Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Huyu Fisrt lady wa mwanakjj hata nywele hana ndio maana Mbowe yuko na kina GRACE KIWELU.

inaoekana jinsi huyu mama anavyoijua pesa na wagonjwa wa muhimbili atakuwa anawachukua Figo na kwenda kuziuza India.
mtizame alivyotoa macho kama mjusi.

http://www.newhabari.com/mtanzania/

Admin nadhani kuna haja ya kuweka utaratibu kudhibiti watu wanaotumia lugha za kudhalilishana kama hizi. cdhani kama kulikuwa na sababu yoyote ya kutumia lugha hiyo na pia hapa hatujadili muonekano wa mtu. Hili linaweza haribu reputation ya JF ambayo imetuchukua muda na gharama kuijenga.
Naomba tusikubali watu wachache ambao naweza sema "wametumwa" kuiharibu heshima nzima ya JF kwa kutumia lugha ambazo zitatoa taswira tofauti kwa wasomaji zaidi ya mamilioni wa JF.
Lets not allow some few "mamlukis" to ruin our reputation and make us seen as Tovuti ya Udaku na majungu
 
Maswala ya Grace Kiwelu yapo humu sikuyaleta mimi. kwanini iwe udaku na Chadema nzima wanajua suala hili.

hivi kuna kipengele gani kinasema kuwa JF ina heshima kubwa?

heshima hiyo inatuzuia kuwataja wizi wa mfuko wa pensioners?

dawa ya deni kulipa tu iwe sumni ni mali ya umma,iwe shilingi kumi lipeni kwanza halafu ndio mseme fulani hajalipa.

anachokifanya Mbowe ni kutaja na fulani nae mwizi sio pekee yake.
Lowassa hakumtaja mtu alikufa kivyake na MBOWE arudishe tu si mjadala.

na mbowe ndio aliyemdhalilisha dada Liliani hadi kupelekwa mahakamani kama ana muheshimu mkewe angelipa deni.
 
Admin nadhani kuna haja ya kuweka utaratibu kudhibiti watu wanaotumia lugha za kudhalilishana kama hizi. cdhani kama kulikuwa na sababu yoyote ya kutumia lugha hiyo na pia hapa hatujadili muonekano wa mtu. Hili linaweza haribu reputation ya JF ambayo imetuchukua muda na gharama kuijenga.
Naomba tusikubali watu wachache ambao naweza sema "wametumwa" kuiharibu heshima nzima ya JF kwa kutumia lugha ambazo zitatoa taswira tofauti kwa wasomaji zaidi ya mamilioni wa JF.
Lets not allow some few "mamlukis" to ruin our reputation and make us seen as Tovuti ya Udaku na majungu

Muonekano wa mtu ningesema kuwa LILIAN MTEI ana kipara kama mwanaume na lip stick aliyoweka utafikiri kala nyama na hana sura ya kuwa Fisrt lady,au ukitiza picha hiyo utajua wote wawili ni wanaume, lakini mimi sikusema hayo.
unanionea bwana mkubwa.
 
Mie sina chama, lakini kushindwa kulipa kwa aliyechukua mkopo bank si kitu cha ajabu na kinatokea katika kila kona ya dunia, bank wanaweza kumfilisi mali zake ili wafidie deni lao. Je, na huyu fisadi Mkapa aliyejichukulia Kiwira Coal Mining bila hata kuwaambia Watanzania na kujifanya ni ya kwake na kisha kuwashinikiza TANESCO waingie naye mkataba wa shilingi 326 bilioni hamuoni ufisadi wake! Duh! Ama kweli ukistaajabu ya hayawani utaona ya taahira!

Bubu ataka kusema,

Huko duniani unakokusema, ukifilisiwa unapoteza uongozi wa siasa hapo hapo. Mbowe hapa hajadiliwi kama mfanyabiashara mwingine yeyote. Ni mfanyabiashara na pia kiongozi wa chama.

Nchi za wenzetu unazozisema, kwa Mbowe kushindwa tu kulipa hilo deni, tena la mfuko wa watu maskini, wastaafu, leo asingelikuwa mwenyekiti wa chama. Lakini kwa Tanzania hawa wanasiasa wanajiona wako juu ya sheria.

Hakuna kosa dogo au kubwa, lazima yote tuyapinge tu. Huwezi kusema hili kosa dogo, tukae kimya mpaka tumalize kushughulikia makosa makubwa. JF lazima ilaani makosa ya aina zote. Huyo anafanya hayo makosa madogo kwasababu hajapata chance ya kufanya makosa makubwa. Ukimkabidhi Ikulu, ndio unajua ni fisadi mkubwa.

Watu tulipiga kelele miaka na miaka kuhusu Mkapa kuitwa Clean, watu wakasema tunamsingizia, leo kila mtu anajua ukweli.
 
Mtanzania, kama hakuwa na uwezo wa kulipa ndani ya miaka sita ni kitu cha ajabu kabisa kutokea duniani? Kama kushindwa kulipa mkopo wa kibiashara ndani ya muda ni jambo ambalo halijawahi kusikika duniani miye nakubali!! alipe! Lakini kama hiki ndicho kipimo siku hizi basi tuanze sasa kuwataja wabunge wote na wanasiasa wote ambao wana madeni ambayo wameshindwa kulipa ndani ya muda uliotakiwa.

Mkisema kuwa kati ya viongozi wote wa kisiasa Tanzania ni Mbowe peke yake miye nitakubali, itakuwaje mtu "mmoja" ashindwe kabisa kulipa deni kama hilo. Sasa kinadharia niko upande wenu kabisa, lakini wangapi wetu hapa tuna madeni kwenye mabenki na credit cards ambayo tunayalipia miezi nenda miezi rudi!? Wale ambao hamna deni hata moja nyinyi ndio mnatakiwa muongoze nchi.

Lakini katika ulimwengu halisia watu wana madeni, watu wanafanya makosa, na watu wanajifunza kutokana na makosa hayo. Kama vile watu walivyopima kipimo kwa Zitto kuhusu Amina tukawakatalia, na hapa nawaasa tena, kipimo mnachotaka kukitumia kwa Mbowe muwe tayari kukitumia kwa wengine and believe me wapo na wanajulikana. That is all I'm saying, isije kuwa kitakapoanza kuinuliwa kwa kina Mwakyembe, Selelii, Mzindakaya, na wengine ambao kwa wengine ni mashujaa tusianze kutafuta udhuru.

Mwanakijiji,

Kushindwa kulipa deni ontime sio kitu cha ajabu lakini kushindwa mpaka kupelekwa mahakamani, tena sio mara moja, hicho ni kitu cha ajabu, hasa mhusika anapokuwa mwanasiasa na mkopeshaji anapokuwa mfuko wa watu maskini ambao wanahangaika kila siku kupata haki zao.

Ninaamini case hii ya Mbowe ingelikuwa West, leo asingelikuwa kiongozi wa CHADEMA full stop.

Lakini sisi Wadanganyika, tumejaa ushabiki wa kisiasa hata kwenye mambo yanayoathiri maendeleo ya nchi yetu, leo tunakuja hapa kuhalalisha ujinga huu.
 
Zito na Team yote ya Chademn waliambatana na Mbowe akiwa mkewe alipokuwa akijetea!lakini akina Mwankijiji na wenzie wa JF hatukuwaona au walikuwa nyuma ya camera!

Masha mwingine huyo! Mambo ya deni lake na uongozi wa CHADEMA vina uhusiano gani? Mtu makini kama Dr. Slaa naona akaamua kuingia mitini. Hata mimi ningelikuwa kiongozi wa CHADEMA nisingeenda kwenye mkutano kama huo.
 
Huyu Fisrt lady wa mwanakjj hata nywele hana ndio maana Mbowe yuko na kina GRACE KIWELU.

inaoekana jinsi huyu mama anavyoijua pesa na wagonjwa wa muhimbili atakuwa anawachukua Figo na kwenda kuziuza India.
mtizame alivyotoa macho kama mjusi.

http://www.newhabari.com/mtanzania/
HIYO SIO HOJA TUNAYOJADILI HAPA,USISABABISHE WAUNGWANA HAPA JF WAKUONE MWEHU KWA KUVURUGA MAJADILIANO YANAYOENDA KISTAARABU KAMA ILIVYO DESTURI YA JF.HAPA KUNA WATU MAKINI AMBAO MICHANGO YAO IMESAIDIA SANA MUSTAKABALI WA NCHI YETU. KULETA MAMBO YA KIPUUZI NI UJINGA AMBAO HAUVUMILIKI,KAMA HUNA CHA KUCHANGIA KWANI HUWEZI KUKAA KIMYA?
ALIYEKUTUMA KUJA KUVURUGA(KAMA YUPO) ASHINDWE NA ALEGEE !
 
Naona ningekusaidia hesabu kidogo.... ila sio vizuri kuwaambia watu wakauze mtori......

Shs 15m kama haikulipwa even a single installment, taking interest rate to be 20% (which is on a higher side kwa loan ya NSSF) compounding it for the 18 years inakuwa hivi Shs 399,349,999 ie Shs 15,0000*(1+0.2)^18.

Lakini kabla ya kufikia kiasi hicho inatakiwa tujue hiyo milioni 75 ililipwa lini, coz hiyo balance ingepungua, na unaweza ukakuta Mbowe ndo anayeidai NSSF (the big issue ni timing tu..when did they pay NSSF?)

TechMaro,

Unajua inaudhi sana unapoona mtu ambaye hajui kitu juu ya mikopo, interests na risks vinavyofanya kazi, anakuja na mahesabu yake uchwara.

Mkuu, mikopo haiendeshwi kwa namna hiyo. Kama hujui sema hujui, omba course ndogo ya finance na utaelewa, vinginevyo omba wana JF hapa wakusaidie.

Masuala ya mikopo yanafuata mambo mengi sana. Lililo kubwa ni risk ya mhusika. Ndio maana machinga akienda kukopa napewa interest 30 wakati shirika likienda linapewa 10%.

Ukishindwa kulipa mkopo hata mara moja, kwenye mkataba kunakuwa na clauses kibao ambazo zinatoa penalties mbalimbali.

Kuongelea mambo ya compound interest kwenye hili ni ukilaza. Hapa ongelea mtu kushindwa kutimiza masharti yaliyoko kwenye mkataba wake na hivyo kujikuta deni dogo linakuwa kubwa mno.

Tafuta hata kwenye internet, hapa kuna familia walikopa 4,000 pounds na haijapita hata miaka kumi, walijikuta wanadaiwa zaidi ya pounds laki moja, Hiyo ni UK ambayo sheria zake ziko wazi kabisa kuliko TZ. Tatizo ni hilo la kukiuka mkataba. Ikabidi watangaze kufilisika na kupoteza kila walichokuwa nacho.

Kila ukisoma case ya Mbowe inaonyesha mara nyingi tu alishindwa kulipa ontime. Kitu ambacho unatakiwa mtu kufanya ni kwamba hata ikitokea hivyo basi ni kuamkia bank na kuongea nao juu ya matatizo uliyopata, ili zile penalties zisifanye kazi. Lakini ukijikalia nyumbani, deni dogo utakuta limekuwa mabilioni.
 
na Salehe Mohamed

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema watu wanaotaka kumtisha kwa kutumia deni lenye utata ambalo moja ya kampuni zake ilikopa miaka 18 iliyopita, wanajidanganya na kamwe hawawezi kusababisha akatetereka.

Mbowe alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wanahabari kujibu tuhuma dhidi yake zilizoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari wiki iliyopita, vikimhusisha yeye na wakurugenzi wenzake wa wa Mbowe Hotels Ltd, kukwepa kulipa deni alilokopa kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mwaka 1990.

Alisema ukiangalia kwa makini habari hiyo ambayo kwa mara ya kwanza iliandikwa katika gazeti la kila wiki la ‘Rai’ linalochapishwa kila Alhamisi, utaona dhahiri kuwapo kwa mkakati wa makusudi wa kundi fulani la watu ambao hakuwataja wanaolenga kumchafua na kumpaka matope wakitumia mzozo wake wa kibiashara na NSSF.

“Ninaamini kwamba habari hizi zinakuja leo hii, si kwa bahati mbaya au kwa sababu ni habari muhimu na za kulisaidia taifa hili. Kwa hakika habari hizi zinalenga kuzima moto tuliowasha dhidi ya mafisadi wa EPA, Richmond, Buzwagi na wale wote wanaotafuna rasilimali za taifa hili. Ni wazi kwamba taarifa hizi zinakusudia kupotosha mwenendo mzima wa namna wapinzani na hususan CHADEMA tunavyotaka serikali iwashughulikie wezi wa EPA na wale wa Richmond.

“Watu hawa wenye nia mbaya na taifa hili, kwa makusudi mazima wameamua kuvitumia vyombo vya habari kutimiza malengo yao maovu ya kuzima uzalendo wetu juu ya rasilimali za Tanzania na mapambano yetu dhidi ya ufisadi,” alisema Mbowe.

Akitoa ufafanuzi kuhusu deni hilo la hoteli yake, Mbowe aliyekuwa ameongozana na mkewe, Dk. Lillian Mtei, ambaye pia ni mkurugenzi wa Mbowe Hotels Ltd, alikiri kukopa shilingi milioni 15 kutoka iliyokuwa NPF (sasa NSSF) mwaka 1990, kwa ajili ya kuendeleza mradi wake wa hoteli hiyo kama mjasiriamali.

Alisema hadi kufikia hivi sasa, hoteli yake hiyo tayari imelipa kiasi cha shilingi milioni 75, kiasi ambacho ni mara tano ya deni la msingi alilokopa na hivyo utata uliobaki sasa ni riba inayotokana na deni hilo.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA, ambaye katika mkutano huo alikuwa ameandamana pia na uongozi takriban wote wa juu wa chama hicho ukimuacha Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, alisema hesabu walizokokotoa kwa kuzingatia utaalamu wa kisheria na kihasibu, zinaonyesha kuwa kiasi cha deni kilichobaki kulipwa hadi hivi sasa hakiwezi kuzidi shilingi milioni 43 na si shilingi bilioni 1.2 kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari wiki iliyopita.

Alisema si kosa wala fedheha kwa mjasiriamali au kampuni yoyote kupata mkopo kwenye taasisi za serikali au benki, lakini ni jambo la kusikitisha kuona watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri, hasa wale wa vyombo vya habari, wakiwa tayari kutumiwa na watu wachache wenye nia mbaya na taifa.

Mwenyekiti huyo katika kauli iliyoungwa mkono pia na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, aliyekuwa katika mkutano huo, alisema watu wanaoeneza taarifa hizo hawafanyi hivyo kwa bahati mbaya, bali wanataka kuona joto la walilopandisha la kutaka mafisadi wachukuliwe hatua kali za kisheria likizimwa.
Mbali ya Zitto, viongozi wengine wa CHADEMA waliokuwapo kwenye mkutano huo wa Mbowe kwa kile walichokielezea kuwa ni kuonyesha mshikamano wao kwa mwenyekiti wao, ni Makamu wa Mwenyekiti, Chacha Wangwe, Mbunge wa Mpanda Kati, Said Alfi, John Mnyika na John Mrema.

Katika hatua nyingine, Mbowe alisema wanasiasa wa upinzani wanaofanya biashara kama yeye, mara kwa mara wamekuwa wakilazimika kukabiliana na adha na vikwazo vya namna hii kimsingi vinavyolenga kuwakatisha tamaa.

“Kuna wakati, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye, alipata kusema kuwa mfanyabiashara yeyote atakayejiunga na CCM mambo yake yatamnyookea,” alisema Mbowe.
Akiigeukia NSSF, Mbowe aliilaumu kwa kutokujua uchungu wa kutafuta fedha kibiashara, hali aliyosema ndiyo iliyosababisha wataalamu wake kuendelea kuibana kampuni yake ambayo siku zote imefanya biashara kihalali.

“Mwizi na fisadi siku zote hajui uchungu wa fedha. Mimi sina kiwanda cha kuzalisha fedha, sitoi wala kupokea rushwa na kila fedha ninayotoa nahakikisha lazima iende kwa haki na kwa wale walioifanyia kazi…kinyume na hapo itakuwa ngumu kuipata fedha yangu.

“Mimi si mwendawazimu hata nikatae kulipa deni nililokopa. Nimekopa fedha kutoka katika benki mbalimbali kwa mamilioni, tena kiasi kikubwa kuliko kile nilichokopa NPF na nimekilipa. Kwa nini nishindwe kuilipa NSSF? Deni hili lina utata na hata leo katika gazeti la ‘The Citizen’ mkurugenzi wa NSSF amekiri kutojua kiasi hasa wanachotudai,” alisema Mbowe.

Kuhusu madai ya gazeti la ‘Rai’ kwamba yeye anaifilisi NSSF, Mbowe alisema kamwe shirika hilo haliwezi kufilisika kwa mkopo wa shilingi milioni 15 alizokopa, bali kutokana na mabilioni yaliyokopwa na wakopaji wanaotajwa na ripoti mbalimbali za mfuko huo ambao hawajawahi kutajwa, kushitakiwa wala kukamatwa.

Alipotakiwa kueleza ni kwa nini basi deni hilo halijalipwa kwa miaka yote hiyo, Mbowe alisema wakati wanakopa deni hilo mwaka 1990, hali ya kiuchumi hasa mfumuko wa bei vilikuwa vikipanda, hivyo mwaka mmoja baadaye walilazimika kuomba mkopo wa ziada kwa ajili ya kumalizia mradi huo wa Mbowe Hotels uliokuwa haujakamilika.

Alisema katika mazingira ya kushangaza, NSSF walikataa kutoa mkopo wa ziada kwa Mbowe Hotels Ltd, hata baada ya shirika hilo kukiri kuwa mradi huo ulikuwa ukihitaji fedha zaidi kukamilishwa.

Mwenyekiti huyo alisema kutokana na uamuzi huo wa NSSF ulioigharimu kampuni yake, walilazimika kwenda kukopa fedha hizo katika Benki ya CRDB walikopata mkopo ambao tayari wameshaulipa.

Kuhusu taratibu za ukopaji, Mbowe alisema ni jambo la kawaida kupitia na kutathimini upya mikataba ya biashara baina ya mkopaji na mkopeshaji, ili kuangalia mazingira ya biashara kulingana na uchumi wa nchi na mradi wa mfanyabiashara husika kama ambavyo Mbowe Hotels wamekuwa wakitaka ifanyike kila siku.

Alisema kutokana na kulitambua hilo, ndiyo maana wao waliamua kuwasilisha maombi ya kutaka kuongeza mkopo ili waweze kumaliza mradi waliokusudia, lakini hawakuweza kupata na badala yake wakafikishwa katika fedheha hii iliyofanywa kwa makusudi na kwa malengo maalumu.

“Ninaamini umakini wa utaalamu wa kibenki haukutumika katika maamuzi haya sambamba na mlolongo wa kushughulikia suala hilo haukuwa na dhamira njema, lakini pia ninahoji uwezo wa kitaaluma wa mfuko kujishughulisha na biashara ya ukopeshaji,” alisema Mbowe.

Alisema tangu mwaka 2003 wawakilishi wa Mbowe Hotels Ltd wamekuwa wakiwaandikia barua za kuwaomba NSSF wakubali mapendekezo ya kumaliza deni hilo. Juni mwaka jana, shirika hilo la umma lilikubali wito wa majadiliano ya kumaliza deni hilo, lakini hadi hivi sasa hawajaandika barua ya kuwataka kukutana na uongozi wa kampuni yake.

Katika kile alichokieleza kuwa ni mazingira ya ajabu, Mbowe alisema wakati mawasiliano yakiendelea, Januari 27, 2004, NSSF iliamua kwenda mahakamani kuomba wakurugenzi wa Mbowe Hotels Ltd wakamatwe kwa kushindwa kuheshimu amri ya kulipa deni, ombi lililokubaliwa.

Alisema Januari 8, 2007, mke wake alikamatwa na akapelekwa Mahakama Kuu Februari 20, mbele ya Jaji Amiri Manento ambako shauri hilo linaendelea.

Kama hiyo haitoshi, Mbowe alitumia mkutano huo kumponda Mwenyekiti wa taifa wa chama cha Sauti ya Umma (SAU), Paul Kyara, aliyekaririwa na gazeti la ‘Majira’ akitaka kukamatwa kwake (Mbowe) na wakurugenzi wenzake kwa kushindwa kulipa deni hilo.

Mbowe alisema Kyara alipata kuwa CHADEMA kama Mweka Hazina na baada ya hapo akatoka na kuanzisha chama chake cha SAU. Siku zote amekuwa akiendesha kampeni za kuwapinga kama alivyomwekea pingamizi mwaka 2005 wakati yeye (Mbowe) alipogombea urais na katika uchaguzi wa hivi karibuni wa Kiteto akasimamisha mgombea aliyefanya kampeni sambamba na CCM.
 
*Asema watakaoifilisi ni makada wa CCM

Na Said Mwishehe

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe, amekiri kudaiwa fedha na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), lakini akakana tuhuma kuwa mkopo aliochukua ndio unalifilisi shirika hilo.

Pia amesema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa kama NSSF itafilisika basi ni kutokana na mabilioni ya fedha yaliyokopwa na wakopaji wengine wanaotajwa na ripoti mbalimbali za kampuni hiyo ya umma, ambao hawajawahi kutajwa, kushitakiwa wala kukamatwa na ni makada wa CCM.

Bw. Mbowe alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi kuhusu deni analodaiwa na NSSF ambalo alilikopa mwaka 1990 kwa ajili ya upanuzi wa kampuni ya Mbowe Hotels Limited ya jijini, ambayo yeye ni mmoja wa wakurugenzi wake mkurugenzi mwingine akiwa ni Dkt. Lilian Mbowe ambaye ni mkewe.

"Naomba ifahamike, deni ambalo nadaiwa na NSSF haliwezi kulifisi shirika hilo, bali watu wanaoweza kulifilisi ni waliokopa mabilioni ya fedha na hawataki kurudisha. Wengi wamekopa katika mazingira ya kutatanisha na ukiwachunguza walio wengi ni makada wa CCM. Ndiyo maana aliyekuwa Waziri Mkuu wa Awamu ya Tatu, Bw. Frederick Sumaye, aliwahi kusema ukitaka biashara zako zinyooke, hamia CCM," alisema Bw. Mbowe.
Alisema kwa mujibu wa mchanganuo wa kitaalamu, deni la sasa linalodaiwa na NSSF kwa kampuni yake ya Mbowe Hotels Limited ambalo halihusiani na masuala ya siasa wala CHADEMA, ni sh. 43,169,227 ambazo zinatokana na riba ya mkopo aliochukua.

Alisema fedha hiyo ni kidogo kwa upande wake na si kwamba ameshindwa kulipa deni bali kinachotakiwa kwanza ni kufanyika kwa mazungumzo ambayo yatahakikisha haki inatendeka na hasa kwa upande wake na NSSF.

Akifafanua zaidi kuhusu deni hilo, Bw. Mbowe alisema kimsingi anadaiwa sh. milioni 15 ambazo alikopa mwaka 1990 kwa ajili ya shughuli za biashara na kwamba ameshazilipa ila deni lililopo sasa linatokana na riba ya mkopo huo.

Bw. Mbowe alisema hadi Juni 30 mwaka jana, kampuni yake imeshalipa jumla ya sh. milioni 75.5 ambazo kimsingi ni takribani mara tano ya kiwango cha fedha kilichokopwa na kampuni yake.

Aliongeza kuwa kampuni ya Mbowe Hotels Limited tangu mwaka 1996 imekuwa na nia ya kulipa deni hilo kwa kuandika barua kwa NSSF kutaka kukutana na kujadili suala hilo, lakini hadi sasa NSSF bado haijajibu barua hizo hivyo yeye na kampuni si kikwazo cha kulipa deni hilo, bali kikwazo ni NSSF yenyewe ambayo haitaki wakae na kuzungumzia suala hilo.

"Katika maisha ya biashara halali na ujasiriamali, kukopa ni jambo la kawaida. Utaratibu wa kupitia upya na kutathmini mikataba nalo ni jambo la kawaida kwa kila taasisi ya fedha inayojua wajibu wake na yenye nia njema. Mazingira ya biashara wakati wa michanganuo ya biashara hutofautiana kwa kiasi kikubwa na hali halisi hasa kutokana na udhaifu wa uchumi wetu hususan mfumuko wa bei," alisema Bw. Mbowe.

Aliongeza kuwa katika maisha yake ya biashara na uwekezaji kwa kupitia kampuni mbalimbali, aliwahi kukopa kwenye benki kadhaa kwa miradi inayotoa ajira kwa Watanzania wengi na kote huko amerejesha mikopo yote na hivyo alisisitiza kuwa ataendelea kukopa kwani ni njia muafaka kwake kujisaidia kimaisha.

Alisema mkataba wake na NSSF wa mwaka 1990 uligubikwa na mizengwe, kwani mwaka mmoja baada ya mkataba huo kusainiwa, aliomba kuongeza mkopo kwa ajili ya kukamilisha mradi lakini alikataliwa.

Bw. Mbowe alisema ataendelea kusimama katika haki hadi mwisho na yuko tayari kutumia gharama kubwa kuliko deni analodaiwa kuona uamuzi wa mwisho unakuwa wa usawa na haki.

Alisema kitu ambacho anakiona kwa sasa ni kuchafuliwa jina lake na chama chake kutokana na jitihada zao za kupambana na ufisadi katika maeneo mbalimbali ukiwamo wa EPA na Richmond.

Alisema pamoja na kuchafuliwa, bado atasimama imara kutetea maslahi ya Watanzania wote kwa kuhakikisha ufisadi unakwisha na yeye akiwa Mwenyekiti wa CHADEMA atahakikisha siku zote anapinga ufisadi.

Kuhusu Mwenyekiti wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Bw. Paul Kyara, kuilingia suala hilo alisema inawekezana kuna watu wanamtumia katika kulichafua jina lake na inawezekana hajui mlolongo mzima wa tukio hilo.

"Sitaki kuwa msemaji wa Kyara, lakini picha ninayoipata hapa ni kwamba anatumiwa na watu kwa ajili ya kuharibu jina langu na chama changu.

"Kyara amekuwa akifuatilia chama chetu katika mambo mbalimbali hata uchaguzi mdogo uliofanyika Kiteto hivi karibuni, kumtafuta mbunge wa jimbo hilo baada ya CHADEMA kusimamisha mgombea naye alisimamisha wake kwa lengo la kutupinga, hivyo unaweza kuona ni mtu wa aina gani," alisema Bw.Mbowe.

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa matatizo hayo, bado viongozi wote wa chama hicho wataendelea kumuunga mkono ili kuona haki inatendeka.

Pia alisema hayo yote ni katika kurudisha nyuma jitihada za kupambana na ufisadi, lakini wao wataendelea kuwa na msimamo wa kupambana na mafisadi wote na wananchi wawaunge mkono katika hilo.
 
Wakuu,

Hivi Mbowe si anasoma MBA Hull? Kama msomi wa MBA anaongelea huo mkopo kama anavyoongea Mbowe, basi hiyo course anayosoma haijaingia kichwani.

Karibu kila course ya MBA kuna financial strategy, na kwa mtu aliyesoma hilo somo, huwezi kusema amelipa deni mara tano ya mkopo na akaona ni sawa.

Labda kama na yeye anajua ila anaweka mambo ya siasa.


"Kwa mujibu wa maelezo yake, hadi Juni 30, mwaka jana kampuni hiyo ilikuwa imekwishalipa Sh milioni 75.5; kiasi ambacho ni mara tano ya kiwango cha mkopo."
 
Kila ukisoma case ya Mbowe inaonyesha mara nyingi tu alishindwa kulipa ontime. Kitu ambacho unatakiwa mtu kufanya ni kwamba hata ikitokea hivyo basi ni kuamkia bank na kuongea nao juu ya matatizo uliyopata, ili zile penalties zisifanye kazi. Lakini ukijikalia nyumbani, deni dogo utakuta limekuwa mabilioni.
Mtz, hivi alikopa kama Mbowe? Inaweza kuwa ni njia ya kummaliza kisiasa. Sipendi mimi watu wanaokopa bila kurudisha au kurudisha kwa kutegea. Mimi mambo ya finance sijui lakini sipendi kabisaaa bila kujali ni nani anafanya hivyo. Mbowe kama kapewa mkopo huo inabidi atufundishe wengine unapataje hiyo mihela twende tukachote NSSF kama yeye.

Kama kukopa pia ni ufisadi basi definition ya ufisadi ni pana kuliko uelewa wangu. Lakini kama suala ni yeye kutolipa deni na amechukua fweza zetu arudishe, hatukubali mpaka kieleweke. Sijafuatilia kwa kina lakini maandishi machache niliyosoma hapa na kusikiliza redioni (Clouds FM) inashangaza na wengi wanahisi kuna siasa katika hili. Mi sielewi mwenzenu eti
 
"Naomba ifahamike, deni ambalo nadaiwa na NSSF haliwezi kulifisi shirika hilo, bali watu wanaoweza kulifilisi ni waliokopa mabilioni ya fedha na hawataki kurudisha. Wengi wamekopa katika mazingira ya kutatanisha na ukiwachunguza walio wengi ni makada wa CCM. Ndiyo maana aliyekuwa Waziri Mkuu wa Awamu ya Tatu, Bw. Frederick Sumaye, aliwahi kusema ukitaka biashara zako zinyooke, hamia CCM," alisema Bw. Mbowe.

Alisema kwa mujibu wa mchanganuo wa kitaalamu, deni la sasa linalodaiwa na NSSF kwa kampuni yake ya Mbowe Hotels Limited ambalo halihusiani na masuala ya siasa wala CHADEMA, ni sh. 43,169,227 ambazo zinatokana na riba ya mkopo aliochukua.
Mtz, bac nimeelewa. Usinipe ufafanuzi zaidi. Loud and Clear. Labda kama ndiko kutapatapa kwake kujitetea. Lakini kama ni kweli kila kitu, bac mi nshajua 2
 
Mtz, hivi alikopa kama Mbowe? Inaweza kuwa ni njia ya kummaliza kisiasa. Sipendi mimi watu wanaokopa bila kurudisha au kurudisha kwa kutegea. Mimi mambo ya finance sijui lakini sipendi kabisaaa bila kujali ni nani anafanya hivyo. Mbowe kama kapewa mkopo huo inabidi atufundishe wengine unapataje hiyo mihela twende tukachote NSSF kama yeye.

Kama kukopa pia ni ufisadi basi definition ya ufisadi ni pana kuliko uelewa wangu. Lakini kama suala ni yeye kutolipa deni na amechukua fweza zetu arudishe, hatukubali mpaka kieleweke. Sijafuatilia kwa kina lakini maandishi machache niliyosoma hapa na kusikiliza redioni (Clouds FM) inashangaza na wengi wanahisi kuna siasa katika hili. Mi sielewi mwenzenu eti


Tina Mbowe kesha nieleza soma habari ziko hapa then tia akili uone lipi ni la kweli . Hapa kuna siasa kibao na si deni la mwaka 1990 .Walikuwa wapi kuandika kuanzia muda huo ?Alipoa 15m amelipa hadi sasa 75m unasemaje ?
 
Mtz, hivi alikopa kama Mbowe? Inaweza kuwa ni njia ya kummaliza kisiasa. Sipendi mimi watu wanaokopa bila kurudisha au kurudisha kwa kutegea. Mimi mambo ya finance sijui lakini sipendi kabisaaa bila kujali ni nani anafanya hivyo. Mbowe kama kapewa mkopo huo inabidi atufundishe wengine unapataje hiyo mihela twende tukachote NSSF kama yeye.

Kama kukopa pia ni ufisadi basi definition ya ufisadi ni pana kuliko uelewa wangu. Lakini kama suala ni yeye kutolipa deni na amechukua fweza zetu arudishe, hatukubali mpaka kieleweke. Sijafuatilia kwa kina lakini maandishi machache niliyosoma hapa na kusikiliza redioni (Clouds FM) inashangaza na wengi wanahisi kuna siasa katika hili. Mi sielewi mwenzenu eti

Tina,

Nakubaliana kabisa na wewe kwamba CCM wanatumia hili suala kutaka kumlima Mbowe ili naye aonekane ni fisadi. Lakini wa kulaumiwa au kujilaumu ni Mbowe mwenyewe. Unategemea kwenye siasa mtu akijua weaknesses zako atashindwa kuzitumia?

Msimamo wangu kwenye haya mambo ni kwamba ukifanya kosa wajibika na kosa lako na sio kuanza kulaumu wanaokuumbua kwa hilo kosa.

JF tunalaumiwa hapa mara nyingi kwa kutoa nyeti za wakubwa. Wasitulaumu sisi, wajilaumu wenyewe kwa makosa yao.
 
Hii strategy milyokuja nayo kundi la RA naona kali sana, baada ya kujadili kitu kinachoongelewa lazima atukanwe mbowe, je Dr. hamjapata deal zake nini?
Kama Mbowe amekopa anatakiwa kulipa kwa sababu dawa ya deni ni kulipa lakina RA ameajiri watu kibao hapa JF kuakikisha Thread zote zinajadili mbowe tu, mkianzisha kitu wanaingiza mambo ya mbowe, ili linatia shaka ndugu zangu maana hata kama unapinga huwezi kusema nonsense mtu mzima ili mradi watu wasiongelee kingine waongelee Mbowe kuweni makini ndugu zangu.
Yes kama mbowe amekopa alipe lakini use lugha nzuri wakati wa kuchangia.
 
Kati ya taasisi zilizojaa ufisadi,uzandiki,unafiki na udini NSSF inaongoza.Tukubali tusikubali hawa watu ndio wanaozifuja pesa za wastaafu bila kujali kwa kuingia mikataba ya mabilioni isiyokuwa hata na macho wala miguu kwa kigezo cha kuisaidia serikali na kujipendekeza kwa wenye nchi siku zao zinahesabika.Kwa hapa mimi silizungumzii tukio lililomtokea mtanzania,mfanyabiashara na mwekezaji mzalendo mwenye machungu na nchi jinsi wanavyomfanyia visa, hasha hao ndivyo wlivyo.Siku zao zinahesabika
 
Mimi bado nauliza hivi: Huyu bwana Mbowe amekopa hizo pesa au ameiba?

Ninavyoelewa mimi unapokopa kunakuwa na mkataba na unakuwa na masharti ya mkopo wenyewe na malipo yawe vipi na adhabu za kushindwa kutimiza masharti hayo na vipengele kadha wa kadha...Sasa hii biashara ya kudaiana magazetini na kupigiana kelele za wizi na ufisadi inatoka wapi kama sio mbwembwe za kisiasa tu? Labda mtu aniambie Mbowe kaiba hizo pesa hakukopa kama anavyotaka tuamini na kama ndio hivyo basi hapatatosha!
 
Mimi bado nauliza hivi: Huyu bwana Mbowe amekopa hizo pesa au ameiba?

Ninavyoelewa mimi unapokopa kunakuwa na mkataba na unakuwa na masharti ya mkopo wenyewe na malipo yawe vipi na adhabu za kushindwa kutimiza masharti hayo na vipengele kadha wa kadha...Sasa hii biashara ya kudaiana magazetini na kupigiana kelele za wizi na ufisadi inatoka wapi kama sio mbwembwe za kisiasa tu? Labda mtu aniambie Mbowe kaiba hizo pesa hakukopa kama anavyotaka tuamini na kama ndio hivyo basi hapatatosha!

Kwahiyo hata ukikopa lakini ukashindwa kulipa ni sawa? Jambo likifika mahakamani, magazeti yatalinasa tu.

Mbowe alipe hilo deni na aendelee na mambo yake. Kuanza kulaumu wengine huku kushindwa kulipa ni makosa yake mwenyewe, naona ni kupoteza muda wake bure.

Kama kuna makosa kwenye deni, kweli inachukua miaka kupata suluhu?
 
Back
Top Bottom