Mbowe anusurika kifo mara tatu

Mbowe anusurika kifo mara tatu

Members wengine humu huyu sawa na baba yenu...shikeni adabu zenu!

MJENGONII%2B020.jpg
 
Mwnyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema amenusurika kuuawa katika matukio matatu yanayotokana na harakati zake za kisiasa.

Akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mji wa Meatu mkoani Simiu jana, Mbowe alisema hata kama atauawa hatasikitika na kwamba Watanzania wasimlilie.

Mbele ya umati huo akiwemo mbunge wa Maswa, John Shibuda, Mbowe alisema kuna watu ndani na nje ya CHADEMA ambao wamekuwa wakifanya kila mbinu kuwaangamiza viongozi na makada wa chama hicho.

Mbowe alisema viongozi wa CHADEMA akiwemo yeye mwenyewe wamekumbana na misukosuko mingi, ikiwemo yenye kuhatarisha maisha yao kutoka kwa wanasiasa wasioipenda nchi, lakini kwa neema ya Mungu wamenusurika.

“Leo hii hata kama nikiuawa, naomba Watanzania msinililie. Mbele ya jeneza langu, nizikeni huku mkisema Bwana Alitoa na Bwana Ametwaaa, Jina Lake Lihimidiwe.

“Leo CHADEMA sio ya Slaa wala ya Mbowe bali ya Watanzania iliyojengwa kwa misukosuko mingi na mkono wa Mungu.

“Mmeshuhudia namna viongozi wake walivyonusurika kuuawa na kufungwa, na watu kufunguliwa na kesi mbalimbali.

“Kwa hiyo yeyote awe kiongozi wa CHADEMA au watawala anayetamani kuibomoa chadema hataweza kamwe,” alisema.

Kiongozi huyo alisema wale wote wanaofanya hivyo, wajue kuwa wanapambana na mkono wa Mungu na wamelenga kuwaumiza Watanzania.

“CHADEMA ina baraka za Mungu na ndio maana imeshinda na kupita katika majaribu mengi ya watawala ambao wameshindwa kuifuta au kuibomoa,” alisema.

Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wako katika ziara ya mikutano ya mabaraza ya wazi kujadili rasimu ya Katiba mpya ambayo itaendeshwa nchi nzima kwa nia ya kukusanya maoni ya Watanzania.

Chanzo: Tanzania Daima

MY TAKE:
Hii inaonyesha siasa za Africa ni ngumu na nizakidhalimu maana watu wanaviziana h ata kwa kuuwana.

Mzimu wa CHACHA WANGWE naona bado unamwandama. na bado, maana imeandikwa auaye kwa panga na yeye atakufa kwa panga
 
kwani jaribio la kuuawa lina uhusiano gani na shughuli za kisiasa

Ndo uwe unasoma vizuri sasa. Alieleta uzi ameelezea kisiasa na ugumu uliopo kuwa mwanasiasa Afrika.
Mwingine akaja kusema Mbowe amedanganya eti amenusurika kuuawa na Ponda nae asemeje. Then followed my question. Soma kwa hatua.
 
sasa Mbowe anadanganya watu ili aonewe huruma? yeye kama amenusurika kufa Ponda naye atasemaje?

Tofautisha Ponda gaidi anaye lia lia na udini mwenye kuongoza kundi la wasio ona wala kusikia na Kamanda Mbowe ambaye anamtetea Ponda .
 
afe tuuuu, kwani ye nani??? wamekufa watu wa maana sembuse mjasiriamali wa siasa bana
 
Tofautisha Ponda gaidi anaye lia lia na udini mwenye kuongoza kundi la wasio ona wala kusikia na Kamanda Mbowe ambaye anamtetea Ponda .
gaidi ni lwakatare na henry kilewo ambao wanalisha watu sumu na kuwamwagia tindikali. walaaniwe milele
 
Ndo uwe unasoma vizuri sasa. Alieleta uzi ameelezea kisiasa na ugumu uliopo kuwa mwanasiasa Afrika.
Mwingine akaja kusema Mbowe amedanganya eti amenusurika kuuawa na Ponda nae asemeje. Then followed my question. Soma kwa hatua.

hivi mtu aliyenusurika kuuawa na aliyeuawa, ni tukio lipi lina ushahidi
 
Hakuna haja ya hofu, Mungu yupo upande wetu daima....
 
Tofautisha Ponda gaidi anaye lia lia na udini mwenye kuongoza kundi la wasio ona wala kusikia na Kamanda Mbowe ambaye anamtetea Ponda .

hayo ni matusi kwa waislam. ina maana waislam wanaomfuata Ponda ni kuwa hawaoni?
 
Hakuna haja ya hofu, Mungu yupo upande wetu daima....

Pompo, wala usimtetee Mbowe. yeye alimuua CHACHA WANGWE, na yeye ipo siku atakufa tu. iwe kwa ajali au kuumwa
 
sasa Mbowe anadanganya watu ili aonewe huruma? yeye kama amenusurika kufa Ponda naye atasemaje?

Hebu nipe FAIDA chanya mbili tu za Sheikh Ponda kwa watanzania(sitaki kwa waislamu) ili nami nikupe FAIDA zaidi ya 10 za Mbowe kwa waTZ
 
Haya yote yatafikia mwisho....!! Kila la kheri CDM katika ukombozi wa nchi hii kutoka mikononi mwa mafisadi.....!!
 
Back
Top Bottom