Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,502
156
Heshima Mbele,

Mbowe aifilisi NSSF

*Adaiwa milioni 1,200, hataki kulipa
*Atumia sheria kukwepa asifungwe
*Adai iliyokopa ni kampuni si yeye


na mwandishi wetu

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anakalia kiasi kikubwa cha fedha za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kukataa kulipa deni alilokopa.

Mbowe anadaiwa wastani wa sh milioni 1200 (sh bilioni 1.2), kutokana na deni alilochukua mwaka 1990 kwa nia ya kufanya upanuzi wa Mbowe Hotel ya jijini Dar es Salaam, maarufu kama Bilcanas.

Kwa kutumia mamilioni aliyokopa kutoka NSSF Machi 10, mwaka 1990, Mbowe aliweza kupanua Mbowe Hotel kwa kujenga mgahawa wa Hard Rock, kumbi za Bilcanas, Much More na Sugar Mama, ambazo amekuwa azitumia kwa ajili ya biashara tangu wakati huo.

Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa deni la mkopo huo aliouchukua kwa kutiliana saini kati yake na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NPF), ambalo baadaye lilibadilishwa jina na kuwa NSSF, sasa limekua na kufikia zaidi ya sh milioni 1200. Deni hili linatokana na mkopo aliouchukua na riba inayotokana na deni hilo.

Wakati wa kuchukua mkopo huo NPF (wakati huo) iliwakilishwa na Mustafa Mkulo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, huku Mbowe Hotel ikiwakilishwa Mbowe mwenyewe aliyetia saini. Pande zote mbili zilikuwa na mwakilishi mmoja. Mkulo kwa sasa ndiye Waziri wa Fedha.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo kati ya Mbowe na NSSF, ambayo ilichukua majukumu ya NPF, Mbowe Hotel ilikopeshwa sh milioni 15, mwaka 1990. Ibara ya 5, ya Mkataba wa Mkopo kati ya Mbowe Hotel na NSSF yenye vifungu 5.01, 5.02 na 5.03, iliweka bayana kuwa riba ya mkopo huo ilikuwa asilimia 31, na kwamba kila mwaka iwapo riba isingelipwa kwa wakati nayo ingetozwa riba ya asilimia 31.

Kifungu cha 6.01 na 6.02 cha mkataba wa mkopo huo kati ya Mbowe na NSSF vinaeleza kuwa Mbowe Hotel ilitakiwa kulipa deni hilo kwa mikupuo sawa mitano katika kipindi cha miaka sita. Mwaka wa kwanza wa mkopo Mbowe Hotel haikutakiwa kulipa kitu kwa nia ya kuipa fursa ya kujiimarisha katika biashara kwa mwaka wa kwanza.

Malipo hayo yalipaswa kufanyika kila ifikapo Desemba 31, kuanzia mwaka 1991, ambapo kila mwezi alistahili kulipa sh 3,000,000 kama deni la msingi na riba ya asilimia 31 kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba.

Wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Manase A. Mbowe, Freeman Aikaeli Mbowe na Dk. Lilian Mtei Mbowe, kwa sababu wanazozijua wao waliamua kuacha kulipa deni hilo bila mawasiliano ya aina yoyote na NSSF wala juhudi za wazi za kuonyesha nia ya kulipa hadi mwaka 1993, walipoamua kulipa sh 3,000,000 kati ya deni lote.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo, hadi mwaka 1993, wakurugenzi hao walistahili kuwa wamelipa wastani wa sh milioni 9,000,000 katika deni la msingi, lakini walikaa kimya hali iliyolitia wasiwasi shirika la NSSF.

Baada ya kutoa malipo ya sh 3,000,000, wakurugenzi hao walikaa kimya na ilipofika Septemba 1996, NSSF iliamua kufungua kesi Mahakama Kuu. Kesi hiyo ya madai No. 277 ya mwaka 1996, ilikuwa ikidai Mkopaji alipe deni la msingi sh milioni 12 zilizokuwa zimesalia pamoja na riba.

Hatua hii iliwafanya wakurugenzi wa Mbowe Hotel kuomba suala hilo walimalize nje ya Mahakama. Hata hivyo, hawakuendelea kulipa hadi mwaka 1998, walipopewa tishio la kufungwa jela ndipo waliamua kulipa kwa mkupuo sh milioni 12.

Hadi wanatoa malipo hayo, deni lilikwishakuwa na kufikia wastani wa sh milioni 145.38, na kimsingi makubaliano ilikuwa ni kwamba deni hilo lingelipwa katika muda wa miezi 24 tangua tarehe ya makubaliano.

Hata hivyo, Mbowe na wakurugenzi wenzake waliamua kutoendelea kulipa deni hilo badala yake wakaamua nao kuchukua mkondo wa kisheria kwa kutumia wahasibu kukokotoa tena hesabu za riba, bila mawasilianao na NSSF, na kisha wakachagua kiasi wanachotaka kulipa wao.

Mbowe Hotel ikitumia kampuni ya uwakili ya Nyange, Ringia & Co., walifanya kazi ya kuwasiliana na wahasibu mbalimbali kisha kuwasiliana moja kwa moja na wakili wa NSSF, Ademba Gomba, kutaka deni la riba lipunguzwe.

Mgogoro na mvutano kati ya Mbowe Hotel uliendelea, huku riba ya deni nayo ikizidi kuongezeka na ilipofika Oktoba 11, 2002 Meneja wa Fedha wa Bilcanas Group Inc, Godbless Naftal, kupitia barua yake yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL02/02/01, alikokotoa hesabu na kutaka wakurugenzi wa Mbowe Hotel walipe wastani wa sh 31,959,369.86, kwa maelezo kuwa kanuni iliyotumiwa kukokotoa riba ilikosewa.

Januari 16, 2003 NSSF kupitia kwa Mussa S. A. kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alimjibu Naftal kwa barua yenye Kumb. No. NSSF/LA/F.131/10/89/135, akimweleza kuwa NSSF imekataa mapendekezo yake (Naftal) na hivyo wanapaswa kulipa deni lote kwa mujibu wa hukumu ya za Mahakama Kuu za mwaka 1999 na 2001.

NSSF na Mbowe Hotel waliendelea kupigana ngwala mahakamani na kwenye bodi za usuluhishi hadi ilipofika Oktoba, 2006 ambapo Jaji Manento alihukumu wakurugenzi wa Mbowe Hotel watiwe mbaroni na kufungwa jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya mahakama ya kulipa deni lao.

Wakili wa Mbowe Hotel, Herbert Nyange, aliwasilisha katika Mahakama ya Rufaa hati ya kiapo ambayo muhuri wake umegonjwa Oktoba 30, 2006 akipinga wakurugenzi wa Mbowe Hotel kukamatwa kwa maelezo kuwa Mahakama Kuu ilikwenda nje ya mipaka kisheria kwa kutaka wakurugenzi wakamatwe.

“Uamuzi wa amri ya kukamatwa kwa walalamikaji (wakurugenzi wa Mbowe Hotel) ulifikiwa kwa misingi ya wazi ya uvunjaji wa kanuni juu ya wajibu wa wakurugenzi dhidi ya deni au uamuzi dhidi ya shirika, hivyo ni kinyume na sheria,” alisema Nyange katika barua hiyo ya kupingwa kukamatwa kwa akina Mbowe.

Hata hivyo, kutokana na Mbowe kuona mambo yanaendelea kuchacha, Desemba 14, mwaka 2006, mmoja wa wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Dk. Lilian Mtei Mbowe, aliamua kutoa malipo ya wastani wa sh milioni 50 kwa NSSF kwa hundi mba 298492, iliyoambatana na barua yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL06/01, huku akitaka warejee kwenye meza ya majadiliano badala ya kufungwa jela.

Barua hiyo pia iliomba NSSF irejee barua ya Kampuni ya Ushauri wa Fedha ya Morgan cKlien Associates iliyoteuliwa na Mbowe mwaka 2004 kushiriki majadiliano na usuluhishi juu ya jinsi ya kulipa deni hilo.

Kampuni hiyo iliyokuwa chini ya Afisa Mtendaji Mkuu, Hubert Mengi, ilitoa maelezo mengi yenye kuonyesha kwa nini Mbowe Hotel ilishindwa kulipa deni lake kwa wakati. Anasema katiak moja ya vielelezo kuwa fedha zilipotolewa na NSSF mwaka 1990, nchini Tanzania hakukuwapo vifaa vya ujenzi.Mengi anaeleza kuwa Mbowe Hotel walilazimika kuagiza vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi, na lilijitokeza tatizo lingine kwamba benki nchini hazikuwa na fedha za kigeni, hivyo Mbowe Hotel ililazimika kusubiri kwa muda mrefu kupatiwa fedha hizo za kigeni.

Kwa maelezo hayo, anasema Mbowe Hotel walichelewa kupata vifaa na mradi ukashindwa kukamilika kwa wakati hali iliyosababisha wakurugenzi wake washindwe kulipa deni hilo kwani walikuwa hawafanyi biashara.

Baada ya mivutano yote hiyo, Mbowe Hotel wamealikwa kwenye NSSF kujadili jinsi ya kulipa deni hilo linaloendelea kukua lakini hadi jana vyanzo vyetu kutoka NSSF vilionyesha kuwa wakurugenzi wa Mbowe Hotel wameamua kukaa kimya.

Kutokana na hali hiyo, ni wazi NSSF inaendelea kupoteza mapato yake yanayokaliwa na wakopaji wa aina hiyo, ambapo mwenendo usipodhibitiwa shirika linaweza kufilisika sawa na ilivyotokea kwa mashirika mengi nchini


=======
UPDATE:

Jan 31, 2011:
NOTICE OF APPOINTMENT OF RECEIVER/MANAGER

Notice is hereby given to the general public that I, Charles Rutayuga Burchard Rwechungura of CRB Africa Legal, Dar es Salaam, was appointed by the National Social Security Fund ("NSSF") to Receiver/Manager of the Mbowe Hotel Limited (the "Company") effective from 25th January 2011

Linaendelea hivo hilo tangazo kwenye gazeti la Mwananchi la leo. Freeman ameshindwa kuwalipa hawa jamaa au? Tungemkabidhi Nchi mwaka 2005........!

May 26, 2014:
Wadau, baada ya kipindi cha Maswali na Majibu, kulikuwa na miongozi ya Wabunge kwa Naibu Spika. Moja ya hoja zilizojitokeza ni madai ya Lissu kuwa Wabunge wa CCM wanachukua fedha kutoka kwenye mifuko ya jamii.

Hata hivyo, waziri Gaudensia Kabaka alisema kuwa si kweli kuwa wabunge wanaenda kuchukua fedha kwenye mifuko ya kijamii na kuweka mfukoni mwao bali wanaomba fedha kwenye mifuko hiyo kwa ajili ya maendeleo kwenye majimbo yao.

Alisema kuwa ni wabunge wa CCM ndio wanaojitokeza kuomba kwa ajili ya majimbo yao jambo ambalo amesema kuwa ni jema. Anawashangaa wabunge wa upinzani kulalamika kuwa wabunge wa CCM wanaomba fedha kwenye mifuko yao ilhali wao hakuna anayewazuia kuomba.

Kibaya zaidi waziri Kabaka alisema ni pale Mbunge ambaye anajitokeza kukopa fedha kwenye mifuko hiyo na akakaa na deni kwa muda mrefu hali inayomfanya awe kwenye risk ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka. Alisema kuwa kuna kiongozi mmoja wa upinzani ambaye amekopa fedha nyingi NSSF na mpaka sasa anakwepa kulipa.

Katika majibu ya nyongeza, Waziri wa TAMISEMI, HAWA GHASIA alimtaja mtu huyo kuwa ni Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani ambaye alikopa kiasi kikubwa cha fedha (kiwango hakikubainishwa) na mpaka sasa hajalipa na haoneshi nia ya kulipa hivyo kujiweka kwenye uwezekano mkubwa wa kukamatwa
 
Nafikiri mikopo ya kibiashara iliyowazi na ina riba kama hii hatuna shida nayo.Wasiwasi ni ile ya siri siri kama zile milioni 50 alizopewa Sumayi wakati ule.
Mkopo unakuwa wa siri na hata riba hakuna ili hali hizo ni fedha za umma. Kuuita mkopo huu wa Mbowe "ufisadi" ni kupotosha maana ya neno lenyewe.
 
Lowassa alishasema "kama tukianza kuchafuana sidhani kama kuna Mwanasiasa anayeweza kubaki".hii kauli inaonesha ni jinsi gani wanasiasa walivyo wachafu.

Haya ni wakati Mbowe kuja hapa na kujibu tuhuma hizi!
 
sidhani kama hii ni hoja ya kujibiwa maana hili ni suala kibiashara kati ya mbowe na nssf na kama tayari kesi iko mahakamani sijui wewe mwenye hoja hii unataka mbowe akujibu kama hakimu au jaji? naomba ulete hoja zenye kujadilika usituletee umbea wa kiswahi ktk jf na kama huna hoja ni bora ukakaa kimya kuliko kutuletea hoja zisizo na kichwa wala miguu
 
sidhani kama hii ni hoja ya kujibiwa maana hili ni suala kibiashara kati ya mbowe na nssf na kama tayari kesi iko mahakamani sijui wewe mwenye hoja hii unataka mbowe akujibu kama hakimu au jaji?

Mkuu Meja kumbe ukishikwa pabaya huwa unakuwa hivi?,Hili si lina mslahi ya taifa??Mbona suala la Lowassa na RDC nalo lilikuwa sula la kibiashara kati ya Lowassa na RDC?Mbona suala la Mzindakaya na kukopeshwa na Bank lilikuwa kati yake na Bank Kuu??Je haya Hayafananani??Mbona watu walikuja juu.Tafuta Jibu lingine na usilete usanii..

Sheikh yahay alkishamsema huu ni mwaka wa kujua mengi yaliyofichwa,na tutasikia mengi tu!

naomba ulete hoja zenye kujadilika usituletee umbea wa kiswahi ktk jf na kama huna hoja ni bora ukakaa kimya kuliko kutuletea hoja zisizo na kichwa wala miguu
unataka tulete hoja za kumtetea Mbowe tu au unataka zipi?tukubali na mambomengine ambayo yanaweza kuwa ya Msingi.Ndio siasa hiyo!!

Mie nataka kujua ni kwasabu zipi Mbowe alipi hiyo pesa??na sina kulinganisha hili na suala la ndanda na Mzindakaya si kuwatetea ni wema ili naangalia uhalisia wa mambo haya.

Lowassa na Mbowe washitakiwe kwa hili
 
sidhani kama hii ni hoja ya kujibiwa maana hili ni suala kibiashara kati ya mbowe na nssf na kama tayari kesi iko mahakamani sijui wewe mwenye hoja hii unataka mbowe akujibu kama hakimu au jaji? naomba ulete hoja zenye kujadilika usituletee umbea wa kiswahi ktk jf na kama huna hoja ni bora ukakaa kimya kuliko kutuletea hoja zisizo na kichwa wala miguu...acha hizo, recently imekuwa ngumu ku-ignore hoja zinazoelekezwa huku dhidi ya Mbowe(zimezidi kwa kweli), however si lazima ajibu hapa JF ila ni wajibu wake kufanya clarification hata kwa kifupi tu kupitia media au njia nyingine yeyote tu!! yeye ni public figure kama alivyo kiongozi wa chama chochote cha siasa Tz!
 
Dawa ya deni ni kulipa! Sasa kama Mbowe alikopa alipe! period!

ila ukiangalaia toka Mwaka 1996 wameombwa walipe deni ila hawajaonesha ushirikiano.Na kama ni hivyo basi na watu waliochukua za EPA warudishe bila kushtakiwa kama mtakavyo Mbowe asishitakiwe.

Suala la pili tunata kujua mazingira ya Mbowe kupewa mkopo NSSF,Je kulikuwa na Fair Game au ??hili ni suala ambalo tunahitaji kulijua.

though Mwandishi hakuupa upande wapili utoe Maelezo,ila tunahitaji kufahamu vizuri suala hili.tuseianza kuupanda Upinzani kumbe ndio hao hao!!
 
Hii MIKOPO ya BENK, NSSF itatuuwa!!! Riba 31% mbona hatari?

Samahani hivi Riba NSSF bado ni hiyohiyo au imepungua sasa?

Nini Tofauti ya MKOPO wa BENK na MKOPO wa NSSF.
 
Kwa maneno mengine Mbowe ni fisadi?

Kibunango maana ya Fisadi ni hii hapa

Fisadi ni mtu mbaya,mtongozaji,mharibifu,mpotevu, mwasherati, kama vile guberi!

Je unadhani Mbowe si Fisadi?
 
Ulimwenguni kote matajiri wanakopa.Hukusoma hata H CLINTON kakopa? Hii si hoja.Tunataka tuambiwe kachota kinanma ya ufisadi.Mbowe amekopa ,akaahidi kulipa.A VERY open and transparent busines deal.Unalinganishaje na ufisadi wa RICH-MONDULI ah sorry RICHMOND.You are not serious. Tuwe makini na deception kama hizi,they are just decoys to divert agenda ya UFISAAADI !!
SORRY TUNAFAHAMU KUSOMA NA KANDIKA.Unayejaribu kutuyumbisha ulaaniwe.
 
Ulimwenguni kote matajiri wanakopa.Hukusoma hata H CLINTON kakopa? Hii si hoja.Tunataka tuambiwe kachota kinanma ya ufisadi.Mbowe amekopa ,akaahidi kulipa.A VERY open and transparent busines deal.Unalinganishaje na ufisadi wa RICH-MONDULI ah sorry RICHMOND.You are not serious. Tuwe makini na deception kama hizi,they are just decoys to divert agenda ya UFISAAADI !!
SORRY TUNAFAHAMU KUSOMA NA KANDIKA.Unayejaribu kutuyumbisha ulaaniwe.


Mie sitaki tulinganishe na suala la Ndanda,ila tuhusishe na suala la Mzindakaya na hili.Kwanini Mbowe akiguswa watu CHADEMA huwa hawajitokezi kuliongelea???
 
Hii MIKOPO ya BENK, NSSF itatuuwa!!! Riba 31% mbona hatari?

Samahani hivi Riba NSSF bado ni hiyohiyo au imepungua sasa?

Nini Tofauti ya MKOPO wa BENK na MKOPO wa NSSF.
Asante sana mkuu CHUMA,
Mimi naona hilo ndio suala la msingi kabisa kulijadili na pengine kugoma kulipa MPAKA KIELEWEKE alikofanya Bw.Mbowe ndio kutatuzindua juu ya ukweli kama viwango vya RIBA katika mabenki ya Bongo na hiyo mifuko yetu ya jamii kweli vinaweza kufanya mikopo hiyo ikawasaidia wananchi kujiinua kiuchumi au ni wizi wa mchanamchana?
Mbowe hastahili kutetewa kama hana sababu za kutolipa deni hilo.Lakini narudia tena ,kumwita Fisadi mtu aliyefuata utaratibu wa wazikabisa kukopa fedha na aka chelewa kulipa ni upotoshaji wa maana ya neno lenyewe, Au ni kujiridhisha tuu kwa baadhi ya watu kuwa "Tunajibu mapigo"
Mafisadi ni wale wanaotumbua fedha zetu kwa siri wakiulizwa wanakataa katakata, mpaka serikali iunde tume na kutumia fedha zingine nyingi kufichua yale waliyokataa ndio kwa shingo upande wanajiuzulu au kuingia mitini.
Tukubali ukweli.
 
Huyu anadaiwa kihalali na alikopa mchana kweupe 1990.
Wale waliokopa miaka iliyofuatia bila interest na hawalipi mbona majina yao hayapo hapa?

Hivi hili deni lilikuwa linasubiri aseme ndipo litolewe?

Naona kuna kila aina ya Hila za Mzee fisi kwenye hili.

Mimi kwngu sioni shida kuhusu hilo deni.

Club ya Bilicanas ipo pale na makaratasi yote ya mkataba wanayo sasa wanasubiri nini?

Hiyo kitu ni Ufisadi kweli au imelazimishwa?
 
Naamini deni hili ndilo lililomfanya afeli chuo kikuu-Hull.
Mwanakijiji a.k.a Mwafrika wa kike leo una kibarua kigumu cha kutetea UFISADI wa mwizi wa kuaminika bwana Mbowe.
 
Huyu anadaiwa kihalali na alikopa mchana kweupe 1990.
Wale waliokopa miaka iliyofuatia bila interest na hawalipi mbona majina yao hayapo hapa?

Hivi hili deni lilikuwa linasubiri aseme ndipo litolewe?

Naona kuna kila aina ya Hila za Mzee fisi kwenye hili.

Mimi kwngu sioni shida kuhusu hilo deni.

Club ya Bilicanas ipo pale na makaratasi yote ya mkataba wanayo sasa wanasubiri nini?

Hiyo kitu ni Ufisadi kweli au imelazimishwa?

Na kweli!

Hawa jamaa kwa nini hawamkamati toka 1990? Wanaogopa nini? Mbona 2005 wakati wa kugombea urais hawakumkamata? Mbona wanatoa maagizo ya mahakama bila ya kuyatekeleza? Wanajua sheria iko upande wake, wanatoa tu matamko ya kuyatumia kisiasa. Kwa nini hawakamati mali yake bilicanas?

Huu ni mkakati wa Rostam wa kuonyesha kuwa pamoja na yeye kuanza kurejesha hela za Kagoda, asikamatwe. Kumbe tofauti yake na Mbowe ni kuwa Rostam alighushi nyaraka na kuiba BOT, Mbowe alikopa na kuna mgogoro kuhusu kiwango cha malipo.

Hapa fisadi Rostam ujue umeshindwa; Balille anakupotosha kama alivyompotosha Lowassa ajitokeze na kujisafisha. Kampeleke tena Hull akajifunze spinning.

Siku zako zinahesabika, ni ama tutakupeleka Segerea au utatoroka kurudi nchi yako ya mapateli matapeli

Asha
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom