Mbowe ameshakosa sifa ya ubunge mahakamani!

Mbowe ameshakosa sifa ya ubunge mahakamani!

Masamila

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2014
Posts
6,506
Reaction score
7,472
Ni baada ya kutiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja au faini mahakamani jana.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Excellence Attorneys Mwanasheria, Alex Mgongolwa akinukuu Katiba ya Tanzania Ibara ya 67 (1)(c); 67(2) (c na d) alisema hukumu hiyo haiwezi kumzuia kugombea ubunge kwa sababu hakwenda jela na kosa lake halihusu kukosa utovu wa uaminifu, kukwepa kodi wala kuvunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Hukumu hiyo iliibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii juu ya uwezekano wa kumzuia Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni kuwania tena ubunge au urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Anaendelea..Suala hilo linafanana na lililotokea katika mchakato wa uteuzi wa wagombea urais mwaka 2005 wakati aliyekuwa mgombea urais wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila na mgombea mwenza wake, Saidi Soud Said walipowekewa pingamizi kutokana na kutumikia kifungo jela, Mtikila akitumikia mwaka mmoja kwa kosa la uchochezi, Said akitumikia chuo cha mafunzo kwa kosa la biashara ya vitambaa. Hata hivyo, pingamizi hilo lilitupwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame (marehemu) baada ya kusikiliza utetezi wa Mtikila na Said, kuwa makosa waliyofungwa kwayo hayakuwa ya kukwepa kodi, kukosa uaminifu wala kukiuka maadili ya viongozi wa umma.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Ni baada ya kutiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja au faini mahakamani jana.
Wataalamu wa sheria watusaidie kulifafanua hili. Sheria inamzuia mtu aliyetumikia kifungo, sijui hapa kwa mtu aliyelipa faini inakuwaje!
cc: Petro Mselewa
 
alimshambulia wakala wa CCM baada ya kuiba kura uchaguzi uliopita.ila sio lazima awe mbunge
 
Sidhani kwa sababu mwka juzi mbunge wa Mbarali( CCM) alihukumiwa kifungo au faini kwa kumpiga mkt wa kijiji alilipa faini na anaendelea kuwa mbunge.
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ya 1977, kifungu cha 67(2)(c) kinasema;

67(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-

(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu;
Kwa kukusaidia zaidi, Katiba imeenda mbele zaidi kwenye kifungu cha 67(7)(b) na kusema,
''ikiwa mtu atapewa adhabu ya kufungwa gerezani ikifahamika kuwa adhabu hiyo ya kifungo imetolewa badala ya adhabu ya kutozwa faini au imetolewa kwa sababu mtu huyo ameshindwa kulipa faini aliyoamriwa kulipa, basi muda wa kifungo cha namna hiyo hautahesabiwa''.

Changanua hayo maelezo na ulinganishe na hakumu!
 
Baada ya mahakama ya Hai kumuhukumu Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe kifungo cha mwaka mmoja au kulipa milioni moja baada ya kumshambulia msimamizi wa kituo cha uchaguzi kwenye jimbo la hai, sasa inaonekana uamuzi huo wa mahakama umemnyima usingizi kwani utamnyima fursa ya kuchaguliwa kuwa ama mbunge au rais. Hivyo amekata rufaa mahakama kuu kupinga uamuzi huo.
 
Mh.Rage kipindi cha FAT alikula mvua kadhaa

Alishinda rufaa iliyofuta ile adhabu japo alikuwa amekwisha toka kwa msamaha wa rais. Sasa Mbowe aanze mchakato wa rufaa leo nadhani itasikilizwa August na maamuzi yatatoka January. UKAWA ingejipanga tu kumsimamisha mgombe mwingine hapo Hai na Mbowe akimshika mkono hata Mbuzi anashinda.
 
Precedence ya mtikila Yeye alienda jela 1 year kwa uchochezi. Hakuwa na faini. Na aligombe urais. What matters, kwa katiba ya sasa.. mtikila hakufungwa jela/ wala mbowe hakuhukumiwa kwa utovu wa uaminifu; kwa kukwepa kodi wala kwa kuvunja maadili ya viongozi wa umma. precedence ya mtikila kwa lugha nyepesi ilitengeneza sheria ambayo inabidi ifuatwe kisheria inaitwa case law
 
Ni baada ya kutiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja au faini mahakamani jana.
Hivi ww mbugila wapinzani wakifanya kosa basi ndy inakuwa mwimbo wa taifa.
nyie magamba chenge ali fanya nini?
ndomana mnachezewaga vichapo ila hamkomi
 
Pole mtoa mada kwa ujinga ulip nao na kutushirikish
 
Back
Top Bottom