Ndugu zangu,
Tuseme tu ukweli hakuna mfuasi yeyote wa Chadema mwenye akili hata asilimia moja ya alionayo Mbowe.
Mbowe hutoa hela zake mfukoni ili kukiendesha chama, yaani ni mwenye upendo wa hali ya juu.
Nimewaangalia kwa makini wafuasi wote wa chadema hawana uchungu na chadema kama Mbowe. Mara kadhaa Mbowe ameicha familia yake analala ofisini kuhakikisha Chadema insonga mbele.
Mshahara na marupurupu ya Mbowe wote unaingia kwenye mfuko wa kuendesha Chama kwa kifupi jamaa anajitolea kila senti yake kuhakikisha chama kinaendelea.
Baada ya chadema kukosa watu wa kugombea uenyekiti Mbowe akajitolea tena na hapa ikabidi ukomo wa uenyekiti uondolewe ili aendelee kujitolea kazi ambayo wengi hawawezi na wamemuachia mzigo mzito.
Mbowe ndiye mwenye ''connections' na CCM na makada wake kwani kipindi cha uchaguzi hukodisha wagombea ili kupaisha ruzuku ya chama, ni mwenye maono hususani kuendesha chama kwa mfumo wa kampuni.
Hayo ni machache unaweza kuongeza mengine; kwa hali ilivyo hakuna mwanachadema hata mmoja anayewezq kufanya hata jambo moja nililoorodhesha hapo juu, nasema hakuna mwanachadema hata mmoja mwenye kuipenda Chadema kama Mbowe, zaidi wafuasi wote wa Chadema ni wapitaji ila Mbowe tu ndiye wakudumu asiye na tamaa ya kwenda popote.
Nimeongea kwa sauti kubwa ili wote msikie, natumaini mmenielewa, mwenye kupinga haya ajenge hoja na si kumshambulia mleta hoja.