Mbowe aiuza CHADEMA kwa Lowassa

Mbowe aiuza CHADEMA kwa Lowassa

Kwa upande mmoja sitaki kuamini kwamba Mbowe anaweza kukubali kujichimbia kaburi la kisiasa kwa kukubali kupokea vipande thelathini vya shaba. Hata hivyo, nikijua jinsi hawa jamaa walivyo na mbinu na kiu ya kujaribu kununua kila mtu, siondoi uwezekano wa hili kutokea na kwa hili nakubaliana na analysis ya Banyimwa.

Sitaki pia kumuondoa Zitto katika hili kwani ukaribu wa Zitto na hawa mafsadi ni mkubwa kuliko hata ule wa Mbowe na mafisadi. Nakumbuka alivyopigia debe Dowans na baadae Mwanahalisi kumuanika.

Kwa hiyo CDM wachunge hili na kulifuatilia kwa kina lakini vile vile huyu Zitto ni wa kumuangalia zaidi maana ilisemwa humu kwamba much as anaipenda sana CDM, lakini anaipenda sana pesa kuliko CDM.
Keshajichimbia kaburi
 
chadema wana malengo yao makini hata iweje 2015 wanashika dora. Huo ni mpango ndani ya makundi ya ccm kumchafua EL ili wamweke mtu wao na hata hvyo hawataweza kamwe..! Kwani 2015 ni cdm tu.
HahahahahahahHHHH
 
Habari hii inaweza ya kupikwa lakini imepikwa kwenye mazingira yanayoelekea kuwa kweli:
Tanzania Daima kumpamba ENL
Mbowe yupo kibiashara zaidi
Mbowe hajawahi kumsifia/kumpamba Dr. Slaa hata siku moja (fuatilia), maana yake hapendezewi naye jinsi alivyo moto kwa mafisadi
Mbowe hawajawahi kutoa kauli yoyote ya kumlaani/kumsema ENL au RA

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Old is Gold
 
Kama chama kizima kilinunuliwa wanashangazwa na nini kuhusu kununuliwa kwa Mtatiro.
 
Kuna mpango wa Mwenyekiti wa Chadema Mh.Freeman Mbowe wa kulipwa mamilioni ya fedha ili Viongozi wa Chadema waache kumsema Mr. Monduli kuwa ni fisadi.

Mhe. Zitto Kabwe anajitahidi kwa kila hali kuzuia mpango huo.
=============

Mmoja kati ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi(jina tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya siri na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Freeman Mbowe ili kuingia ubia na chama hicho.

Inaelezwa kuwa ,lengo la kigogo huyo ni kukiziba mdomo chama hicho kisimrushie makombora ya ufisadi kama walivyowahi kumrushia siku za nyuma.

Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili kwa muda mrefu sasa umebaini kuwa kigogo huyo wa CCM amekuwa na mawasiliano ya siri na ya karibu na Mbowe huku vikao vingi vikifanyika ndani ya hoteli moja ya kitalii iliyopo jijini Arusha (jina tunalo)

Imebainika kuwa ndoa hiyo ya siri ni ya wanasiasa hao wawili,lakini ikilenga uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kigogo huyo wa CCM amemuahidi Mbowe kwamba wataunda "serikali ya umoja wa kitaifa" endapo Mbowe atasaidia kuacha kumuandama kwa tuhuma za ufisadi na kuwadhibiti viongozi wengine wa chama chake, kutofanya hivyo kwenye maandamano na mikutano yao ya hadhara, pamoja na kwenye mahojiano na vyombo vya habari.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa tayari kigogo huyo amempa mwenyekiti huyo wa CHADEMA kiasi kikubwa cha fedha ili chama hicho kinapoendelea na kampeni yake ya bomoa-bomoa mafisadi yeye asiguswe kabisa, kama hatua ya kumfikisha ndoto yake ya kutaka chama tawala kumteua kuwa mgombea wa nafasi ya urais.

Chanzo chetu cha uhakika kikiongea na Sauti Huru kwa sharti la kufichwa jina lake kimedai " huu mpango unafanywa kwa siri kubwa na ninajua hata mhusika (anamtaja) akijua habari hii imetoka atafadhaika sana"


Habari zaidi zinadai kwamba kigogo huyo amefikia hatua hiyo baada ya kusoma alama za nyakati na kuona kwamba uwezekano wa mwenyekiti wa chama chake kumuunga mkono ni mdogo, hivyo hatoweza kupenya katika kinyang'anyiro cha uraisi 2015.

" Huyu bwana amesoma alama za nyakati ,ameona kabisa uwezekano wa kuungwa mkono na mwenyekiti wake(wa CCM) ni mdogo sana hivyo ni lazima atafute njia nyingine hata kama njia hiyo itakuwa na madhara kwa chama chake", kilieleza chanzo hicho na kufafanua;

"Si kwamba hajui mwenyekiti atalalia wapi, anajua lakini yuko tayari hata kukisaliti chama ili wote wakose,hivi ninavyoongea nanyi watu hawa wana mawasiliano ya kila mara juu ya suala hili ila Mbowe kaweka ngumu kuwa lazima waandikishiane ajue kabisa endapo (kigogo huyo atafanikiwa kuingia madarakani basi wataunda government of unity(serikali ya umoja wa kitaifa)".


...Aidha imefafanuliwa kwamba habari hizi zimeweza kumgusa hata Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, lakini kwa namna ya pekee Zitto ameweza kudhoofisha mkakati huo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni 'unafiki kwa Mbowe'


"Mtakumbuka siku za hivi karibuni Zitto alishutumiwa na chama chake kwa madai ya kuwa na uhusiano wa mashaka na Idara ya Usalama wa Taifa. Chadema wamekuwa wakidai kwamba Zitto anatoa siri za chama chao nje na hata kumuundia kamati ya wazee kumshauri?" alihoji.

Aliendelea:" Kilichotokea katika kamati hiyo siku walipokutana na Zitto ilikuwa tofauti kabisa, Zitto akawabadilishia mada pale alipowaambia wazee,'jamani ugomvi wangu na Mbowe ni pesa za chama, anatumia chama hiki hiki kupata fedha toka nje ya nchi na ndani ya nchi, lakini ninapojaribu kumkosoa kuwa tabia hiyo si nzuri kwa mwenyekiti wa chama ananijia juu,nyie mnajua kuwa amepokea fedha mamilioni kutoka kwa(anamtaja kigogo huyo) kwa ajili ya kutunyamazisha tusipige kelele za ufisadi dhidi yake?' "

"Hivi hamjui tayari anafanya mazungumzo na mtu wa CCM kwa ajili ya power sharing ya mwaka 2015?"

Kwa mujibu wa habari hiyo ni kwamba kigogo huyo atafanya kila liwezekanalo CCM imteue kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi; lakini anajua hilo litawezekana endapo kelele za ufisadi dhidi yake zitamalizika.

"Huyu mtu ni mjanja sana na kwa sasa ana nguvu na mtandao mkubwa ndani ya CCM unaoweza kumfanya ateuliwe na chama kuwa mgombea, si hilo tu anajaribu hata kutafuta nguvu nje ya nchi ili endapo akikataliwa aweze kuwa na cha kuieleza jumuiya za kimataifa,"

"Na kwa hatua aliyofikia ni kwamba endapo hatoteuliwa hasa kutokana na ufisadi wake,yuko tayari hata chama chake kipoteze nafasi ya uraisi kitu ambacho kinaonyesha kuwa hana sifa za kiuongozi isipokuwa ni tamaa ya utawala."

Source: Gazeti la Sauti Huru

My Take:
Wale viongozi wa Chadema na wakereketwa waliopo humu JF watuthibitishie hii habari kama ni kweli.
Hili linaitwa kaburi MUJARABU.

Kila kitu kitafahamika tu.

Ni suala la muda tu kabla haijafahamika hao wanaoitwa "wasiojulikana" ambao wanadhuru Wanachadema wanaoonyesha kutofautiana na Mwenyekiti wa chama, wanatumwa na nani.

R.I.P Chacha Zakayo Wangwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili linaitwa kaburi MUJARABU.

Kila kitu kitafahamika tu.

Ni suala la muda tu kabla haijafahamika hao wanaoitwa "wasiojulikana" ambao wanadhuru Wanachadema wanaoonyesha kutofautiana na Mwenyekiti wa chama, wanatumwa na nani.

R.I.P Chacha Zakayo Wangwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukweli huwa haujifichi
 
Kama kila anayeihama CDM kanunuliwa then inashindikanaje mtu kukinunua chama kizima maanake wote mnatembea na price tag shingoni sasa na chama ni mali ya kikundi kidogo tu wengine wapiga vinubi tu.
 
Mnajaribu kumpamba Zitto aonekane malaika???? upuuzi mtupu leteni habari za maana watu tujadili, kutuletea habari kama japo mtu anatumia demokrasia, lakini ikumbukwe kuwa ni uharifu wa rasilimali, muda na akili na utayari wa watu katika kushiriki kuchangia mambo.....mtatumia misuli sana kumpamba Zitto bila mafanikio mwenzenu kila kukica anaoga matope kwa hiari yake.

Kuhusu CDM NA mbowe HOJA ZILIZOTUMIKA NI UPUUZI MTUPU WAANDIKISHIANE HALAFU WAKIGEUKIANA WAKSHITAKIANE WAPI LABDA KAMA MNGESEMA WAMEENDA KWA MGANGA KUNCHANJIANA DAMU (KULA YAMINI)
Watu kama Wewe sijui huwa mnatoa wapi UKAUZU wa kuingia humu JF na kuendelea kuchangia mijadala kwa kutukana na kukejeli watu!?
Jifunze kuweka AKIBA YA MANENO.
Miaka 7 baadae unakula matapishi yako kwa kumuita ZItto SHUJAA. Wakati huko nyuma ulikuwa tofauti na nafsi yako mwenyewe.
Ama kweli kuwa uyaone!
 
Hili linaitwa kaburi MUJARABU.

Kila kitu kitafahamika tu.

Ni suala la muda tu kabla haijafahamika hao wanaoitwa "wasiojulikana" ambao wanadhuru Wanachadema wanaoonyesha kutofautiana na Mwenyekiti wa chama, wanatumwa na nani.

R.I.P Chacha Zakayo Wangwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnooooooo!
Only Time Will Tell. Kwa hakika ipo siku ukweli utakuwa Upenuni na kuna watu humu wataanguka kwa presha siku hiyo.
 
Ndio maana tulivyoona michezo ile 2015 plus tetesi zilizokuwa zinazunguka ukiwemo uzi huu wengine ikabidi tuwe wapole tu na kujitenga na usanii ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu kama Wewe sijui huwa mnatoa wapi UKAUZU wa kuingia humu JF na kuendelea kuchangia mijadala kwa kutukana na kukejeli watu!?
Jifunze kuweka AKIBA YA MANENO.
Miaka 7 baadae unakula matapishi yako kwa kumuita ZItto SHUJAA. Wakati huko nyuma ulikuwa tofauti na nafsi yako mwenyewe.
Ama kweli kuwa uyaone!
Uwe unaangalia watu wa kuwajibu kwa upuuzi wa hoja zako nyepesi, wapi nilipomuita zitto shujaa? Huwa mimi si kati ya wale walambao matapishi unasikia wewe?
Miaka 7 baaadaye ni wapi umeona msimamo wangu ukibadirika au unafananisha na kukariri watu?
Na hata ingetokea nimemsifu Zitto kwa hoja fulani aliyoitoa hiyo haimaanishi kuwa ni kubadili misingi.
Tafuta watoto wenzako ubishane nao, maana mimi unayenijaribu siyo shabiki wa mtu wala huwa sina upande pale ninapojadili jambo au ninapo simamia misingi.
Huwezi ukanielewa kiwepesi hivyo. Jaribu unisome vizuri labda itakusaidia.
 
Mkuu Nickname

Hii taarifa ilipotoka mara ya kwanza wasomaji wengi waliipuuza. Wakaipa majina mabaya. Wasomaji wachache walizingatia. Wakatoa maangalizo. Ambayo yalipuuzwa pia.

Tatizo halikuwa taarifa, wala mtoa taarifa. Tatizo ni sisi Watanzania wenyewe. Proportion kubwa ya Watanzania hata wanaopita humu JF sio watu wa kuchambua na kupembua taarifa kwa uyakinifu. Ndiposa ni rahisi sana kuzolewa na viroja badala ya kutohoa maudhui ya hoja na hojaji.

Faida kubwa tuliyonayo humu JF ni uwepo wa proportion ndogo ya Watanzania wenzetu ambao mboni zao zinaona mengi ambayo wengi hawayaoni. Kwa hekima za wachache hawa, mara zote huwa wanatuasa. Ni vile tu baada ya kutoa maangalizo, hawatulazmishi kufuata maono yao. Hii ndio hulka yao. Hawatumii mabavu kufikisha ujumbe ama wa heri ama wa hatari kadri ya ufahamu wao.

Bila shaka wakati umefika, Watanzania wenzangu tubadili namna tunavyopokea taarifa. Waamini wanafahamu imeandikwa: "yapimeni maandiko". Neno hili linamaanisha uwepo wa vipimo vya kupima maandiko. Swali ni ikiwa Watanzania tunatumia vipimo sahihi kupima relevancy, reliability, validity na credibility hasa ya maandiko. Badala ya kupoteza wasaa kumpima mwandishi. Maana ni wazi haisaidii sana kumpima Mwandishi.
Respect mkuu!
Ulichoandika katika Uzi huu Dec 2016, ndio kitu ambacho kila mara huwa najaribu kuwaasa watu humu JF. UONGO, Unafiki, Uzandiki, Ufitini, Undumi la Kuwili, Ndimimbili n.k ni HATARI sana katika jamii yetu watanzania.
Leo hii 2018 mambo hayo yameshika kasi kubwa katika mitandao.
Halafu tunashangaa Sheria mpya za matumizi ya mitandao zikizaliwa. Ni kwa sababu hatuna nidhamu katika matumizi ya mitandao na kuheshimu Maoni na Hoja za watu wenye maoni tofauti.
Muda ni Mwalimu nguli.
 
Uwe unaangalia watu wa kuwajibu kwa upuuzi wa hoja zako nyepesi, wapi nilipomuita zitto shujaa? Huwa mimi si kati ya wale walambao matapishi unasikia wewe?
Miaka 7 baaadaye ni wapi umeona msimamo wangu ukibadirika au unafananisha na kukariri watu?
Na hata ingetokea nimemsifu Zitto kwa hoja fulani aliyoitoa hiyo haimaanishi kuwa ni kubadili misingi.
Tafuta watoto wenzako ubishane nao, maana mimi unayenijaribu siyo shabiki wa mtu wala huwa sina upande pale ninapojadili jambo au ninapo simamia misingi.
Huwezi ukanielewa kiwepesi hivyo. Jaribu unisome vizuri labda itakusaidia.
Hahahahaha....Just Hahahahaha. How You like Zitto Now!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom