Mbowe ameshakosa sifa ya ubunge mahakamani!

Mbowe ameshakosa sifa ya ubunge mahakamani!

Wataalamu wa sheria watusaidie kulifafanua hili. Sheria inamzuia mtu aliyetumikia kifungo, sijui hapa kwa mtu aliyelipa faini inakuwaje!
cc: Petro Mselewa

Kulipa faini ni sehemu ya kutumikia kifungo,ebu fikiria endapo angeshindwa kuilipa hiyo faini si angeishia magereza?
 
Nafikiri kuna maelezo mazuri tu ya kisheria yametolewa kufafanua kuwa Mbowe hazuiliwi kugombea ubunge kisheria. Hayo ya Chenge unayaleta bila sababu kwa maana hayana msaada wowote kwenye muktadha huu. Hukumu yake na muda wa kuchaguliwa vinapishana zaidi ya mwaka. Chill tu Mbowe atagombea ubunge.
kumbuka kuwa CCM ni wabishi wa kuzaliwa na wameanza kuleta udini kwamba aliyetandikwa makofi ni mwakilishi wa BAKWATA
 
kumbuka kuwa CCM ni wabishi wa kuzaliwa na wameanza kuleta udini kwamba aliyetandikwa makofi ni mwakilishi wa BAKWATA

Hayo hayana nafasi kwenye sheria , akichapwa padri au sheikh mbele ya uso wa sheria kachapwa binadamu.
 
Sheria inasema akifungwa gerezani.

Yeye hajafungwa,so nadhani anaweza kugombea.

.Nakubali kukosolewa kwa hili

Sio kufungwa gerezani bali ni KUHUKUMIWA kufungwa gerezani kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita. Haijalishi kama ataingia jela au la hata kama atalipa faini ya kiwango cha adhabu hiyo bado hana sifa. Kibaya zaidi hakukata rufaa bali amelipa faini fasta hilo ndio tatizo sasa.
 
Hivi ww mbugila wapinzani wakifanya kosa basi ndy inakuwa mwimbo wa taifa.
nyie magamba chenge ali fanya nini?
ndomana mnachezewaga vichapo ila hamkomi

Mbona makosa ya baadhi ya wana ccm walioleta kashfa za escrow ndio wimbo wenu wa taifa? kweli mkuki kwa nguruwe. Na tutalirudiarudia saana tu swala hili kwani sio la uongo.
 
Ni kwamba Mbowe hajapoteza sifa za kugombea ubunge kwasababu hajatumikia kifungo. Soma tena hapo juu,ni mpaka utumikie kifungo kisichopungua miezi 6 ndiyo utapoteza hiyo sifa.

Jamani ee hata kutoa faini ni kutumikia adhabu, mbona mnajitoa akili!! au kwa kuwa limemgusa chairman wenu!! acheni kujidhalilisha kutetea ma criminal.
 
Jamani ee hata kutoa faini ni kutumikia adhabu, mbona mnajitoa akili!! au kwa kuwa limemgusa chairman wenu!! acheni kujidhalilisha kutetea ma criminal.
Chenge alihukumiwa kufungwa miaka mitatu au kutoa faini, na alitoa faini, hakupoteza ubunge.

Soma hapa:
Hatima ya Ubunge wa Chenge baada ya hukumu

Kama sheria ilitekelezwa hivyo kwa Chenge, inapaswa kutekelezwa hivyo kwa wote.
 
Mbunge wa Tabora Mh. Hadeni Ragembona alifungwa jela kabisa na kisha baada ya hapo akachaguliwa kuwa Mbunge

Uwe unasoma michango ya wachangiaji post kabla hujakurupuka. Hilo limeshajibiwa kuwa alikata rufaa na alishinda rufaa yake.
 
Kama ni hivyo ni heri pia kwa afya ya demokrasia, Mbowe ni kiongozi thabiti na kwakweli busara zake zimesaidia sana kudhibiti mihemuko ya vijana wake hasa katika bunge hili.

Mbowe mwenyewe ana mihemko lini aliwahi kuzuia mihemko ya vijana wake zaidi alitangaza siku ya tarehe 11 OKT 2014 Siku ya kutotii sheria yaani civil disorder sasa hapo ndio kuzuia mihemko!?
 
Sio kufungwa gerezani bali ni KUHUKUMIWA kufungwa gerezani kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita. Haijalishi kama ataingia jela au la hata kama atalipa faini ya kiwango cha adhabu hiyo bado hana sifa. Kibaya zaidi hakukata rufaa bali amelipa faini fasta hilo ndio tatizo sasa.

hata kama asipokata rufaa bado ana sifa za kugombea urais au ubunge..kosa lililomtia hatiani halimzuii kugombea ubunge au urais kikatiba...
 
Hata asipokata rufaa bado hakuna sheria za kumzuia kugombea kwa kosa la kumkata makofi mtendaji mpuuzi. Kosa hilo halijaainishwa na Katiba yetu kama kosa la kumnyima mtu uongozi maana halihusiani na makosa ya rushwa au maadili.

Kama ni hivi chadema bado mna kazi ndefu sana ya kujitambua na kuthamini utu wa mtu, kwa tabia hii mtabaki kuwa chama cha upinzani milele.
 
Hili lilishatokea hapa Tanzania kwa Chenge:

Chenge alihukumiwa kufungwa au faini, na akalipa faini akaonekana hakupoteza sifa ya kuwa mbunge. Na hii ni December 2010, na tunavyoongea Chenge bado yu bungeni, na hakukata rufaa yoyote ile.
Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. Andrew Chenge ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za juu katika serikali ya Tanzania ikiwamo ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, leo alipona kutupwa jela miaka mitatu baada ya kulipa faini ya sh 700,000 katika kesi yake kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake wawili.

Hakimu Mfawidhi Kwey Rusema wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo.

Rusema alisema kutokana na ushahidi wa watu sita uliotolewa,mahakamani imemhuona na hatia ya makosa manne ambapo alimuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh 700,000.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rusema alisema kuwa,Mahakama imemkuta na katika makosa yote manne na kwa kosa la kwanza na la pili alitakiwa alipe faini ya sh 250,000 kwa kila kosa ambayo ni sawa na sh 500,000 au kwenda jela miaka miwili na katika shitaka la tatu na la nne alitakiwa kulipa faini ya sh 100,000 au kwenda jela mwaka mmoja.

Chenge alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake waWili,uharibifu wa mali na kuendesha gari bila kuwa na bima.
Picha Na Habari Kwa Hisani Ya Michuzi
Au tuthibitishe kuwa kuna sheria kwa viongozi wa CCM tofauti na kwa wengine?
 
Sio kufungwa gerezani bali ni KUHUKUMIWA kufungwa gerezani kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita. Haijalishi kama ataingia jela au la hata kama atalipa faini ya kiwango cha adhabu hiyo bado hana sifa. Kibaya zaidi hakukata rufaa bali amelipa faini fasta hilo ndio tatizo sasa.
Muwe mnaomba msaada kwa fani ambazo siyo zenu.

Hapa issue siyo kuhukumiwa au kufungwa bali atapoteza haki iwapo hukumu yake imesababishwa na makosa matatu,
1.utovu wa uaminifu
2.kukwepa kodi
3.kuvunja sheria ya Madili ya Viongozi wa Umma.

Mbowe hajahukumiwa kwa kosa lolote kati ya hayo kwa hiyo bado ana haki ya kugombea nafasi yeyote ile hata bila kukata rufaa.
 
Back
Top Bottom