasa ndo sahihi. Shem on you
 
Kanisa lake lenyewe lipo kwa sababu ya katiba. Yaani katiba ya nchi ndiyo iliruhusu hilo kanisa lake liwepo. Bila Katiba kila kitu ni vurugu. Katiba huleta utengamano katika Taifa. Ndio maana kuna wakati Gwajima alihoji huyu ndugu amekula maharage ya wapi?
 
Wanampenda mtu kama Gwajima tu huyo hawawezi kumpenda,ukiwa unawaunga mkono kwa mambo ya UKUTA,BASHITE,KUTEKWA,LISSU,NA JULLIANA SHONZA sijui watakusifu.
 
Photo from bndilahomba.jpg
 
Kama Mbowe alijua mchakato wa katiba mpya umegharimu mabilioni Ni kwa nini walisusia katikati ya mchakato? Au Hilo amelijua Leo?

BTW:Hayo Ni maoni ya Pengo tu kama alivyotoa yule wa Bukoba na hampaswi kumlazimisha kila mtu awe na maoni sawa na yenu.
 
Siyabonga101: Mbona na yeye haheshimu maoni ya Askofu mwenzake Niwemugizi? Huyu mwenzake hakuwahi kusema anasema kwa niaba ya kanisa bali maoni yake kama mtanzania. Ina maana sasa tuseme hicho alichokisema pengo ndio msimamo wa Kanisa? Kwamba kanisa katoliki halioni umuhimu wa katiba bali mradi watu wanasoma na kula basi inatosha. Kwani hiyo haki ya kusoma na kula inalindwa na nini kama si katiba ya nchi?
 
Huyu Mbowe yeye mbona huwa anatoa kauli zinazoshangaza na kusikitisha mara nyingi tu!
Ana uhuru na haki kutoa maoni yake kikatiba bila ya kuvunja sheria za nchi.
Mnataka watu watoe maneno yanayowapendeza na kuwasifia ili iweje? Vumilieni fikra, maoni na mitazamo ya wengine kama wao wanavyowavumilia.
Unasumbuliwa na ujinga. Yaani maoni ya Pengo hutaki yakosolewe? Pengo ana haki ya kutoa maoni hapo hapo wengine wana haki ya kumkosoa -nao wanakuwa wanatoa maoni pia. Ni wajibu wa wananchi wanaopokea maoni kupima ya nani yanawafaa.

Pengo kajichanganya katika kutoa maoni yake. Apuuzwe tu!
 
Nimekumbuka kile kitabu changu

The Church and the Government
 
Kamanda tambua ule u katoliki uliotumika kumshawishi padre slaa kuondoka katikati ya vita ndio huo huo unaendelea hata sasa, tukaze buti tutafika tu
 
Umri na maradhi pengine vinachangia.......Cardinal angesema yote lakini sio kusema haoni umuhimu Wa katiba, kwakweli ameshangaza.
Inabidi tumsamehe mzee wa watu hataki matatizo kwa sababu toka mwanzo hakuna aliyesema kuwa matamshi ya askofu Niwemugizi ni ya kanisa katoliki. Matamshi ya kanisa hutolewa na TEC.
Umri na maradhi pengine vinachangia.......Cardinal angesema yote lakini sio kusema haoni umuhimu Wa katiba, kwakweli ameshangaza.
 
1. Anamshangaa vipi anajua msimamo na misingi ya habari ya kanisa katoliki ili hali yeye ni mlutherani?

2. Anajua nini maana ya ROMA LUCUTA CAUSA FINITO?

3. Angemshangaa huyo aliyetoa habari ambao si msimamo wa kanisa bali ni maoni ya mtu binafsi

4. Kama kitu ni msimamo wa kanisa hutolewa kwa njia ya waraka na sio kwa press conference ambaozo kila mtu akijisikia siku hizi anaitisha.
 
Kwa nini hampendi kuheshimu fikra na maoni ya wengine? Hayo ni maoni yake binafsi kama Raia wa Tanzania na ana uhuru na Haki kikatiba.
Shame!
Kumbe wewe na pengo hamna tofauti.
Ni maoni gani hayo yasiyo na kichwa wala miguu?
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kauli ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuhusu mchakato wa Katiba imewasikitisha.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema kiongozi huyo wa dini anapaswa kulinda heshima aliyonayo ndani na nje ya kanisa.

Akizungumza na Mwananchi, Mbowe amesema, “Askofu Pengo ni kiongozi wa kanisa, anaheshimika na wananchi ambao si wale anaowaongoza lakini kwa kauli yake kuhusu Katiba, imetushangaza na imenisikitisha.”

Mbowe amesema, “Suala la elimu, chakula na maisha yetu yanalindwa na Katiba, ndiyo msingi wa mifumo ya rasilimali za Taifa. Anaposema haoni umuhimu wa Katiba anatufikirisha, anataka kusema mchakato wa Katiba uliogharimu mabilioni ya fedha leo hauna maana?”

Amesema umefika wakati mchakato wa Katiba uliokwama ukaendelezwa na hasa kuanzia katika rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti, Jaji mstaafu Joseph Warioba.

“Katiba ni maridhiano, tunahitaji kupata maridhiano ya pande zote, nirudie tu kwamba alichokisema Askofu Pengo kinasikitisha,” amesema Mbowe.

Kardinali Pengo Jumamosi iliyopita alinukuliwa akisema kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi kuwa Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni yake binafsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Alisema hilo alipotoa ufafanuzi kuhusu sitofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo si msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu sisi tuna utaratibu wetu wa kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kipaumbele cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza yeye binafsi ni miongoni mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.

Chanzo: Mwananchi
kwahiyo Mbowe haruhusu mitazamo tofauti....anyway.....ila kikubwa ni kuwa ujumbe umefika.....
 
Hawa jamaa wananishangaza sana!

Wao hawataki wengine watoe maoni yao ambayo yanakinzana na mitazamo yao.

Mbaya zaidi wanaanza kumshambulia mtoa maoni kwa kutumia matusi na dharau.

Suala la katiba lilishabuma na CCM wanafahamu lilileta mgawanyiko mkubwa na upotevu wa pesa. Hawawezi tena kuingia kwenye tatizo hilo kwa kipindi hiki.

Tatizo kuu ni idadi ya serikali.

Huyu ngosha Magu hawezi kuleta tena huo mchakato katika kipindi hiki cha utawala wake wa miaka 5 labda atafanya hivyo katika awamu ya pili ya utawala wake.

Mchakato ule wa katiba ya Wananchi "ulibuma" kwasababu CCM walitaka kulazimisha maoni yao ya wachache yapite, ili kulinda maslahi ya chama chao. Wananchi (tulio wengi) tunataka katiba ambayo italinda maslahi yetu na ya nchi sio ya kikundi fulani tu cha walafi kama ilivyo sasa. Wewe na Pengo endeleeni tu kusinzia, ila ukweli ndio huo. Katiba mpya ni matakwa ya wananchi, na sio ya Magufuli.
 
Hawa jamaa wananishangaza sana!

Wao hawataki wengine watoe maoni yao ambayo yanakinzana na mitazamo yao.

Mbaya zaidi wanaanza kumshambulia mtoa maoni kwa kutumia matusi na dharau.

Suala la katiba lilishabuma na CCM wanafahamu lilileta mgawanyiko mkubwa na upotevu wa pesa. Hawawezi tena kuingia kwenye tatizo hilo kwa kipindi hiki.

Tatizo kuu ni idadi ya serikali.

Huyu ngosha Magu hawezi kuleta tena huo mchakato katika kipindi hiki cha utawala wake wa miaka 5 labda atafanya hivyo katika awamu ya pili ya utawala wake.

kama kuheshimu angeanza pengo. kwanini apige ya mwenzie ?
 
Siyabonga101: Mbona na yeye haheshimu maoni ya Askofu mwenzake Niwemugizi? Huyu mwenzake hakuwahi kusema anasema kwa niaba ya kanisa bali maoni yake kama mtanzania. Ina maana sasa tuseme hicho alichokisema pengo ndio msimamo wa Kanisa? Kwamba kanisa katoliki halioni umuhimu wa katiba bali mradi watu wanasoma na kula basi inatosha. Kwani hiyo haki ya kusoma na kula inalindwa na nini kama si katiba ya nchi?
Hayo ni maoni yake binafsi kama MTANZANIA na ana uhuru kikatiba ili mradi havunji sheria za nchi.
Huyo Mbowe kama alitambua umuhimu wa Katiba mpya kwa nini aliongoza kususia na kutoka nje ya Bunge wakati wa mjadala/mchakato?
Msiwafanye Watanzania wajinga kwa manufaa yenu binafsi tafadhali.
Watanzania wamechoka na hakuna mbadala wa Chama makini cha upinzani....kwa hiyo ni bora CCM ikamate DOLA mpaka hapo kitakapozaliwa Chama madhubuti na chenye sera shupavu ya kukamata Dola, na sio hiyo SACCOSS.
 
Naweza nikawa na uwezo mkubwa Wa kufikiri kukushinda wewe.

Uwezo Wa kufikiri mtu anazaliwa nao HAKUNA SHULE INAYOFUNDISHA UWEZO WA KUFIKIRI.
UNAWEZA UKASOMA SANA LAKINI UKAWA HAUNA AKILI
WEWE NI MMOJA WAPO.
Ungekuwa una uwezo mkubwa wa kufikiri kushinda mimi usingeninukuu na ungepita kimya.
Pathetic creature!
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kauli ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuhusu mchakato wa Katiba imewasikitisha.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema kiongozi huyo wa dini anapaswa kulinda heshima aliyonayo ndani na nje ya kanisa.

Akizungumza na Mwananchi, Mbowe amesema, “Askofu Pengo ni kiongozi wa kanisa, anaheshimika na wananchi ambao si wale anaowaongoza lakini kwa kauli yake kuhusu Katiba, imetushangaza na imenisikitisha.”

Mbowe amesema, “Suala la elimu, chakula na maisha yetu yanalindwa na Katiba, ndiyo msingi wa mifumo ya rasilimali za Taifa. Anaposema haoni umuhimu wa Katiba anatufikirisha, anataka kusema mchakato wa Katiba uliogharimu mabilioni ya fedha leo hauna maana?”

Amesema umefika wakati mchakato wa Katiba uliokwama ukaendelezwa na hasa kuanzia katika rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti, Jaji mstaafu Joseph Warioba.

“Katiba ni maridhiano, tunahitaji kupata maridhiano ya pande zote, nirudie tu kwamba alichokisema Askofu Pengo kinasikitisha,” amesema Mbowe.

Kardinali Pengo Jumamosi iliyopita alinukuliwa akisema kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi kuwa Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni yake binafsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Alisema hilo alipotoa ufafanuzi kuhusu sitofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo si msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu sisi tuna utaratibu wetu wa kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kipaumbele cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza yeye binafsi ni miongoni mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.

Chanzo: Mwananchi

Swali zuri la kumwuliza Kardinali Pengo ni je anaongoza Kanisa Katoliki (Dar es Salaam) kwa kutumia biblia tu (neno la Mungu) au kuna sheria za kanisa pia (zinazotoa mwongozo kutokana na mazingira tuliyomo)? Kama atajibu ni neno la Mungu pekee, ina maana pia katiba siyo kipaumbele. Lakini kama anatumia na Canon Law, then kusema katiba haina kipaumbele si kweli. Serikali haiwezi kutoa huduma za jamii bila ya kuwa na mfumo unaoeleweka wa kulinda au wa kuifanya serikali itoe hizo huduma katika ubora wake (kama inavyotakiwa).
 
Back
Top Bottom