Mbowe akiri kumkosea Zitto; Amuangukia!

Mbowe akiri kumkosea Zitto; Amuangukia!

WanaJF,

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwenyekiti wa CHADEMA, mhe Mbowe, amemuangukia Zitto na kueleza namna ambavyo yeye na chama chake wamemkosea Zitto wakati huo Zitto akiwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA.

Mbowe ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la Mwananchi na kueleza yafuatayo:

Source: Mwananchi

My take,

Baada ya madhambi ya CHADEMA kumuangukia Lowassa, sasa wameenda kumuangukia Zitto. Kwa sasa ni suala la muda tu kusubiri CHADEMA wamuangukie Dkt Slaa.

Nyumbu, kuweni makini na Mbowe. Mbowe hana adui wa kudumu. Anatazama maslahi yamekaa vipi, anabadilika fasta. Msiumize mishipa yenu kutukana watu halafu baadae viongozi wenu mnao wasujudu wanakuja kuwaomba msamaha hao mlio watukana. Mfano mzuri ni kwa Zitto na Lowassa.

Hivi ule ugonjwa wako hauponi tu? Wewe unaisujudu CCM ambayo inawadhalilisha watanzania kwa kutumbua majipu waliyoyasababisha. Huishii hapo umekomaa na Mbowe na CHADEMA badala ya kujadiri mema ya CCM (kama yapo).

1. Zito ni msaliti
2. Alijiondoa CHADEMA kwa kukiuka taratibu za chama
3. Kuondoka kwake kulisababishwa na CCM ambayo ameisaidia lakini haisadiki afanyaje?
4. Kamwe Zitio hana nafasi CHADEMA kama unayosema kweli anika barua ya kukubaliwa maombi ya chama chake ACT kujiunga na UKAWA.

Dawa ya mpuuzi kama wewe ni kupuuzwa
 
.....sioni cha ajabu wala mtu kumuangukia mwenzake .......sasa kwa mfano ulitaka mbowe popote atakapokutana na zitto ngumi zipigwe au!?!? yaani kuna watu wengine sijui huwa wana ubongo wa mbuzi!!
 
Hivi ni lini wanaccm watamsaidia Dr wetu Slaa asiikane nchi yake na kuwa mcanada? au sasa ccm wanamsaidiaje ili walau kanyumba kake kasiuzwe? au ndo toilet paper ukishalizana nayo tupilia mbali?
 
Ugomvi wa watoto mkiuingilia watu wazima mwishoni mtabaki kuumbuka tu,maana wao baada ya muda mfupi tu watasahau.
 
teeh barikiwa kwa jina la udaku/ haya bwana eti mbowe kumwangukia zzk daaah
mm najiamin mwenyewe simwamini mtu yeyote yule hasa wanasiasa maana naijua sana
 
hata hivo tunajifunza kua mwema nae anafaa kwa wakati wa wema na m'baya nae anafaa kwa wakati wa ubaya usishangae m'baya wa jana akawa mwema wa leo na mwema wa leo akawa m'baya wa kesho yamkin huenda ZZK alionesha usaliti akin kwa maslahi ya wakati huo sasa akawa amebadilika na kua mwema kwa maslahi ya sasa NI MTAZAMO TUU!!
 
Utapata shida sana maana tena inabidi mle matapishi yenu kama ilivyokuwa kwa Lowassa....mwenyekiti ndo kasema wewe utapingana na uamuzi wa m/kiti wenu?

Nadhani unayekula matapishi wewe mwenyewe.Hakuna UADUI kwenye siasa.Pole ukishalijua hilo utaishi kwa raha sana duniani hapa
 
Toka ZZK aandike kwenye ukurasa wa FB haya maneno na Mbowe kushindwa kujitetea, sina imani nao wote wawili, nawaona ni wezi, wanafiki na waongo kama walivyo wanasiasa wengi wa nchi hizi za Africa.

Kuna kipengele cha Chacha died, I won't, huwa kinaniachaga na maswali na ninatamani uchunguzi ungefanyika kwa kuanzia na haya maneno ya Zitto. Yeye na Mbowe wanajua nini walifanya kwa Chacha Wangwe, sijui lini Mungu atalipa ila atalipa tu.

Wote ni majambazi na ni Political Entrepreneurs!

Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. NaaminiMkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini.

Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.

Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?

Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda. Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.

They must know I am not a push over. Chacha died, I won't. Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili."
 
WanaJF,

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwenyekiti wa CHADEMA, mhe Mbowe, amemuangukia Zitto na kueleza namna ambavyo yeye na chama chake wamemkosea Zitto wakati huo Zitto akiwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA.

Mbowe ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la Mwananchi na kueleza yafuatayo:

Source: Mwananchi

My take,

Baada ya madhambi ya CHADEMA kumuangukia Lowassa, sasa wameenda kumuangukia Zitto. Kwa sasa ni suala la muda tu kusubiri CHADEMA wamuangukie Dkt Slaa.

Nyumbu, kuweni makini na Mbowe. Mbowe hana adui wa kudumu. Anatazama maslahi yamekaa vipi, anabadilika fasta. Msiumize mishipa yenu kutukana watu halafu baadae viongozi wenu mnao wasujudu wanakuja kuwaomba msamaha hao mlio watukana. Mfano mzuri ni kwa Zitto na Lowassa.
KUANGUKIA!!!!!!? Mimi sijaona kuangukia wala kuangukiwa hapa aliyo eleza yana balance kuna maumivu pande zote huo ndio ukweli Zitto alikosea na mahali fulani alikosewa,ila kwa watu wanao ongozwa na hisia wata yaweka wanavyo taka wao ili kufurahisha nyoyo zao,kwani waliopishana kauli wakipatana kuna dhambi gani?
 
Hili la kwamba kuna maumivu pande zote umelijua leo baada ya Mbowe kutoa kauli zake au ulilijua toka zamani? Kama mlijua toka mwanzo kuwa kuna maumivu pande zote kwanini msingesema tangu wakati ule, mkakomaa tu kumfukuza Zitto na kuyumbisha chama hali mkijua Mbowe na chama pia walikuwa na makosa?
 
If you want to destroy your enemy make him a friend
 
WanaJF,

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwenyekiti wa CHADEMA, mhe Mbowe, amemuangukia Zitto na kueleza namna ambavyo yeye na chama chake wamemkosea Zitto wakati huo Zitto akiwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA.

Mbowe ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la Mwananchi na kueleza yafuatayo:

Source: Mwananchi

My take,

Baada ya madhambi ya CHADEMA kumuangukia Lowassa, sasa wameenda kumuangukia Zitto. Kwa sasa ni suala la muda tu kusubiri CHADEMA wamuangukie Dkt Slaa.

Nyumbu, kuweni makini na Mbowe. Mbowe hana adui wa kudumu. Anatazama maslahi yamekaa vipi, anabadilika fasta. Msiumize mishipa yenu kutukana watu halafu baadae viongozi wenu mnao wasujudu wanakuja kuwaomba msamaha hao mlio watukana. Mfano mzuri ni kwa Zitto na Lowassa.
Ni mpaka uwe mtu usiyejifunza au kujua siasa ndio utakuwa na mawazo kama yako. Yakupasa ujue kuwa wanasiasa hawana uadui wa kudumu na pia hawana urafiki wa kudumu. Mifano ni mingi sana. Wassira alitoka CCM akaenda NCCR na wakati huo alisema CCM ina UKIMWI. Baadaye alirudi akawa mbunge kupitia CCM hadi kuwa waziri. Historia haijafutika pia kuwa mwaka 2005 JK alitaka kuingia kugombea kupitia CHADEMA kama CCM wangemkata. Wakati huo mtarajiwa alikuwa Salim A. Saluim. Mkapa akaogopa wakampitisha. Tambwe Hizza aliwahi kusema kurudi CCM kwake itakuwa sawa na kulala na mama yake. Lakini aliingia CCM na sasa ametoka tena yuko CHADEMA. Wako akina Kingunge, Lowassa, na wengine wengi tu. Hata Cuba na Marekani wamekuwa maadui muda mrefu lakini sasa wanapatana. Usitake kufanya jambo hilo kuwa ni issue kubwaaaa!
 
sasa hapa sie 'nyumbu' tutaficha wapi sura zetu?. zitto tumemtukana sana kuwa ni msaliti...halafu mwenyekiti anabadilisha gia angani kwa kufanya kazi na zitto...hii sio haki basi tumrudishe dr slaa
 
  • Thanks
Reactions: nao
wewe una akaili kama za Lusinde, una tofauti na iddi amini kwa sababu muda wote kwako ni uadui, vita, hata nyerere aliwasamehe wakina Babu, kambona hata walitaka kumpindua, mbona kaburuu yuko kwenu, mbona JPM ameende kumtembelea Sumaye Hospitalini, pia mbona Majaliwa alikutana na kusalimiana na lowasa, siasa sio uadui hayo yote ni kwa ajili ya wananchi, HAMDY huna tofauti na yule jamaa wa kimwani aliyemtuma muuaji amuue Diwani aliyempiga chini kwa kitita cha tshs mil. 1
 
WAtu hawakumwelewa Mbowe; watu hawamuelewi Mbowe; watu hawatamwelewa Mbowe. Endeleeni kuimba kila wimbo anaouanzisha. Mwaka jana alianzisha MABADILIKOOO----LOWASAAAA; LOWASAAA------MABADILIKOOO! Sote tuliimba.
 
WanaJF,

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwenyekiti wa CHADEMA, mhe Mbowe, amemuangukia Zitto na kueleza namna ambavyo yeye na chama chake wamemkosea Zitto wakati huo Zitto akiwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA.

Mbowe ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la Mwananchi na kueleza yafuatayo:

Source: Mwananchi

My take,

Baada ya madhambi ya CHADEMA kumuangukia Lowassa, sasa wameenda kumuangukia Zitto. Kwa sasa ni suala la muda tu kusubiri CHADEMA wamuangukie Dkt Slaa.

Nyumbu, kuweni makini na Mbowe. Mbowe hana adui wa kudumu. Anatazama maslahi yamekaa vipi, anabadilika fasta. Msiumize mishipa yenu kutukana watu halafu baadae viongozi wenu mnao wasujudu wanakuja kuwaomba msamaha hao mlio watukana. Mfano mzuri ni kwa Zitto na Lowassa.

Umeandika uongo: Mbowe amezungumza in general hataja nani kamkosea mwenzake ila amejaribu kusema tu kwamba si kila wakati unatengana na mtu ambaye mulikuwa na migongano. kuna wakati lazima muwe wote akawataja hata CCM huungana kwa baadhi ya mambo hii ndio mantiki ya Mbowe. umepotosha sana kwenye Tittle yako.
 
Mbona sioni alipomuangukia??? Ungeleta hata picha jinsi mbowe alivyomuangukia zitto gamba wewe
 
Hili la kwamba kuna maumivu pande zote umelijua leo baada ya Mbowe kutoa kauli zake au ulilijua toka zamani? Kama mlijua toka mwanzo kuwa kuna maumivu pande zote kwanini msingesema tangu wakati ule, mkakomaa tu kumfukuza Zitto na kuyumbisha chama hali mkijua Mbowe na chama pia walikuwa na makosa?
Uki eleza kuwa MLIJUA una kosea maana niko neutral kupitiliza ninacho jua wote walilalamika na kulaumiana na kwa kuwa yali baki hivyo bila kuwapo kushitakiana kwa hekima japo ndogo utasema walikosana kwa kuwa hakuna hukumu na sisi wa nje hatumjui mkosaji na aliye kosewa sijui wewe kwa upeo wako una yatazamaje unge bahatika kusoma kitabu Cha The merchants of venice alicho tafsiri Mwl.Nyerere kama Mabepari wa Venice juu ya kuhukumu mambo hata kama si hakimu ungenielewa vizuri tu.
 
Back
Top Bottom