Mbowe arejesha Shangingi la Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Mbowe yuko sereous sana kwenye mambo ya taifa, huu ujasiri naomba utuambukize na sisi wananchi ili tulinde kura zetu October 25 ,2015

Ujasir wa kutudanganya watanzania alipokabidhiwa aliahidi kulirudisha mpk waandishi wa hbr na pic nyingi alipiga lkn cha ajabu gari hadi leo analo na anapgia kazi za bnafic kibao Duh siasa jaman
 
Mashangingi sio kuwa yapo kwa viongozi wenye afya mgogoro maana naona wengi wana umri vile. Labda kama tukichagua vingozi wa umri mdogo au watoke Mbeya, Kigoma na kanda ya ziwa ukiondoa Kagera
 
Ningemkubali sana kama angelirejesha siku aliyopewa. Lakini anaona kipindi cha bunge kinakishwa na ni lazima alirejeshe maana hatokua tena n a hiyo fursa ya kulitumia ndo anadai analirejesha. Nitamuona mzalendo wa kweli na pia mjali mali za watanzania kama akizirejesha na zile pesa za matumizi ya gari toka alipokabidhiwa. Akifanya hivi nitampa kura yangu
 
ndo anakumbuka leo!!!! c alilifwata huyu jamaa ni mnafiki kwa watanzania
mtu anaependa cheap popularity
hafai kuwa kiongozi!!!!
 
Mbowe ni mnafiki sana. Ukiyauza mashangingi ukatoa mikopo ya magari, allawansi za dereva, matengenezo na mafuta gharama si imerudi palepale au ni nafasi kwa Mheshimiwa kubana masurufu? Halafu ukiyauza magari kila baada ya miaka mitano kuyanunua tena kwa mkopo. Mikopo yenyewe haina riba au kodi na siyo lazima hata wayanunue magari yenyewe. Hesabu zimekaaje

Pili ukiondoa posho za vikao unamkomoa nani? Huo ni motisha viongozi wakutane badala ya kusafiri. Kusafiri ni ulaji kukaa ofisini hakuna motisha.
 
soma tamko lililotolewa muda huu bungeni.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2011/2012

Utangulizi
Mnamo tarehe 21/06/2011 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2011/2012.

Pamoja na Bajeti ya Serikali kukubali na kuzingatia baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani CHADEMA kama vile ;

a) Kupunguza kodi na tozo mbalimbali kwenye mafuta ya petrol na dizeli.

b) Kupunguza kiwango cha faini za makosa ya barabarani kutoka shilingi 300,000/50,000 hadi kufikia ukomo wa shilingi 30,000.

c) Kufuta leseni za biashara kwenye Majiji,Halimashauri za Wilaya na Vijiji.

d) Kufuta misamaha ya kodi kwenye makampuni yanayotafuta mafuta na gesi Nchini.
e) Kuongeza pesa kwenye bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kwa kuhakikisha kuwa kodi ya skills development levy 2/3 inapelekwa kwenye bodi kwa ajili ya Mikopo.


Katika kupitisha bajeti hiyo wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani wa CHADEMA tuliamua kupiga kura za HAPANA kwenye mapendekezo hayo ya Serikali kutokana na sababu mbalimbali na haswa hizi zifuatazo;
1. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuondoa posho za vikao (sitting allowances) kwenye mfumo wa malipo ndani ya serikali.

2. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa magari yote aina ya "Mashangingi" yanayotumiwa na viongozi na watumishi wa umma yauzwe kwa mnada ndani ya miezi sita na viongozi hao wakopeshwe magari kwa ajili ya kufanya majukumu yao mbalimbali.

3. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kufuta/kupunguza misamaha mikubwa ya kodi ambayo Makampuni ya Madini yanapata ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

4. Serikali imekataa kuingiza pensheni kwa ajili ya wazee wote nchini ya shilingi 20,000 kila mwezi ili kuweza kuwapunguzia ukali wa maisha wazee wetu .

5. Serikali imekataa Kufuta/kuondoa misamaha ya kodi kwa kipindi cha miaka 10 kwenye maeneo maalum ya uwekezaji (EPZ).

6. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa tunapunguza gharama za safari na haswa kuhakikisha kuwa ni viongozi wakuu na wenzi wao tuu ndio waruhusiwe kusafiri kwa kutumia daraja la kwanza (first class) ambao ni ;


  • Rais
  • Makamu wa Rais
  • Waziri Mkuu
  • Spika
  • Jaji Mkuu
Mawaziri wasafiri kwa kutumia daraja la pili (bussines class) na viongozi wengine wote wa umma na watumishi wa umma wakiwemo wabunge wasafiri kwa kutumia daraja la kawaida (economy class).

Pia misafara ya viongozi wakuu ipunguzwe ili kupunguza gharama za kuhudumia misafara hiyo pindi wanaposafiri nje ya Nchi.

Hitimisho.

  1. Tumeamua kumwandikia katibu wa Bunge barua ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhurio na kwa ajili ya posho na wabunge wa CHADEMA hawatasaini fomu za posho.
  2. Kuhusu magari, kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe ameamua kurejesha gari yake aina ya "Shangingi" alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada.
Tunawataka wabunge wengine waunge mkono hoja hizi kwa masilahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na ;
&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];
Mhe. Freeman A. Mbowe (Mb),
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
21 Juni 2011

hahahahahaaa
 
Two don't wrongs don't make it right.
Pamoja na unafiki wa Mbowe, lakini serikali ya CCM ndiye yenye sera ya hayo mashangingi. Pinda alisema wameacha kununua hayo mashangingi. Magufuli kayarudia kwa kasi ya hatari. Yeye anatumia LC200 Limousine. Dawa ya kumaliza unafiki wa Mbowe ni serikali kuondoa hiyo sera ya magari ya bei mbaya.
 
unacheka nini? haya yalikuwa ni maagizo ya Pinda na mbowe alikuwa wa kwanza kurejesha la chaa jabu viongozi wa ccm mlikataa sasa mlitaka gari ya mbowe iuzwe? malofa nyie
Kwi kwi kwi!Uongo dawa yake muda tu!
 
Back
Top Bottom