Wakuu zangu kuna habari nzito sana kuhusu huyu jamaa yetu Lipumba na sijui baada ya kuisoma hii habari kama mtakuwa na hamu naye tena..
Nikiwa Chef Pride na wanachama wa CUF ambao kwa uhakika wana asili ya Zenj, walinijulisha habari moja tata sana sasa sielewi kama ni udaku wa kumpaka Mbowe na Chadema au ndio ilivyotokea haswa..
Yasemekana baada ya Muafaka wa Zanzibar na CCM viongozi wa Chadema waliwafuata viongozi wa juu wa CUF bara na kuwaomba wajumuike pamoja kuunda nguvu moja itakayowawezesha kuishinda CCM bara..Na Lipumba akiwa mwakilishi wa CUF aliyapokea maombi hayo na kuyapeleka Zenj kwa makusudi ya kuwambia mbinu ya Chadema kuwatenganisha CUF visiwani na bara..
Hawa jama kwa uhakika wanaichukia Chadema kwa kufanya move hiyo ambayo haikuwajumuisha Wazanzibar hata baada ya kuungana na CCM hivyo ktk mtazamo wao kuungana kwa CUF na Chadema bara ni njama ya kuiangusha CUF visiwani na ndio hapo chuki kubwa ya wanachama wa CUF ambao wengi ni Wazenj kwa asili ulipoanza na hakika CUF yenyewe kutangaza vita kati yake na Chadema..
Sasa mimi nisichoelewa haswa ni kwa nini iwe vigumu kwa CUF na Chadema waungane bara lakini halali kwa CUF na CCM visiwani kuungana, tena chuki hii imetokana na Lipumba mwenyewe kumwaga mboga visiwani..Je hivi kweli Inahusu? hata kama hakupendezewa muungano wa vyama hivi bara kulikuwa na maana gani kwa Lipumba, msomi mwenye nia ya kuwaondoa CCM madarakani kwenda kufitinisha vyama ktk wakati muhimu sana wa uchaguzi..
Hata hivyo, msinitoe roho hizi ni habari za kijiwe cha Wapemba hivyo tuyapokee kama yalivyo..