Mbowe amtolea uvivu Lipumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe amtolea uvivu Lipumba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, May 15, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,843
  Likes Received: 11,962
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemshutumu Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, kuwa ni miongoni mwa wanasiasa wanaowahadaa wananchi kutojiunga na Chadema kwa sababu ya dini zao.

  Akituhubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Tunduru jana, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kwa muda mrefu viongozi wa CCM wakiwatumia viongozi wa dini na baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitoa shutuma kuwa chama hicho kina udini na ukabila na kueleza kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.

  "Mheshimiwa Lipumba namuheshimu sana, lakini amekuwa akiwahadaa wananchi kwa kuwataka wasijiunge na CHADEMA kwa kuwa ni chama cha udini na ukabila". Tanzania hakuna chama kama hicho alisema.

  "CHADEMA kina watu wa dini na makabila tofauti. Kuna watu wanaotoka Arusha, Mbeya, Iringa na hata Zanzibar, sasa huo udini wanaosema unatokea wapi?" alihoji Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

  Katika mkutano huo, Mbowe alionyesha barua aliyoeleza kuwa imesambazwa na maofisa wa usalama wa taifa kwa masheikh wa Ruvuma na mkoani Mbeya ikiwataka Waislamu kutohudhuria mikutano ya CHADEMA kwa madai ya udini na ukabila.

  "Watu wa Usalama wa Taifa wamesambaza barua kwa masheikh wa Ruvuma na Mbeya inayoeleza kuwa waumini wa dini hiyo wasihudhurie mikutano ya CHADEMA kwa kuwa ni chama cha Kikristo na kina Ukabila," alisema Mbowe huku akionyesha barua hiyo kwa umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  PHP:
  "Watu wa Usalama wa Taifa wamesambaza barua kwa masheikh wa Ruvuma na Mbeya inayoeleza kuwa waumini wa dini hiyo wasihudhurie mikutano ya CHADEMA kwa kuwa ni chama cha Kikristo na kina Ukabila," alisema Mbowe huku akionyesha barua hiyo kwa umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo
  Ndio maana tukastuka na kuhoji tangu mapema kuhusu kazi haswa ya hawa TISS!...wANAKUWA KAMA KAMPUNI YA MTU BINAFSI!
   
 3. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Hizo zote ni mbinu za kukiangusha chama! Ila hakuna jipya wanaloweza kuongea zaidi ya udini! Tumechoka na bra bra za CCM za kukishu2uma chama kila mara udini udini, hawaon kuwa wanajionyesha ni jinsi gani walivyodhaif kimawazo, kama mbowe alivyosema chama ci cha kidini maana kimechukua viti sehemu mbalimbl nchni, siyo moja kwahyo watasemaje ni chama cha dini... Kama kingekuw chama cha dini basi kila mara kingekuwa kinatetea wakristo pekee na ci watanzania! Inamaana watanzania ni wapumbv kiasi gani mpaka waambiwe kuwa ni chama cha dini,wakati wanaakili timamu za kuchambua mambo ndo mana wamekichagua kiwaongoze.. CCM shughulikieni mambo ya maendeleo ci kila kukicha ni kupambana na chadema, tekelezeni yale mambo ambayo chadema inajaribu kuyaweka sawa! Msipofanya hvyo basi chama chenu ni kushnahi na Chadema itaendelea kutikisa milele.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wanapiga kote kote, yaani no stone will be left unturned and untouched.
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,843
  Likes Received: 11,962
  Trophy Points: 280
  Walimlea sana Lipumba naona sasa Chadema inataka kula naye sahani moja hakuna kuleana ni mwendo live live kwa wanafiki wote wawe chama tawala ama wapinzani.
   
 6. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  hawana tofauti na KK hawa...
   
 7. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wanatapatapa, kama kweli kuu anauzibitisho basi lazima tuoji ualali wa Usalama wa Taifa kuingilia mambo ya siasa, kweli CCM noma wanajaribu kutumia kila mbinu kuangusha upinzani. buti ipo siku wataanguka tuuu
   
 8. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwanini wao? Nafurahi kusikia kuwa hakuna chama cha kidini lakini imechukuwa muda kukubali hilo! Tulizoelea kusikia CUF kuwa ni cha udini!
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ngekewa ndugu yangu, umesahau kuwa aliyeongoza kukiita CUF chama cha kidini ni huyo huyo Kikwete?
   
 10. K

  Kihyoi Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 11. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wow.... WOw CDM tafadhali sana chungeni midomo ili mueleze sera zenu zikubalike. Acheni kutolea uvivu watu au kujibishana na watu kama Nape. Inakuwa sasa mnacheza miziki mingi kwa pamoja ebu elezeni sera zenu kwa ufasaha ili watu wawaelewe vyema kwani mumeshaungwa mkono tayari na umma. Acheni kutaja majina ya akina Lipumba n.k elezeni sera kisha semeni juu ya udini huo bila kutaja majina yao.
   
 12. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hapana watu kama Lipumba wakiachwa waendelee eti kutunza heshima watu watachukulia wanachosema ni kweli hakuna siasa za heshima sasa mtu anakatiwa live.
   
 13. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Ajira za usalama wa taifa ziangaliwe upya au tayari watoto wa vigogo washapewa ajira huko nini? Wasije wakaigeuza ka walivyofanya BoT. TISS now ni ka NGO
   
 14. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  TISS,PCCB,DOWANS,RICHMOND,EPA,MEREMETA.
  Ee Baba wa mbinguni naomba uingilie kati.
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,270
  Likes Received: 19,413
  Trophy Points: 280
  mbona profesa Safari hawamtumii ipasavyo kwenye mikutano ya hasa huko ruvuma?
   
 16. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu siasa za siku hizi sio za kuuma uma maneno. Sio za kinafki. Usipotaja majina na kueleza ukweli vizuri utaambiwa toa ushahidi. Ukitaja biashara imekwisha.

  I think sio vizuri kupuuzia kauli za kipuuzi zinazotolewa na wanasiasa wengine kwani zinaweza kuwa na madhara makubwa sana. Ni lazima kuzishughulikia na kisha kuendelea kutangaza sera.

  Unakumbuka kampeni za uchaguzi zilipoanza 2010? Ni nini kilimfungam mdomo makamba? Baada ya kuambiwa aeleze umma kwa nini alifukuzwa ualimu mkuu. Simple, ndivyo siasa za Tanzania zinavyoenda. Hoja kwa hoja, upupu kwa upupu.
   
 17. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni lazima ku defend na ku attack..
  Makamba alinyamza kimya, Shimbo, Kinana, na Nape juzi kashindwa kujibu shutuma za Mpendazoe
   
 18. t

  tambarare Senior Member

  #18
  May 16, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaaani kama kuna viongozi wenye akili hasi na mgando ni hawa wa chama cha magamba.........hivi mpaka sasa hawajui kwa nn wanainchi wa tanzania wanakichukia chama chao??????? hata mtumie nguvu gani chama kimekwenda na maji ............HUWEZI ZUIA MAJI KATIKA MKONDO WAKE BALI UNAWEZA UKAYABADIRISHIA MKONDO MAJI .........SASA KAMA NINYI BADO MNAONA KUWA MNAWEZA ZUIA MAJI ENDELEENI MUONE MWISHO WAKE
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kweli mkuu na alivyotajwa next time kabla ya kuropoka Lipumba atakuwa anajiuliza mara mbilimbili hata akisema watu watakuwa na mawazo ya kuwa huyu jamaa ni mdini, wanavyofanya Chadema ni sawa kabisa mbona wao wanatajwa tena kwa majina kwanini wao wakitaja wanaambiwa wasiattack.
   
 20. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #20
  May 17, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33


  Umesahau KAGODA na ndugu zake wengine
   
Loading...