Mbowe ameshakosa sifa ya ubunge mahakamani!

Mbowe ameshakosa sifa ya ubunge mahakamani!

Amekosaje?? Makhakama ya wilaya siyo ya mwisho. Kuna nyingi sana juu ya hiyo. Acheni ushabiki wa upofu.
 
Ni baada ya kutiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja au faini mahakamani jana.

Hakuna kitu kama hicho. Mbona mafisadi wa Richmond, EPA, Meremeta, Deep Green Finance, Buzwagi, Kiwira, Tokomeza, ESCROW wametiwa hatiani na bado wameendelea kuwa wabunge na mawaziri na sasa wanafanya kufuru kubwa zaidi ya kutaka kuwa rais? Je, hilo hujaliona?
 
Ni baada ya kutiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja au faini mahakamani jana.
Mkuu tafuta ushauri kabla hujahukumu mbona Mtikila alishinda baada ya kufungwa mwaka mmoja.Sifa bado anayo kwakuwa si kosa la kukwepa kodi au kimaadili,sheria ukiijua unadunda wanzaidi kushangaa
 
Kumchapa makofi mtendaji wa umma (msimamizi wa kituo cha uchaguzi) mzembe na mpuuzi sio tuu kuwa hakumkoseshi sifa za uongozi Mbowe au kiongozi yeyote bali kunamwongezea sifa zaidi kuwa huyo ni kiongozi makini na anayechukua maamuzi sahihi kwa wakati muafaka.
Hukumu hii itakuwa rejea kwa uchaguzi mkuu wa oktoba pale ambapo wasimamizi wa vituo wataleta masihara. Tutawachapa makofi sana ili wakaonyeshe mashavu yaliyovimba kwa wake/waume zao ili watimize wajibu wao na hukumu ya mwaka jela au faini ya milioni moja tunachangishana kulipa lakini haki inakuwa imetendeka ipasavyo.
Hii ni hukumu imetuondoa woga. Wito kwa wale tutakao tembeza makofi, judo na kareti, mahakamani hakuna haja ya kukana shtaka maana linaweza kutupotezea muda ni kukiri na kulipa faini na kuendelea na shughuli zingine huku mgombea aliyeshinda kihalali akitangazwa mshindi.
Mbowe kila siku unakuja na fundisho jipya, hakika hili nalo ni fundisho. HONGERA.
huyu mbugila wala hakuwa msimamizi, yeye alienda kama mwangalizi lakini kwenye list ya waangalizi iliyotolewa na tume ya uchaguzi wala hakuweno na alipoombwa kitambulisho hakuwa nacho
 

Kumekuwa na mjadala mkubwa tangu jana baada ya hukumu ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Hai, Denis Mpelembwa kuhusu kesi ya jinai na. 73 ya mwaka 2011.

Mjadala uliokuwa unaendelea kwenye mitandao ya kijamii zikiwemo forums kama Jamii Forums na kwingine ambako wanachama wanajadili masuala serious ya kisiasa, kijamii na kiuchumi, imeleta hali ya utata kuhusu sifa za kugombea ubunge.

Vyombo vya habari baadhi vikitumia anonymous sources, wanasheria bila hata ya kufanya citations either ya vifungu vya katiba, sheria za nchi au precedence zilizowekwa na kesi zingine za namna hiyo, vimekwenda hatua ya kuandika kuwa Mwenyekiti Mbowe amepoteza sifa za kugombea uchaguzi kwa sababu ya hukumu hiyo.

Vyombo vya habari makini vimefanya uchambuzi kwa kunukuu wanasheria ambao wamefanya citations na kutoa precedence zilizowahi kutokea.

Mathalani katika Gazeti la Mwananchi wakitumia kichwa cha habari "Hukumu ya Hakimu Mkazi; Mbowe azua utata wa sifa ya kugombea; Mbowe ahukumiwa, utata wa sifa ya kugombea waibuka - Kitaifa wameandika;

"Hata hivyo, Mwanasheria, Alex Mgongolwa akinukuu Katiba ya Tanzania Ibara ya 67 (1)(c); 67(2) (c na d) alisema hukumu hiyo haiwezi kumzuia kugombea ubunge kwa sababu hakwenda jela na kosa lake halihusu kukosa utovu wa uaminifu, kukwepa kodi wala kuvunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

"Suala hilo linafanana na lililotokea katika mchakato wa uteuzi wa wagombea urais mwaka 2005 wakati aliyekuwa mgombea urais wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila na mgombea mwenza wake, Saidi Soud Said walipowekewa pingamizi kutokana na kutumikia kifungo jela, Mtikila akitumikia mwaka mmoja kwa kosa la uchochezi,

Said akitumikia chuo cha mafunzo kwa kosa la biashara ya vitambaa. Hata hivyo, pingamizi hilo lilitupwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame (marehemu) baada ya kusikiliza utetezi wa Mtikila na Said, kuwa makosa waliyofungwa kwayo hayakuwa ya kukwepa kodi, kukosa uaminifu wala kukiuka maadili ya viongozi wa umma."


Kesi hiyo ya Hai, inatukumbusha kesi ya aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare ambaye mwaka 2006 alishtakiwa na baadae kuhukumiwa kwa kosa la namna hiyo, kisha akawa na sifa za kugombea ubunge mwaka 2010 katika jimbo hilo.

Tutawapatia taarifa kamili juu ya hatua ambazo wanasheria wa chama wanachukua baada ya kupewa maelekezo juu ya kesi hiyo.

Kwa sasa kauli aliyotoa Mwenyekiti wa Chama jana baada ya hukumu hiyo, zinapaswa kuwatia ari wapiganaji kusonga mbele kuendelea na majukumu ya kupigania haki kila mahali, wakijipanga kuiondoa CCM madarakani.

Kwa wale wanaoweza kusoma, ni vyema wakapitia Katiba ya Tanzania, Chapter 3, Part II, Section 67(2).

"Akizungumza nje ya chumba cha Mahakama hiyo, Mbowe aliwatoa hofu wanachama wa Chadema kwamba wasikatishwe tamaa na hukumu hiyo ambayo alisema alitegemea ingekuwa hivyo.“Mnanipa pole ya nini? Kuna msiba hapa? Tupeane hongera. Sikutarajia cha tofauti na hiki kilichofanyika. Hakinivunji nguvu, bali kinaniimarisha katika mapambano,” alisema.

“Haki katika nchi hii itapiganiwa kwa watu wengine kuumia na wengine kuokoka. Nimesota mahakamani miaka mitano badala ya kufanya kazi ya wananchi. Hainivunji moyo,” alisema na kuongeza:

“Hainivunji moyo katika azma yangu ya kuikomboa nchi hii na ukombozi uko jirani. Mahakama ya nchi hii vimekuwa ni vyombo vya kutoa dhuluma kwa wananchi japo siyo mahakimu wote. Lakini iko siku Mahakama zitakuwa ni sehemu ya kutolea haki, kutenda haki na haki ionekane imetendeka. Mapambano yanaendelea na nawaomba msiwe wanyonge,” alisisitiza.

“Sitaki kuizungumzia Mahakama katika hatua ya sasa lakini ndani ya Mahakama kuna watu wanaotenda haki na ndani ya Mahakama kuna watu wasiotenda haki,” alisema Mbowe.

Alisema kesi hiyo haikustahili kuiendesha kwa miaka mitano na kwamba kodi za wananchi zinateketea pamoja na muda, akisema haiwezekani nchi ikaendeshwa katika utaratibu huo.

“Kama mimi mbunge, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mtunga sheria wa nchi hii naweza kusoteshwa mahakamani miaka mitano, mwananchi wa kawaida atafanywaje?” alihoji Mbowe."

Makene


Mkuu tunashukuru sana kwa ufafanuzi huo wa kisheria kutoka kwa mwanasheria mgongolwa,kwani hapa jukwaani wana ccm na act,wamekuwa wanapotosha sana jamii juu ya majaaliwa ya mbunge wa jimbo la hai,na kilichopelekea hayo yote ni woga wao juu ya mwanasiasa huyu nguli na kiongozi wa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.
 
Kamanda mbowe hana litakalomzuia kugombea kwa sababu (i) Hajafanya kosa lolote linaloambatana na kukosa uaminifu (ii) kukwepa kodi (iii) kuvunja maadili ya uongozi wa umma.

Hata mtikila aligombea uraisi 2005 japo alikuwa ametoka kufungwa miezi 6 jela, na wagombea wenzake walipomuwekea pingamizi, jaji Makame alitengua pingamizi kwa sababu havikuangukia kwenye makundi hayo.

Sasa kama CCM walikuwa wanaivuta kesi miaka mitano toka 2010 ili waje wamuwekee pingamizi wamechemsha.

Mshauri wa ccm ni adui yao namba moja
 
Precedence ya mtikila Yeye alienda jela 1 year kwa uchochezi. Hakuwa na faini. Na aligombe urais. What matters, kwa katiba ya sasa.. mtikila hakufungwa jela/ wala mbowe hakuhukumiwa kwa utovu wa uaminifu; kwa kukwepa kodi wala kwa kuvunja maadili ya viongozi wa umma. precedence ya mtikila kwa lugha nyepesi ilitengeneza sheria ambayo inabidi ifuatwe kisheria inaitwa case law

Huu utitiri wa vyuo vinavyotoa wanasheria ni hasara, maamuzi ya mwenyekiti wa NEC unayaita kuwa case law? Case law inatokana na hukumu ya kimahakama siyo utashi wa jaji nje ya huduma ya mahakama..! waweza kunikosoa.
 
Kosa alilo hukumiwa nalo hata asipokata rufaa kisheria halimzuii kugombea ubunge kamwe. Unakumbuka kesi ya Mtikila na mgombea mwenza wake pale walipokua wanagombea uraisi wakawekewa pingamizi na ccm pale nec chini ya Jaji Makame? Mtikila alikaa gerezan miezi6 na mgombea mwenza kwa mwaka1 lkn bdo Nec chini ya Makame ikaona kosa lililowahukumu bdo halimzuii kugombea uraisi.
Wewe mdanganye, kwa vile maamuzi ya jaji yalitolewa nje ya huduma ya kimahakama... yanaweza kutenguliwa hata na hakimu wa mahakama ya mwanzo. Ingawa angeyatoa katika huduma ya kimahakama yangegeuka sheria kwa mahakama zote za chini. Kwa hiyo, huo uamuzi ulitokana na utashi wa jaji makame tu, siyo utashi wa mahakama.
 
Wewe mdanganye, kwa vile maamuzi ya jaji yalitolewa nje ya huduma ya kimahakama... yanaweza kutenguliwa hata na hakimu wa mahakama ya mwanzo. Ingawa angeyatoa katika huduma ya kimahakama yangegeuka sheria kwa mahakama zote za chini. Kwa hiyo, huo uamuzi ulitokana na utashi wa jaji makame tu, siyo utashi wa mahakama.

Sio swala la utashi wa judge makame hapa bali swala lipo wazi. Sherua inasema kuwa kama kafanya kosa lolote la namana yoyote linaloambatana na utovu wa uaminifu. Full stop. Hivyo kosa alilofanya mboe ni lile linaloambatana na utov wa nidham ya kueshimiana mtu na mtu due to emotions and in accordance to the environments . ukiwa ccm unakuwa huna akili kabisa mana z8nakuwa zimebadilika kuwa akili za unafiki.
 
huyu mbugila wala hakuwa msimamizi, yeye alienda kama mwangalizi lakini kwenye list ya waangalizi iliyotolewa na tume ya uchaguzi wala hakuweno na alipoombwa kitambulisho hakuwa nacho

kwahiyo kumbe huyu jamaa alikuwa muhuni tu aliyevamia kituo cha kura ( inawezekana kwa malengo ya kukwapua simu au uhalifu mwingine ) , safi sana mbowe .
 
Sio swala la utashi wa judge makame hapa bali swala lipo wazi. Sherua inasema kuwa kama kafanya kosa lolote la namana yoyote linaloambatana na utovu wa uaminifu. Full stop. Hivyo kosa alilofanya mboe ni lile linaloambatana na utov wa nidham ya kueshimiana mtu na mtu due to emotions and in accordance to the environments . ukiwa ccm unakuwa huna akili kabisa mana z8nakuwa zimebadilika kuwa akili za unafiki.

Hizi taaluma za watu, matusi na mapovu hayasaidii.. Turudi kwenye hoja, maamuzi ya mwenyekiti wa NEC siyo maamuzi ya mahakama ingawa huyo mwenyekiti ni alikuwa ni jaji. Kwa hiyo yasitumike katika hili suala, maana hata yakitumika hayatasaidia. Unakumbuka kesi ya Zombe? tume iliyoongozwa na majaji ilitoa ripoti gani na mahakama ilitoa hukumu gani? Nguvu ya maamuzi ya jaji ni mahakamani tu, nje ya mahakama hata PCM atatosha kuyatengua!
 
natoa onyo kwa yeyote atayejaribu kuhujumu haki kwenye vituo vya kura , asijaribu , atashughulikiwa bila huruma , MBOWE NI SHUJAA ! maana kiongozi ni lazima kuwa mfano wa kulinda kura .
 
Back
Top Bottom