Mbowe arejesha Shangingi la Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Hata kama sababu zote ulizosema hapo ni za kweli na ni kwamba anatafura umaarufu...., Lakini ukweli unabaki kuwa kwamba anaonyesha mfano wa kubana matumizi na kunusuru kodi zetu..., kwahiyo hata kama motive ni mbaya lakini alilofanya ni jambo zuri. Ningependa sana kama wabunge wote wangekuwa wapenda sifa na watafuta umaarufu ili nao wakatae huu ufujaji
 
Kufuatia mheshimiwa mbowe kiongozi wa kambi ya upinzania bungeni kuamua kuachia shangingi kumekuwa na maoni tofauti tofauti.
  • Kuna wanaoona kwamba kwa kufanya hivyo ameonyesha uadilifu na kwamba kama kiongozi ni mfano mzuri wa kuigwa na wengine.
  • Lakini kuna ambao wanaona kwamba hii ni kutokana na ukwasi alionao kwa hiyo hata alivyoachia hana cha kupoteza kutokana na kuwa navyo vingi.
  • Na kuna wanaona kwamba ni mtego kwa wanamagamba kwani wametumia ghalama kubwa kuingia bungeni wakitegemea sasa ni wakati wa kurejesha kile walichowekeza kwa wapiga kura ikiwa ni pamoja na faida. Kwa hiyo kwa kufanya hivyo ni njia ya kuwahalibia mipango yao.
  • Kuna wanaoona kwamba anatafuta umaarufu.
Kutokana na hayo maoni si vibaya namii nikatoa mtazamo wangu. Binafsi naona hoja nyingi ni dhaifu ispokuwa ya uadilifu kwani kuna wabunge wengi ni matajili lakini hawapo tayari kufanya hivyo.Kuhusu umaarufu mimi naona tayari anao na suala la kuwatega magamba inahitaji mjadala.

Sijui mwanajamvi unamaoni gani au upo upande upi?

Nimekuandalainia hiyo sentence kuonesha msisitizo. katika kila nchi kuna madaraja/matabaka katika mfumo wa uongozi. haiwezekani Rais wa nchi atembelee gari toka tradecarview, mawaziri pia na hata wabunge. hayo magari ya tradecarview ni yetu sisi tabaka la chini. na kama mnataka rais,mawaziri na wabunge watembelee magari hayo basi kuna hatari ya sisi watumishi wa kawaida kutembelea baiskeli, jambo ambalo halikubaliki.msiturudishe nyuma enzi za baiskeli za mbao.huyo mbowe anatafuta tu umaarufu.
 
Kanisani huwa tunahaswa kutoa haijalishi utajiri/umaskini wako (kutoa ni moyo...na bora anayenyosha mkono wake akaweza kumege kipande cha mkate wake akaweza kumrisha mwenye njaa

Mbele za Mungu,Mbowe katii maandiko na kwetu sisi masikini Mbowe yu mkombozi wetu maana si wote wenye navyo watavitoa ama wako tayari kula na sisi

Na ukitoa wewe umebarikiwa,huyu atabarikiwa!!
 
Posho zitatugawa! Watanzania hatuna mishahara tunaishi kwa posho!! Hii si mishahara bali maskhara. Yaani Mshahara sh. 2.3 million Posho Shs. 5.0 million. Sasa kama hatuishi kwa posho nini hiki? Posho ni mara 2.5 ya mshahara. Muonavyo hivyo kwamba wabunge wanaishi kwa posho ndivyo hivyo pia watumishi wengine wa serikali wanaishi kwa posho. Tuangalie posho zote. Tusiangalie posho ya Shs. 70,000.00 lakini tunafumbia macho posho ya Shs. 5.0 million. YTuidadavue hiyo ya Tshs. 5.0 million tuone ina nini ndani yake. Ama kweli posho ni janga la Taifa
Watu wanafata mkumbo tu wanampongeza Mbowe bila kujua, kwenye hizi posho nilizozibandika hapo hakuna ata moja ambayo Mbowe kazipinga, Mbowe anazopinga ni Sitting Allowance, sasa tafakari kama una akali timamu hizi zote mbowe na wenzake wanachukuwa
 
Nimekuandalainia hiyo sentence kuonesha msisitizo. katika kila nchi kuna madaraja/matabaka katika mfumo wa uongozi. haiwezekani Rais wa nchi atembelee gari toka tradecarview, mawaziri pia na hata wabunge. hayo magari ya tradecarview ni yetu sisi tabaka la chini. na kama mnataka rais,mawaziri na wabunge watembelee magari hayo basi kuna hatari ya sisi watumishi wa kawaida kutembelea baiskeli, jambo ambalo halikubaliki.msiturudishe nyuma enzi za baiskeli za mbao.huyo mbowe anatafuta tu umaarufu.
Kama nchi ingekuwa na uwezo huo halafu mambo yakaenda vuzuri ingekuwa hakuna tazizo. Lakini kwa wakati tulionao hayo magari si kipaumbele.
 
kama mnataka rais,mawaziri na wabunge watembelee magari hayo basi kuna hatari ya sisi watumishi wa kawaida kutembelea baiskeli, jambo ambalo halikubaliki.msiturudishe nyuma enzi za baiskeli za mbao.huyo mbowe anatafuta tu umaarufu.
Kaka naomba niseme kukosa exposure ndio kunakufanya useme hivi. Nchini Uholanzi (the Netherlands), nchi ambayo ni miongozi mwa nchi zinazofanya vizruo sana kiuchumi Sio ulay tu bali duniani, idadi ya Baskel inazidi idadi ya watu (nimeacha kuspport kwa evidence ili ufanye assignement kwa kugoogle kidogo) na mawairi hata wakurugenzi wanatumia Baiskeli kwenda kazini. Ni nchi iliyofanikiwa watu wake kuwa very efficient katika kutunza mazingira, kutunza muda kwa sababu ya matumizi ya baiskeli, Kule ukisikia kuna traffic Jam ni ya dakika 5 na watu kesho wanalalamika vibaya mno kwanini kulikuwa na jam. Sasa Dar mnakuwa na jam inayokuchukua mtu masaa zaidi ya 5 kutoka Posta mpaka Ubungo hapo sijasema ukitoka posta kwenda Kunduchi. Naomba uwe na uhakika na unachosema, nchi zilizoendelea zimerudi kwenye Baiskeli kutoka kwenye magari wakati wewe unadhani ni kurudi nyuma
 
Hitimisho.
  1. Tumeamua kumwandikia katibu wa Bunge barua ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhurio na kwa ajili ya posho na wabunge wa CHADEMA hawatasaini fomu za posho.
  2. Kuhusu magari, kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe ameamua kurejesha gari yake aina ya “Shangingi” alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada.
Tunawataka wabunge wengine waunge mkono hoja hizi kwa masilahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na ;………………………Mhe. Freeman A. Mbowe (Mb),Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.21 Juni 2011.
NImeipenda hii
 
Mbowe kaonyesha mfano wa kiongozi makini, kutoa shangingi lipigwe mnada si jamba rahisi hata kidogo. lakini mbowe kaonyesha kuwa kweli tukiamua tunaweza. Hongera sana Mbowe. Na wengine walio makini wafuate nyayo. Na CCm nawashauri someni alama za nyakati. Huu si uele wakati wa Zidumu fikira za M/kiti wa chama. Ni muda wa action siyo blaablaa tu kama za kina T. Hiza
 
Mbowe bwana anaponda mashangingi wakati kachukuwa milioni 90 kwa ajili ya gari, kachakuwa tena mkopo wa milioni 200 benki mdhamini wake ni ofisi ya katibu mkuu wa bunge, acha usanii bwana

Mkuu kumbe kachukua MKOPO! atalipa
 
Mkuu una tabia za popo, maana popo sio ndege na wala si mnyama,...........refer to thread yako isemayo, Asante sana mheshimiwa Zitto, lakini unatuuzia mbuzi kwenye gunia.
Nilitegemea hapa umkosowe Mbowe na sio kumpongeza kwa sababu katika falsafa yako ya kibepari uamuzi wa Mbowe ni kurudishana nyuma kuwa na viongozi maskini.
Ningeomba kukuuliza umetumia vigenzo gani kumpongeza Mbowe kinyume na msimamo wako wa hapo majuzi? mimi sio mfuata mkumbo nina hansard zangu za jamii forums.
Huyo mtu wa nyuyoko humjui nini leo anampongeza kesho utamsikia anasema Mbowe anatuuzia mbuzi kwenye gunia haaminiki huyo.
 
Du...!Bravo!
Nchini Burundi huu ndiyo utaratibu uliotumika!
Ilianza kama mzaha, lakini baadaye kweli kabisa viongozi wote waandamizi serikalini walilazimika kurudisha mashangingi, chini ya usimamizi wa Kamanda Kagame!
****** uko wapi?...wanaume washakuanzishia kutafuna, meza sasa!

Nchini Burundi???? Chini ya Kamanda Kagame???? Anyway yatakuwa ni matatizo yangu binafsi tu.........
 
mbowe kakataa shangingi la serikali ila atakuwa anatembelea vogue yake. unafiki tu, kafanya nini hapo
Hata akitembelea helikopta kama ni yake inatuhusu nini tulicho na concern nacho ni kile kinachotumia kodi zetu.
 
Rais wetu tunakuomba utoe maamuzi magumu ili wananchi wawe na matarajio hata kwa kutangaza kama Mbowe. Jamani mbona raia wako tunaumizwa hivi kuwagharimia?
 
quote_icon.png
By Memo
Yuko huyu FaizaFoxy, tarehe 7/6/2011 ametuma posts 75 kuanzia saa sita usiku Jumanne hadi saa sita usiku Jumatano. Huu ni wastani wa post zaidi ya tatu kwa saa, assuming halali kabisa na hana muda wa kusoma posti za wengine, je hii yawezekana ? Kwa mtindo huo atakuwa amefikisha posti 75 x 365 = 27,375 na kumpita Mwanakijiji aliyejiunga na JF mwaka 2006 ! Mfano kidogo ni posti zake hizi;
  1. 6.16 pm
  2. 6.19 pm
  3. 6.21 pm
  4. 6.24 pm
  5. 6.25 pm
  6. 6.26 pm
  7. 6.29 pm
  8. 6.29 pm
  9. 6.31 pm
  10. 6.32 pm
Hizi ni posti kumi kwa robo saa ! Kwa ufupi ni kuwa katika masaa 24 aliweza tu kupumzika kwa masaa chini ya manne (kati ya saa kumi usiku na saa mbili asubuhi), je ni binadamu au mashine ! Hapumziki, halali, hali, haogi, haendi chooni - anayo kazi moja tu kuitetea serikali ya KiweteKikwete. Je hii ni ajira au utumwa ?Duh, yaani Chadema inawakosesha watu usingizi namna hii !
Naamini kama JF wangekuwa wanatoza pesa kwa kila post wapuuzi kama hawa wangepungua.
 
Back
Top Bottom